Aliko Musa
JF-Expert Member
- Aug 25, 2018
- 209
- 315
Kuanza kuwekeza kwenye ardhi na majengo imekuwa ni chanagamoto kubwa kwa wengi. Changamoto hii inasababishwa na kukosa maarifa sahihi na kufanyia kazi maarifa sahihi.
Ili uondoe hofu ya kuanza kuwekeza kwenye ardhi na majengo unahitaji kuwa na maarifa sahihi.
Maarifa sahihi yatasaidia kuondoa sehemu ya hofu ya kuogopa kuwekeza kwenye ardhi na majengo.
Hofu itaondoka kabisa kwa kuchukua hatua na kuanza kuwekeza moja kwa moja kwenye ardhi na majengo
Kumbuka; hakuna mbadala ya kufanya kazi kwa bidii. Haiwezekani kupata mafanikio makubwa na ya kudumu bila kufanya kazi kubwa.
Iandae akili yako na mwili wako kufanya kazi kwa bidii kama kweli unahitaji kujenga mafanikio makubwa kupitia uwekezaji kwenye ardhi na majengo.
Kuanza Kuwekeza Kama Kazi Ya Ziada.
Uwekezaji kwenye ardhi na majengo hufaa zaidi kuanza kufanywa kama kazi ya pembeni hasa kwa ambao hawana sifa zifuatazo;-
✓ Hawana uzoefu na maarifa sahihi ya kuwekeza kwenye ardhi na majengo.
✓ Hawana mtaji fedha wa kutosha.
✓ Wafanyabishara na waajiriwa serikalini na taasisi binafsi.
Njia Rahisi Za Kuanza Kuwekeza Kwenye Ardhi Na Majengo.
1. Mikopo Ya Ukarabati Wa Nyumba Za Kupangisha
Kutoa mikopo ya ukarabati na maboresho ya nyumba za kupangisha. Hapa mwekezaji anapata nafasi ya kujifunza kwa undani zaidi kuhusu majengo ya kupangisha.
Hapa anapata nafasi ya kujifunza moja kwa moja kutoka kwa anaowakopesha mikopo kwa ajili ya kukarabati na kuboresha nyumba za kupangisha.
Mwekezaji anakuwa anatoa mikopo kwa ajili ya kununulia samani (furnitures) za kuweka kwenye majengo ya kupangisha.
Njia hii haihitaji kiasi kikubwa cha mtaji fedha. Njia hii inahitaji uwe na mfumo mzuri wa kutathimini uzuri wa soko la nyumba za kupangisha.
Kila mahali kuna nyumba za kupangisha. Hivyo huwezi kukosa wawekezaji wanaohitaji mikopo kwa ajili ya nyumba zao za kupangisha.
Uzuri wa kutoa mikopo kwa njia hii ni kuwa ni vigumu sana kutolipwa marejesho ya mkopo wako kwa sababu chanzo cha marejesho ni cha uhakika.
Huhitaji kutoa mikopo kwa ajili ya ukarabati wa nyumba ambazo zina chanagamoto ya kupata wapangaji bora kwa zaidi ya miezi miwili (2) kwa mwaka.
Pia, sio vyema kutoa mikopo ya ukarabati wa nyumba ambazo sio za kupangisha. Hii inaweza kupelekea kupoteza mtaji fedha wako.
Unapoanza unaweza kutoa mikopo bila kusajiliwa. Njia rahisi na bora kabisa ni kusajili kikundi cha kutoa cha mikopo ya ukarabati kwa wawekezaji kwenye majengo ya kupangisha.
Baada ya kukua kwa kikundi chenu mnasajili kampuni dogo la kutoa mikopo kwa wawekezaji wa nyumba za kupangisha.
Kwenye hatua hii ya kumiliki kampuni ya mikopo, mnaweza kuongeza wawekezaji kwenye aina nyingine ya majengo au viwanja.
