Jinsi wenye mafanikio wanavyotudanganya

Huwezi kuwa bilionea kwa kuanza na mtaji au biashara ya kawaida (ndogo) and then eti ndiyo hiyo hiyo ikukuze mpaka uwe bilionea.
Lazima, ukwapue sehemu au ufanye janja fulani ili ukue zaidi.
Ndiyo maana biashara haramu zipo kwa ajili hiyo.
Sasa wewe komaa na laki mbili kama mtaji wako huku ukitegemea kuwa bilionea, haitatokea.
 

[emoji3]
 
................Bro umejaribu kumung'unya maneno kidogo but ukweli hasa kwa hizi nchi zetu za Kiafrika bila wizi na ujanja ujanja mtu hutoki,watu wanakataa tu ila hawajui kuwa kitendo cha kudanganya uhalisia wa mtaji wako na mapato yako kwa afisa wa kodi tayari umeshafanya wizi.

Hata hao wanaopeana tuzo za walipa kodi bora kuna sehemu huwa wanapiga na hawa huwa na watu wao kwenye system ambao kama mtu upo nje ya biashara huwezi kushtuka.
 
Hahahahahaha duuuh unazingua
 
kuna mtu alishawahi kuniambia, katika nchi zetu hizi za kiafrica ukitaka kuwa tajiri haswa, tajiri kwelikweli lazima ashiriki moja ya mambo haya ili kumuwezesha kufika huko.
1. Rushwa,Ufisadi/wizi wa mali za umma/kampuni
2. Kukwepa kodi, Biashara za magendol/Haramu
3. Ushirikina
4. Kurithi mali
Hizi zingine ni porojo tu za mdomoni
 
Konde boy alianzia chini, sa ivi anagawa hela jukwaani.

Pia Makonda kuna picha za zamani alikua choka mbaya sa ivi yuko hapo alipo.
The Masanja na wenzake walikua choka mbaya, sa ivi wana magari ya kubadilisha kuanzia jumapili mpaka jumaosi.

Tatizo hapo katikati huwa hatuambiwi ukweli walifanyaje, labda mfano kujipendekeza kwa wakubwa, kuuza unga, walisoma elimu ya juu zaidi, walienda kanisani na kuombewa etc. huwa hawatamki kabisa, ili na sisi tuwe matajiri.
 
Ndio kona kona na ujanja ujanja! Sio kwa Africa tu. Ni duniani kote kwa ujumla..lazima ucheze na system ili ufike juu. Hakuna bilionare yoyote duniani ambae hajacheza na system.
 
Ninachojua ni kwamba kuna vitu wanatuficha katika kufanikiwa kwao... Atakuambia nilianza na mtaji wa laki lakini hatakuambia kama kuna mtu alimshika mkono na kumoa connection hadi kufika hapo. Kwa wanawake hawezi kukuambia kama huenda alitoa papuchi kwa boss kubwa ndio akapata mtaji wa milioni ila utasikia tu nilijichanga sasa mbona unajiuliza wengine wanajaribu kujichanga wanakwama?
 
Watu wamekazania tu alianza kwa kuuza Katanga, sio kweli; njiani kunakuwa na back ups nyingi tu, mfano: wizi kwenye mashirika au makampuni wanakopita kufanya kazi. Unadhani ni kwa nini vyama vya ushirika vinafilisika?
 
Kumbukumbu zinasema mengi amewah kuwa mfanyakazi wa serikalini tena taasisi za kifedha
 
Siri kubwa ya kufanikiwa ni kugundua talanta yako na itumie ikuletee mafanikio. Wengi mnafeli sababu mnataka kufuata vitu ambavyo by nature hauko talented. Kama ambavyo Dangote hawezi kuwa footballer mkubwa ndivyo sawa na wewe hutoweza kuwa Dangote katika biashara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…