Jinsi vyakula tulavyo vinavyotumaliza

Mkuu, kwanza tambuwa kuwa HATULI CHAKULA KWA SABABU NI KITAMU MDOMONI, bali ni kwa sababu tunajuwa hiki chakula ninachokula kinaenda kufanya nini mwilini, FULL STOP. Kinaweza kuwa kichungu sana mdomoni lakini kina faida kibao mwilini, mimi nitakula tu maana kikishapita mdomoni kazi imeisha!.

Kwa upande wa dona, mimi huwa nachanganya mahindi na ngano kisha naenda kuvisaga kwa pamoja mashineni kwa uwiano wa ngano nusu kilo na mahindi kilo 1, unga wake unakuwa laini mzuri ukipika ugali unakuwa mzuri hauwi unaonekana vibayavibaya au usio na radha,kwa staili hii unaweza kula na mboga yeyote hata kama ni maharage. Ukitaka nikutumie kilo 1 ya unga huu halafu uniambie kama hujaupenda.

Jaribu kupata multivitamins tablets nzuri kila umalizapo kula chakula umeze 1, vidonda mdomoni vitakoma,pia pata asali nzuri kila siku unapoenda kulala kijiko 1.

Japo nikiri, mie muumini wa ugali mweupeee tena nataka mahindi yalowekwe kwanza. Dona halishuki asilani. Na chapati za atta zinanishinda, nimefanikiwa tu kwa kupenda kutumia brown rice.
 
Kuhusu MAJI, si vibaya SANA kunywa ya dukani, si vibaya sana. LAKINI MI NASHAURI MAJI YALIYOCHUJWA TU/FILTERED KWA KITAMBAA AU FILTER YA UMEME NDIYO TUYANYWE ZAIDI, Kama ni ya bombani ukishayachota yaache kwenye jagi lililowazi kama nusu saa ndipo uyanywe maana siku hizi kuna dawa zinaongezwa ambazo huyatibu maji lakini hupelekea maji yasiwe na radha nzuri.

 
kwa kifupi afya zetu ziko matatani sana leo hii vijana wengi tunamagonjwa ya kila aina. Lakini tatizo nikuacha vyakula vyetu vya asili babu zenu walikuwa wanaishi muda mrefu leo hii ukikutana na kijana wa miaka 40 ni mzee. tubadilikeni jamani hata kama watasema wewe ni mshamba kubaline tu ushamba lakini mwili unakuwa na afya njema
 
yaani nimeipenda kweli mada hii lakini sasa dah yaani vyote vilivyosemwa havifai mimi ndio muumini wake jamani mbona maisha yanakuwa magumu hivyo? chips ndio nyumbani, soda ndio kabisaa maana huwa situmii pombe nyma choma sasa dah hapo penyewe, ule ugali wa sembe ulinishinda kwa kweli, nilinenepa vibaya nikaonekana kama simtank nikaenda kwa doctor akaniambia dawa pekee ni mazoezi nilianza mazoezi mwaka mzima na nikapunguza kula hayo mavitu nikawa slim kabisa watu wakaanza kusema mngonjwa mwezi huu nimeanza tena kuona uvivu wa mazoezi naona hali inatakiwa kujirudia, dah maisha nayaona magumu kweli aisee
 
JINSI VYAKULA TULAVYO VINAVYOTUMALIZA - 6




VYAKULA vinavyotumaliza na tutazungumzia vitafunwa; endelea.

Hali hii haiko kwenye mkate peke yake, bali iko karibú kwenye vitafunwa vyote ambavyo ndivyo vyakula vikuu vya familia nyingi nchini. Vitafunwa hivyo ni pamoja na chapati, ‘skonzi' ambazo nazo hutengenezwa kutokana na ngano iliyoondolewa virutubisho vyake baada ya kukobolewa. Utaona ni jinsi gani tuko hatarini kwa kupenda kula kila siku vyakula vinavyotuangamiza.
​


Katika hili, tunashauriwa kula mkate unaojulikana kama ‘mkate mweusi' au ‘Brown Bread', wenyewe kidogo una nafuu kutokana na kutengenezwa na ngano isiyokobolewa na huwa haiongezwi sukari au makorombezwo


mengine. Ingawa kwa ladha mkate huu siyo mzuri mdomoni, lakini kiafya ni bora na mzuri uingiapo tumboni
kwa sababu una kamba lishe za kutosha.


Halikadhalika, wanaopenda kula chapati, maandazi na sikonzi, wanashauriwa kutumia unga wa ngano isiyokobolewa ili kujiepusha na madhara yatokanayo na ulaji wa nafaka zilizokobolewa. Tupende kuthamini




sana vyakula vyenye faida mwilini hata kama havina ladha nzuri mdomoni, kuliko kupenda kula vyakula vyenye ladha nzuri mdomoni lakini vyenye madhara tumboni.

