Tanzanian priest
New Member
- Jul 24, 2022
- 1
- 0
Habari Yako mpendwa msomi, natumai uhali njema. Nataka nitumie fursa hii kukupa muangaza ya mengi wanayopitia vijana wenzangu kwani mengi yanaumiza na kusikitisha. Natumai mwisho wa makala hii utapata kujua mazingira yanayomzunguka kijana katika uchumi unaodoroda na maamuzi magumu anayoyachukua kijana huyu kuhakikisha anapata fedha za kujikimu ama mlo wa siku.
Maporomoko ya kiuchumi ni Mfumuko wa bei za bidhaa kuwa ghali ilhali kipato Cha kujikimu Bado kipo duni. Hali hii inapelekea wengi washindwe kununua bidhaa na baadhi ya mahitaji Yao ya Kila siku. Kwamfano sabuni, dawa za meno, sukari, mchele n.k ,na vijana wengi wamekamatwa katika wimbi hili la poromoko la kiuchumi.
Vijana wanaozunguka jamii yangu hawana ajira maofisini, wengi wameishia elimu ya kidato Cha nne au shahada ya chuo kikuu. Vijana wengi wamejikita kwenye biashara ndogondogo wengi wao wakikimbilia kua madereva bajaji na bodaboda. Asubuhi zinakuwa ngumu Kwa vijana Hawa wanaogombana na abiria Kila kukicha kuhusu kupanda Kwa bei za nauli, abiria ambao hawapo tayari kulipa nauli kubwa kwani nao Hali kiuchumi Bado ni ngumu.
Vijana Hawa wanalazimika kukubali nauli ndogo licha ya kuwa mafuta ya kuendesha bajaji na bodaboda zao yanapanda bei kila wiki panapo kucha. Na Kama haya yote Bado hayawatoshi wanasemwa na kutukanwa na watu wa sheli Kila asubuhi wanapopanga foleni ndefu ya kugombania mafuta ...amaa kweli msiba usikie Kwa mwenzio, vijana Hawa wamepewa barabara duni za kutumia kwasababu idadi Yao ni kubwa sana kutumia kwao barabara nzuri kungetengeneza msongamano wa magari barabarani hivyo wanalazimika kutumia barabara chakafu. Na wengi wenye lengo la kudumisha vyombo vyao vya usafiri Kwa kutumia barabara nzuri huishia kupelekwa kituo Cha polisi. Hali inayowafanya wengi wabaki kwenye umaskini.
Siku hizi kumekuwa na ongezeko la matapeli wa mitandao wengi hupigiwa simu ama hutumiwa ujumbe dhumuni kuu wakidai kutaka hela, Kwa wenye hasira Kali vijana Hawa ni wahuni na wanahitaji kuadhibiwa ila Kwake yeye kijana hii ni fursa ya kupata mlo Kwani hana chanzo Cha ajira kwenye uchumi huu unaoshuka Kwa Kasi ....je kijana huyu aadhibiwe Kwa kujipa ajira ya utapeli au lah jamii ivae viatu vya kijana huyu na kutafuta suluhu la ajira ? Swali hili naomba nikuachie wewe ndugu msomi.
Acha nihamie kwenye jinsia ke, jinsia inayofanya maamuzi magumu Kwaajili ya kujikimu kwenye Hali hii ya kiuchumi, mnamo wiki hii kumekuwa na taarifa ya wanafunzi wa darasa la sita chini ya umri wa miaka kumi na mbili wakiwa wamekamatwa kwenye biashara ya uuzaji wa miili Yao yaani ukahaba na wengi wao walipoulizwa kwanini wamejiingiza kwenye biashara hii walijibu ili waweze kujikimu.
Wakati Mimi darasa la sita nilikuwa nawaza jinsi ya kufaulu mtihani wangu wa mchujo Ili nisirudie darasa watoto hawa wanawaza namna za kujikimu kimaisha. Uchumi unaanguka na unaanguka na kizazi chetu, Kama binti wa chuo kikuu naweza kuwa shuhuda wa maisha ya wasichana wengi wanaonizunguka . Hupati kitu bila kutoa kitu ndio mfumo wa maisha ya chuo na hivi sasa mfumo huu ndio unaoshamiri katika maisha yetu ya Kila siku wasichana wengi wanajiingiza kwenye mahusiano ya muda mfupi Ili mwenza wao aweze kuwahudumia mahusiano ya kidumu basi heri huyo ni wandoa ila yanapoisha basi alhamdulillahi hujulikana Kama mfadhili.
Tupo katika uchumi unaoshuka, vitu vinapanda bei Kila panapo kucha, ajira hamna za kutuajiri vijana, wachache wanajishughulisha na biashara ndogondogo ambazo haziingizi faida nyingi kutokana na Kodi na makato. Vijana tunashindwa kukopa kwani riba zipo juu sana mahitaji yetu ni mengi kushinda hata bidhaa zilizopo, na bidhaa ambazo zipo zinabei kiasi tunashindwa kununua, shida zetu zilizojaa zinapelekea vijana wengi waangukie kwenye mkumbo wa ujabambazi na utapeli, Jana rafiki yangu alinisimulia alivyoibiwa kweupe machoni mwa watu, hawakuwa wazee waliomuibia Bali vijana wenzio waliomshikia mapanga na kumdai fedha ,wakichukua Kila alichonacho, tukio hili limenifanya niwaze je? Uchumi wetu unaoshuka unachochea matukio ya kihalifu Kama haya? Au la ni ulimbwende wa vijana?
Kwakweli maisha ni magumu na uchumi unashuka na vijana wanaumia zaidi inasikitisha kuona vijana wengi wakianguka, ndoto zao zikiishia katikati na wenyewe wakianguka mkumboni ,mkumbo mchafu unaochochewa na Hali mbaya ya uchumi ,ila je ni sahihi kulaumu uchumi tuu? vitu vinapanda bei na fursa mpya za kazi ni finyu, ila Hali hii haimaanishi hakuna kazi.
Ningependa nishauri serikali, mashirika binafsi, jamii na vijana wenzangu kiujumla ; tunahitaji kuangalia vijana Kama taifa la kesho taifa ambalo lisiposaidiwa Leo halitapata nuru ya kuiona hiyo kesho elimu za kujikimu zinahitaji zihamasihwe Tena, Ili tupunguze hili wingu kubwa la wasio na ajira, vijana wanahitaji kupewa fursa maofisini kwani Kuna wengi wenye ujuzi ambao unaweza kulisaidia hili taifa lakini hawana ajira, kubwa zaidi Kama jamii tunahitaji tutatue hiki kimbunga ,kimbunga kinacho haribu uchumi wetu ,tutawezaje? Kwa kuendelea kufanya kazi.
Kama mwanafunzi wa uchumi naweza kusema Kwa hakika hakuna uchumi Bora,kosekano la ajira halitatokea kuondoka, ukweli ni kwamba Ili mizani ya uchumi iwe sawia Kutakuwa na wenye ajira na wasio na ajira ,uchumi utapanda na utashuka ila Kama jamii ikijikita katika sekta zote za uzalishaji tatizo hili linalowakumba vijana litatatuliwa Kwa kiasi chake. Pia Kama vijana tunahitaji kujifunza kutengeneza fursa tuupunguzie mzigo serikali na jamii yetu.
Asante kwa kusoma makala hii Kama umejifunza lolote kupitia makala hii tafadhali sambaza Kwa mwengine Ili nae apate kujua. Usisahau kuipa kura Yako makala hii kwani utakuwa unamuunga mkono kijana mwenzako na vijana wengine wengi katika jamii Yako.
Asante.

Upvote
1