2. Kutoa Huduma Za Udalali Wa Ardhi Na Majengo
Hii kazi haitaji kiasi kikubwa cha mtaji fedha. Unahitaji vifaa kama vile simu janja (smartphone) au kompyuta kwa ajili ya kuwafikia wateja wengi zaidi.
Kazi hii inalipa zaidi kwa watu ambao wanaishi kwenye majiji makubwa kama vile Dar Es Salaam. Na jiji la Dodoma udalali unalipa kwa sababu ndio jiji linalovutiwa na wengi.
Kazi hii inaweza kukupa matokeo ya haraka sana endapo utaifanya kwa ubora na uaminifu mkubwa.
Ni vyema kama utaifanya kama kazi ya pembeni hasa kipindi ambacho hauna mtandao mkubwa wa kuwafikia wateja wengi.
Muhimu ni kuwa unahitaji kutengeneza wafuasi wako kupitia moja ya njia zifuatazo;-
✓ Mtandao wa Telegramu.
✓ Blogu.
✓ Ukurasa wa facebook.
✓ Ukurasa wa instagram
Mtandao wa Telegramu au WhatsApp utakupa matokeo mazuri sana ukilinganisha na facebook, instagram na blogu.
Unachotakiwa kufanya ni kuwakusanya wafuatiliaji wa blog kwenda kwenye kundi la Telegram.
Unatakiwa kuwakusanya wafuatiliaji wa ukurasa wa facebook na instagram kwenda kwenye kundi la Telegramu.
Zipo njia nyingi za kuwafikia wateja wengi zaidi, lakini hizi tatu (facebook, instagram na blog) ndio zinawatumiaji wengi zaidi.
Hutakiwi kutumia mitandao mingi ya kijamii. Mitandao ya kijamii mitatu tu inatosha kujenga mtandao mkubwa wa wafuasi wako wa kundi la Telegramu.
3. Kutoa Huduma Ya Kusimamia Nyumba Za Kupangisha
Hii ni kazi ambayo inahitaji kiasi kidogo sana cha mtaji fedha. Hapa unatafuta mwekezaji ambaye anamiliki majengo ya kupangisha na kumfanyia kazi kwenye nyumba zake za kupangisha.
Wapo wengi ambao hawana uzoefu na muda wa kusimamia majengo yao ya kupangisha. Hawa wanaweza kukupa kazi za kusimamia nyumba zao.
Makundi ya wawekezaji ambao wanaweza kukupa kazi ya kusimamia nyumba zao za kupangisha ni kama ifuatavyo;-
✓ Wanaoishi mbali na nyumba zao za kupangisha.
✓ Wafanyabishara mbali na nyumba za kupangisha.
✓ Waajiriwa serikalini na taasisi binafsi.
✓ Wawekezaji wasiokuwa na maarifa sahihi na uzoefu wa kuwekeza katika nyumba za kupangisha.
✓ Wawekezaji wenye uhitaji wa wabia. Njia pekee ya kufahamiana vizuri sana ni kufanya kazi fulani pamoja kwa miaka kadhaa.
Hakikisha unakuwa mwaminifu kwa mmiliki wa nyumba na wapangaji wa nyumba husika. Uaminifu ndio itakuwa tiketi itakayokufikisha kwenye maono yako makubwa.
Pia, hakikisha unaanda mfumo ambao malipo ya kodi yatatoka kwa wapangaji kwenda kwa mwenye nyumba bila kupitia mikononi mwako.
Kwa kipindi hiki cha teknolojia hili ni rahisi sana kufanyika. Pia, hakikisha gharama za ukarabati wa nyumba zinakuwa wazi na kuwe na ripoti maalumu ya kuainisha jumla ya gharama za ukarabati na maboresho.
Hizi ndio njia tatu (3) ambazo zinaweza kufanya ndani ya miaka miwili (2) tu uanze kuwekeza kwenye ardhi na majengo.
Muhimu; njia zote hizi vitakupa matokeo mazuri sana endapo utakuwa na tabia ya kuwafuata wateja walipo.
Rafiki yako,
Aliko Musa.
WhatsApp; +255 752 413 711