STAILI HII YA MAISHA NDIYO SABABU ZA WEWE KUUGUA MARA KWA MARA


Baada ya kuelezea aina ya vyakula tunavyopenda kula na kuona namna vilivyo hatari kwenye miili yetu, hebu tuangalie staili ya ulaji ya baadhi ya watu kuanzia asubuhi hadi mlo wa usiku, kila siku na kwa maisha yao yote.
Usemi usemao kuwa ‘jinsi ulivyo, kunatokana na unavyokula', una maana kubwa. Baada ya kuangalia ratiba hii utaweza kujijua uko kundi gani na pia utajua kwa nini hali yako ya kiafya ni dhaifu.

Wako baadhi ya watu na ndiyo familia nyingi, huanza asubuhi kwa kutia tumboni vyakula ambavyo siyo tu havina viini lishe au virutubisho vyovyote, bali vyenye hatari kwa ustawi wa afya zao.



Mfano, unaamka asubuhi huku kitu cha kwanza kuingia tumboni mwako kinakuwa chai ya rangi iliyoungwa kwa vijiko vitatu mpaka vinne vya sukari, kitafunwa ni mkate, chapati au maandazi. Baada ya kunywa chai, pengine unashushia na soda au juisi za rangi.


Mchana unawadia, unakula ugali wako uliopikwa kwa unga wa sembe nyeupe na nyama. Wengine mchana watakula wali wa pilau ya nyama ya ng'ombe na baada ya mlo watasindikizia na soda. Au wengine watakula chips kuku au mayai. Vyote ni vya kuku wa kizungu.


Awamu ya mwisho inakuwa ni mlo wa usiku, ambao nao kwa aliyekula ugali mchana, labda usiku atakula wali na aliyekula wali pengine ataamua kubadili kwa kunywa chai na mkate mweupe au chai na chapati, au kurudia tena chips mayai.


Kwa zile baadhi ya familia zenye kipato, asubuhi huweza kuanza kunywa chai ya maziwa yenye sukari mpaka ya ‘kujilamba' ikisindikizwa na mayai ya kukaanga kwenye mafuta kibao, na kisha kushusia na juisi ya boksi. Mchana ukapita kwa kula pilau ya kuku wa kizungu na kushushia na bia na usiku labda ukala chapati na mchuzi


wenye mafuta kibao na mapochopocho mengine ya kukaanga kisha kushushia na ka mvinyo kidogo.
Kwa mtizamo wa kawaida, utaona ulaji wa vyakula vyenye mafuta, sukari nyingi na vilivyonona ndiyo maisha bora, lakini kwa upande mwingine ulaji wa vyakula vya aina hiyo huwa ndiyo chanzo kikuu cha maradhi hatari ya moyo, saratani, kisukari na unene wa kupindukia.



JINSI VYAKULA TULAVYO VINAVYOTUMALIZA - 7




WIKI ninaendelea kuelezea namna vyakula tunavyokula kila uchwao vinavyotumaliza kwa kujua au pasipo kujua. Tuwe pamoja.
Katika milo yote hiyo, mtu huyu hajala tunda la aina yoyote wala hajala mboga yoyote ya majani. Mbaya zaidi, siku nzima inaweza kuisha bila kunywa maji hata glasi moja. Kwa sababu kila amalizapo kula au asikiapo kiu, hunywa soda, bia, mvinyo au juisi iliyotengenezwa kwa kuchanganya rangi za ladha mbalimbali.

Ingawa chai, chapati, ugali mweupe, nyama, soda na juisi zilizotajwa hapo juu siyo sumu, lakini vyakula hivyo havina virutubisho vyovyote mwilini, ukiacha chai tu. Vyakula hivyo havina faida mwilini kwa sababu virutubisho vyake


vilishaondolewa wakati wa matayarisho yake, kama vile unga wa sembe nyeupe, mkate mweupe na chapati zilizopikwa kutokana na ngano iliyokobolewa.


Halikadhalika soda na juisi za kutengeneza hazina virutubisho kwa sababu ni mchanganyiko tu wa kemikali, sukari na maji ambavyo havijengi mwili. Vyakula hivi vinapoliwa kwa muda mrefu bila kula vyakula vingine huufanya mwili kukosa virutubisho, vitamini na madini, hivyo kuufanya mwili kuwa dhaifu na usio na kinga.


Kwa baadhi ya watu, ulaji wa namna hii ni wa kila siku na wa maisha yote tangu mtu azaliwe. Ulaji wa matunda, mboga za majani na ulaji wa vyakula vingine vyenye virutubisho huonekana ni anasa, ingawa vipo katika mazingira wanayoishi. Katika staili ya maisha kama hii, mwili hauwezi kuwa na kinga ya kupambana na maradhi.


Kama wewe ni miongoni mwa watu wenye staili ya ulaji wa vyakula kila siku kama nilivyo elezea hapo juu, usishangae kwa nini unaugua mara kwa mara au kwa nini unakabiliwa maradhi hatari. Yakupasa kuelewa kwamba mwili wako hauna kinga kwa sababu huwa huli vyakula vyenye kuupa mwili kinga inayotakiwa.


