Jinsi ya kuandaa mchuzi wa nyama ya kusaga

Jinsi ya kuandaa mchuzi wa nyama ya kusaga

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Habari ya leo wadau wa jinsi ya kupika.
Karibuni tena jikoni tuandaeandae vitu vizuri, leo ni mchuzi wa kima au mchuzi wa nyama ya kusaga. Ni kitoeleo kizuri cha wali, mkate, chapati na hata maandazi.

Mahitaji

  • Nyama ya kusaga nusu kilo
  • vitunguu robo kilo
  • nyanya 6 kubwa
  • viazi mbatata robo kilo
  • mafuta nusu kikombe
  • thoum kiasi
  • hiliki kidogo
  • mdalasini kiasi
  • bizari nzima kiasi
  • chumvi nusu kijiko
  • tangawizi nusu kijiko

Kuandaa Mchuzi wa Nyama ya Kuasaga Hatua kwa Hatua
  1. Osha nyama uitie kwenye chujio ivuje maji
  2. kata vitunguu, nyanya, menya viazi uvikate vyembamba
  3. menya thoum usage, saga na viungo vyote vilobakia
  4. teleka sufuria tia samli, ikichemka tia vitunguu ukaange mpaka vibadilike rangi viwe vya hudhurungi, kisha tia viazi na nyanya. Baadae tia viungo ulovisaga vyote pamoja na nyama
  5. endelea kukaanga kidogo na kisha utie maji pamoja na chumvi na limao. Acha ichemke mpaka karibu ya kukauka. Hapo itakua tayari.

Namna hiyo tutakua tumeshaandaa mchuzi wetu wa nyama ya kusaga, natumai mmelielewa na kulifurahia. Huu mchuzi waweza utoelea chapati, maandazi, mkate, ila kwa wali unaenda vizuri.
Karibuni sana
 
Maji,maji,maji!
Mkuu.
Nyama yenyewe ina maji. Jumlisha yale ya kuoshea, Nyanya nazo zina maji. Pia ni vema na muhimu kuelekeza namna ya ukataji wa vitunguu na viungo vingine kwa pishi hili.
Nyama ya kusaga na baadhi ya mapishi yanategemea sana mwonekano ili kuleta mvuto kwa mlaji kabla hata ya ladha yenyewe.

Pongezi zangu kwako pia.
 
Back
Top Bottom