Jinsi Wanamuziki wadogo wanavyoangamia ndani ya uadui wa Ali Kiba na Diamond

Diwani

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2014
Posts
2,680
Reaction score
2,779
Habarini wanajamvi.
KUTOKA BONGO FLAVA:
Muziki wetu kwa sasa unakua kwa kiwango cha kimataifa kiasi cha kufanyika kile ambacho hakikuwahi kufikirika kichwani mwa watanzania wenyewe kuhusu BONGO FLAVA, Ingawa kuna juhudi za wasanii wengi katika kuufikisha mziki wetu katika kiwango cha kimataifa lakini katika vinywa vyetu hatuwezi kuacha kutamka ALI KIBA na DIAMOND kama mifano ya kuigwa ndani ya harakati za kukuza muziki wetu.

Wasanii hawa wawili hawana nguvu yoyote kama wangesimama wenyewe bila nguvu ya wananchi waliyoona kazi na kuikubali kwa kuweka usikivu na mchango wa maendeleo ya wasanii binafsi na maisha yao ili waendeleze burudani kwa watu hawa

Hata mbuyu ulianza kama mchicha, tulianza kumsikia ALI KIBA na CINDERELLA, DIAMOND na KAMWAMBIE hizi ni nyimbo zilizowatambulisha kama wasanii wachanga lakini sasa ni wasanii wakubwa.

Tuna ndoto za kukuza muziki wetu kwa kiwango cha juu zaidi lakini tukisema wasanii wakuwatumia ni DIAMOND na ALIKIBA basi ni dhahiri tunaota ndoto za mchana kweupe, hawa watu ni icon za muda huu, na bila shaka wanazidi kupanda lakini kuna wengine wanaofanya vizuri

kibaya zaidi wao hushhindana kutoa nyimbo kwa sababu attention za watu zipo kwao, lakini hakuna ushindani kwa wengine kwa sababu wananchi hawajazipi kipaumbele kazi zao kabisa,
wasanii hao huishia njiani na kisha kupotea kabisa kwa sababu kipaumble chao ni kidogo mno, na hakikidhi haja yao ya kujiweka kimataifa, hii ni hatari ya kupolomoka mzik wetu, nchi za nje wanatazama BONGO FLAVA kupitia hawa watu wawili, ssa endapo wasanii hawa wawili wakipotea nani tutamsimisha tena kwa ajili ya kutangaza kimataifa? lets stop this kuna wasanii wengi wanahitaji kuona nguvu yetu tukiwafikisha pale walipo, mfano RUBY, BARNABA, DITTO, MAUA SAMA, YOUNG KILLER, NANDY, BARAKA THE PRINCE, WCB (exclude DIAMOND), CHIN BEEZ, YOUNG DEE, ROSA REE, IBRA NATION, na wengine

kwa mtazamo wangu, jeshi tajwa hapo juu litatufikisha tunapotaka, ila wawili hawatutoshi, tujifunze kwa NIGERIA kule humtaji Davido na Wizkid peke yake yaani hata roho inakataa ukiiona ile team ya MAVINS RECORDS na akina P-SQUARE na wengineo

Nawasilisha
 
Naomba kujua mpaka leo upelelezi umefikia wapi!
 
Mkuu umesahau Lionel Messi Na Cristiano Ronaldo wamefanya wachezaji wanaojua kuonekana Wa kawaida...

Aguero
Sanchezi
Lewandosk
Coutinho
Dybala
Higuain


Wote hawa ni mfano Wa wachezaji wanaosakata mpira vizuri ila Kimvuli cha Messi na Ronaldo wanaonekana Wa kawaida

Sent From My Nokia Ya Tochi
 
Alikiba naye kawa wa kimataifa kweli.. Ebu achane masihala nyie. Hamkusikia Tecno kwenye fiesta mwaka jana au. Tanzania tuna wasanii wawili tu wa kimataifa. Diamond & V.money.

Ali msanii wa kichina
 
point mkuu,

But swali moja,hivi had Alikiba na Diamond wakafika hapo walipo,walipewa sapoti gan unique na mashabiki ambayo hawa hawapewi?

Nadhani ni juhud zao binafsi na kujitofautisha na wengine,hivyo nasisitiza hawa nao wafanye juhud na wawe tofaut

Umemtaja Ibranation ,sijui kwa nini but huwa namkubali sana huyu dogo ,nadhan ana uwezo mkubwa kuliko ambavyo watu wanamchukulia
 
juhudi katika kazi haiwezi kuonekana endapo ulipozielekezea juhudi zko kuna kiza, hawa ni wanamuziki, tuache for leisure hawa wanafanya muziki ili waonekane na watu, lakini je kama watu hawaoni juhudi zao wanaishia wapi? naombba uangalie nguvu ya umma kwa nyimbo aliyoitoa ali kiba ya seduce me, its okay nikapata kifani kwa msaniii kutoka kenya, NYOTA NDOGO alisema kwammba anawapenda watanzania kwa sababu wanasapoti sana wanamziki wao, kwanini asiwapende wakenya? unakuja kona kumbe wao wamesahaulika na uma, ndio mana muziki kenya lives in coma, Ibranation hat mimi naelewa kazi yake, inapendeza
 
Alikiba naye kawa wa kimataifa kweli.. Ebu achane masihala nyie. Hamkusikia Tecno kwenye fiesta mwaka jana au. Tanzania tuna wasanii wawili tu wa kimataifa. Diamond & V.money.

Ali msanii wa kichina
Ndio ni msanii wa kimataifa, sifa za msanii wa kimataifa zipo nyingi, kwa mfano, msanii kuwekwa katika categories za ushindani wa kimataifa katika tuzo za kimataifa, MTV etc, kuwa signed chini ya kampuni ya kimataifa as well, vanessa ni msanii pia wa kimataifa, lakini je, mziki ndio ulimuweka vanessa kuna icon ya kimataifa toka Tanzania, kwa mimi, hapana, MTV hosting ndio ilimuweka vanessa ktambulika kimataifa mziki ukafuata, kwa Diamond na alikiba ni vitu tofauti yaani wao waliwekwa kimataifa na muziki
 
Kumbe hata kwenye mpira wapo, nashukuru sna kwa kujazia nilipoacha
 
Tukiongea mnasema tunawashwashwa
 
Kiukweli mond na kiba hamna kipya wanacho Fanya ila majina yao na fanbase Kubwa inawabeba ila kuna wasanii wanafanya kazi mf aslay nyimbo zake nzuri hazina mbwembwe za beats maneno ya naskika vzr na melody,akina bright baraka Beka n.k. wanafanya mziki mzuri hadi dmpoz kakumbwa na upepo wa kiba na mondi akati alikuwa ana -ahead top then kaflop.
 
Kwa kutomuweka hazard hapo hujatendea haki hii comment yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…