Kwa kawaida mwili wa binadamu unapopewa virutubisho vinavyotakiwa, hujitengenezea wenyewe kinga ya kujilinda dhidi ya maradhi mbalimbali na kinga ya mwili hujengwa kwa kula zaidi matunda ya aina mbali mbali na mboga za majani.


Aidha, kinga ya mwili huimarishwa kwa kula vyakula asilia au vyakula vitokanavyo na nafaka zisizokobolewa.
Ili kujenga mwili imara na kujiepusha na maradhi na hali ya kuugua mara kwa mara, ni lazima uchukue hatua ya kubadili


staili ya maisha yako kwa kuangalia upya aina ya vyakula unavyokula kila siku, kuanzia asubuhi hadi jioni. Bila kukubaliana na ukweli huu, kuumwa mara kwa mara na kusumbuliwa na maradhi hatari, huwezi kukuepuka na wala usidhani umerogwa.
Katika makala nyingi zilizopita, nimeelezea kwa kirefu aina mbalimbali za vyakula, faida zake na madhara yake. Lakini katika makala haya tutaelezea kwa kifupi kanuni sahihi za ulaji vyakula na mpangilio wake.

 
Mkuu UKI unaweza kutumia lakini sio ndio kila siku kula chips au kunywa soda haifai hata kidogo ukitaka kula kila siku

fanya hivi chemsha viazi usivikaange kuwa chips tengeneza Juisi yako nyumbani kwa kutumia matunda fresh tumia mashine ya Blenda

kwa kutengeneza Juisi yako kivyako usinywe Coca Cola au Pepsi au Fanta au Mirinda zote hizo ni Feki au usinywe juisi ya Maboksi za

aina zozote zile hizo ni Feki zina madhara juu yako kiafya tumia matunda yaliyokuwa ni Fresh tengeneza wewe mwenyewe juisi

nyumbani kwako huo ndio ushauri wangu.
 
Reactions: UKI
Safi sana Mzizi Mkavu, Mimi kwa sasa nina Miaka Miwili tangia niachane na Soda na mwaka mmoja tangu niache Juice za Makopo na Mabox, Hata Sembe huwa naitumia nikiwa safarini tu tena mara moja moja, Ila nikiwa nyumbani ni Dona kwenda Mbele ingawa watu huwa wananishangaa sana kwa nini nakula Dona, na hata Hotelini mara Nyingi huwa naulizia Dona ingawa ni hoteli chache mno unazo weza kukuta wanapika Dona,

Na hata ishu ya Mikate kwa kweli Mikate myeupe ilisha nishinda siku nyingi sana, na Huwa natumia sana Brown Bread ingawa ni Ghali sana, na ni kikosa bora kula viazi vitamu kuliko kula Mandazi na Chapati,

MKUU TATIZO NI KWAMBA WATANZANIA WENGI WANAAMNI MTU ANAYE KULA MIKATE YA BROWN ANA KISUKARI NA MIMI NISHA ULIZWA MARA NYINGI SANA KAMA NINA KISUKARI AU LA
 
wanaoishi kijijini wanatamani kula kama watu wa mjini(vyakula vya kukaanga na kutumbukiza kwenye mafuta) hawajui kama watu wanaoishi mjini nao wanatamani kula kama wao( michemsho ya vyakula na matunda)......
 
Mkuu Chasha waache washangae kwa sababu hawaujuwi thamani yake huo mkate wa Brown bread mimi ndio chakula changu cha

kila siku asubuhi hivi sasa nimeuagiza huo mkate wa brown kutoka katika duka wananiletea nimewapigia simu na uwe unakunywa sana maji ya Uvuguvugu asubuhi kabla ya kunywa kitu glasi 2 na ukisha maliza kupiga mswaki unywe tena

maji ya uvuguvugu glasi moja asubuhi kabla ya kula kitu na ukae kama dakika 45 ndio waweza kunywa chai ya asubuhi. Na mchana unywe glasi moja kabla ya kula chakula cha mchana kisha kaa kama saa 1 ndio ule chakula na usiku kabla ya kula kitu kunywa maji ya uvuguvugu glasi1 kisha kaa kama saa

1 kisha ule chakula na usiku wakati wakulala unywe glasi moja maji ya uvuguvugu kisha lala utaona afya yako itakavyokuwa ni nzuri hutawezatena kuumwa ovyoovyo na unaweza kukaa mwaka pasipo na kuumwa na kitu .

Tembelea Thread yangu hii hapa bonyeza https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/365977-muujiza-ya-matibabu-kwa-maji-ya-moto-kunywa-2.html
 
Asante mkuu mungu akubariki sana kwa kutufumbua macho kuhusu vyakula hivi!
 
Aisee hii nguna nimekuwa nikiipeleka mdomoni karibu kila siku---Ahsante na ninashukuru kwa somo
 

Mkuu shukurani, nitaanza kufanya hivyo mara moja
 
Ahsante dokta, ngoja nibadili mfumo wangu wa misosi sasa. Sijui nimechelewa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…