Jinsi ya kuanzisha Biashara ndogo ambayo inategemea ujuzi

Jinsi ya kuanzisha Biashara ndogo ambayo inategemea ujuzi

Emmanuel Budigila

New Member
Joined
Feb 2, 2018
Posts
1
Reaction score
4
Ikiwa una ujuzi wa fani fulani mfano( Ufundi Umeme, Ufundi Mekanika, Ufundi Bomba n.k). Andiko hili litakufaa namna ambavyo unaweza kushughulikia hali hiyo na kukuwezesha kupata mteja wa kwanza na hatimaye ikiwa utaendelea kujibidiisha utapata wateja zaidi siku za usoni. Ili tuweze kuelewa andiko hili na kurahisisha kulitumia napenda kutoa mfano wa Fundi Bomba na jinsi anavyoweza kupata mteja wa kwanza.

Swali

Fundi Bomba anawezaje kupata mteja wa kwanza?

Jibu

Ili kupata mteja wa kwanza na kuendelea fundi bomba anaweza kufanya yafuatayo:-

1. Kuandaa “Business cards” za kutosha na kuwapa wanafamilia/ au watu wa karibu na awaombe wawape watu wanaowafahamu ndani ya wiki moja tangu awape na vile vile awaombe wawaeleze marafiki zao vizuri kuhusu yeye na kazi zake

2. Kwenda kwenye maduka yanayouza vifaa vya ujenzi na kuwapa kadi na pia ikiwezekana awaruhusu wenye maduka waandike namba zake kwenye vitabu vyao

3. Ikiwa atapata mteja kwa mara ya kwanza na kufanya naye kazi mara baada ya kumaliza kumfanyia kazi ampigie simu na kumuuliza kuhusu huduma ambayo alimpatia kama aliridhika nayo na kama kuna shida yoyote asisite kumtembelea na kurekebisha hali hiyo. Na mara hiyo anaweza kumuachia mteja yule “Business Cards” ili awape marafiki zake ambao huenda watahitaji huduma za Fundi bomba siku za usoni au kumuomba ikiwa watu watahitaji huduma hiyo awaelekeze kwake kwa kuwapa namba yake.

4. Pia anaweza kufanya kazi na wajenzi wanaojenga majumba(Contractors au waliochukua Kazi ya Kujenga Nyumba, au wajenzi wa nyumba ambazo hazijaisha) huenda wakati fulani watahitaji huduma ya fundi bomba wakiwa katika hatua ya muendelezo wa kujenga. Fundi bomba anapaswa kujitahidi kuwa na mawasiliano na mafundi Umeme na mafundi bomba wengine na awaeleze kuwa ikiwa kuna kazi ya fundi bomba itahitajika yuko tayari kufanya. Pia awaeleze wao pia kuwa yuko tayari kuwapa kazi ikiwa atapata kazi zinazohusiana na Umeme n.k

5. Kufungua akaunti kwenye mitandao ya kijamii na kueleza kazi ambazo anafanya na ikiwezekana aweke picha za kazi ambazo amefanya. Pia kutenga muda wa kupitia akaunti zake ili kujua maombi au maswali yaliyoulizwa na watumiaji wengine wa mtandao wa kijamii.Fundi Bomba anapaswa kufanya akaunti zake ziwe ni kwa ajili ya kazi tu na sio akaunti ambayo zinaruhusu mizaha.

Mawazo haya yanaweza kutumika hata kwenye biashara nyingine / kazi nyingine jambo la msingi ni kuwa makini na kutopoteza lengo. Ukifanya hivi baada ya muda utapata mteja wa kwanza na hatimaye utapata wateja wengi baadaye..

Kazi yoyote ili ufurahie ni pale unapokuwa na wateja hivyo fanya haya na utafanikiwa kupata wateja

Ni matumaini yangu mawazo haya yatakuwa ni yenye manufaa kwako.
 
Back
Top Bottom