BarakaMaiseli
Member
- Feb 15, 2012
- 9
- 5
Watanzania, napenda kufahamu kuhusu hii biashara ya mabango makubwa kwa ajili ya kutangaza biashara za makampuni mbalimbali. Na, nina interest zaidi na mabango ya ki elekroniki, au niseme ambayo yanatumia umeme na yanakuwa yanaonesha tangazo zaidi ya moja kwa awamu awamu. Kwa mfano, inaweza ikawa ni makampuni matatu yote yanatangaza kwenye bango moja, yanakuwa tu yanapewa muda kama dakika 3 hivi kila moja, baadae mzunguko unajirudia. Sasa maswali yangu ni haya hapa chini (tunaweza kurahisisha kwa kuchukua bango la 1m x 1m, au 1 square meter):
(1) Mchanganuo wa faida kwa hii biashara uko vipi? Kwa wastani, makampuni huwa yanalipa gharama kiasi gani kwa mwezi? Nadhani hii pia inaweza ikawa inategemea na mahali bango lilipo, tufanye assumption kwamba bango lipo eneo lenye watu wengi.
(2) Utaratibu wa kuanzisha biashara ya mabango ukoje? (TANROADS, Halmashauri, na TRA)
(3) Changamoto za hii biashara ni zipi? Naweza ku guess moja kuwa ni suala la nishati ya umeme, kwa vile mabango yatakuwa yanaendeshwa kwa nishati hiyo.
(4) Gharama za uendeshaji wa biashara ni zipi?
(5) Ushindani wa biashara ya mabango ya Electroniki uko vipi kwa sasa Tanzania?
(6) Ni maeneo Tanzania ambayo ni potential na yanayoweza kutoa faida nzuri?
(7) Ni makampuni gani yanayoendesha biashara kama hii Tanzania? (kama ntapata websites zao au contacts ntashukuru)
Ushauri mwingine pia, ambao labda haujagusa hayo maswali, nitashukuru kuupokea. Kuna kiambatanisho kinachoonesha mfano wa bango la Electroniki (kwa Dar es Salaam, kule Posta kuna mabango flani yanakuwa yanabadilisha matangazo kila baada ya muda; au pale opposite na mlimani city oilcom kuna moja linalotumia LED)
Ahsanteni sana.