Jinsi wenye mafanikio wanavyotudanganya

chizcom

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
8,680
Reaction score
18,035
Fanya wewe kama wewe, siyo kusikia kwa kudanganywa na watu wanaosema nilianza na mtaji wa laki, sijui maisha ni polepole, sijui kidogo ndiyo kingi n.k.

Hii ni picha ya babu wa Aliko Dangote, Sanusi Dantata. Alikuwa mmoja wa matajiri zaidi nchini Nigeria, katika miaka ya 70.

Pia, baba wa Dangote alikuwa tajiri barani Afrika mnamo mwaka 1955.

Aliko Dangote alizaliwa katika familia ya bilionea; usiruhusu msemaji yeyote wa motisha akuue. Unajaribu wewe, siyo kudanganyika na hao.

 
Kuna watu utawasikia eti mbona Bill Gates aliacha shule unaanza kumwambia ukweli usiseme shule sema Havard. Chuo cha watu wenye hela na wenye akili na siyo kwamba aliacha shule aliishindwa ila aliacha kwakua aliona anachokitaka yeye kifundishwe hakikuepo, kwahiyo ni shule ilimshindwa yeye siyo yeye aliishindwa shule.

Sasa kijana unapata division zero shule ya kata ukiambiwa rudi darasani utetezi wako ni Bill Gates naye hakusoma, pumbavu.
 
Overrated ume genelize sana, mbona mifano ya walioanza chini wapo kibao Regnarld Mengi kaanza from Zero kabisa Mamayake alikuwa muuza mboga tu, MarkZuck, Elon Musk kaanza Zero kaanza Zero, hapa Tz wakina Bruno Smartcode wameanza Sayansi. Pia usifosi kuangalia ma Billionaire iyo level kubwa sana vijana kibao umewashuhudia kwa macho yako wanatoka form Zero kabisa DIAMOND PLATNUM.. Mifano ipo mingi.

Kunzia chini inawezekana ukapanda mdogomdogo ila njiani utakutana na backup mbalimbali/nyingi zitakazo ku-push kwenda fasta na safari yako ila ukikaa tu bila kuanza izo backup hutozisikia mfano Harmonize ameanzia chini ila kwenye njia amepata Backup kutoka kwa MOND ukiwa na resources zinazokuwezesha kuanza anza mkuu...
 
Eti Mengi alianza kwa kuuza karanga, hii fix

Karanga hizi hizi za mia.mia[emoji2957]
Katika utajiri wa watu wengi,kuna msukumo wa namna flani uliowawezesha kufika hapo walipo,lakini sio mapambano tu ya kawaida,mfano mtu kaiba hela serikalini katajirikia halafu mwisho wa siku anataka kusadikisha watu kuwa alifuata rules flani ndio maana kawa tajiri...
 
Hongera mkuu umenena vyema, angalau huu uzi umeutia sura mana sio kwa mauzauza alioyaandio mtoa mada...

Aache kujilegeza apige kazi kwa akili na aanze kwa icho alichonacho atatoboa tu
 
Njia za kufanikiwa from zero ni hizi. Kamari, kazi/biashara kwa bidii na urithi.

Changamoto ni hapo kwenye kufanya kazi/biashara kwa bidii. Kona kona na ujanja mwingi uko hapo. Kuna mikono mingi Sana hapa ambayo ni ngumu kupata ukweli.

Jiulize, Kama mtu alianza na mtaji wa karanga/chapati, it means kuna watu alikuwa anafanya nao hiyo biashara, Pia kuna waliomu inspire kufanya hiyo biashara na mafanikio yao ndio yaliyomvuta. Sasa Mbona wanafanikiwa wenyewe tu na kuacha wengine wakiwa chini kwenye biashara ile ile?

Si kwamba watakuwa smart Sana! La hasha! Maana wangekuwa smart wasingefanya biashara hizo hizo za kawaida za kuzoeleka na wengi. The point kunakuwa na untold story behind. Na ndio Siri yenyewe ya utajiri au mafanikio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…