Jinsi ya kubadili jina kwenye TIN NUMBER

Abu Haarith

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2015
Posts
314
Reaction score
165
Salaam wakuu
mimi ni kijana niliyekutana na mkanganyiko kidogo kwenye familia yangu

lakini nimegundua ukweli kuhusu nasaba yangu zaidi upande wa majina mwanzo nilikuwa naitwa WALED lakini nimegundua kuwa mimi naitwa IBRAHIMU je nawezaje kubadilisha jina kwenye TIN number yangu maana nahitaji kwenda kuchukua leseni ya gari
 
Nenda TRA na kitambulisho chako cha jina la sasa hivi watakubadilishia
 
Au nenda TRA chukua TIN mpya. Ni buree tu
 

Naamini unapobadili jina ni suala la kisheria zaidi, kwani itaathiri nyaraka zako zote zilizomo kwenye jina la awali.
Hivyo nakushauri upitie kwa mwanasheria/wakili ili ule kiapo kwamba wewe Ibrahimu ndiye ulikuwa ukiitwa Waled hapo awali. Itabidi kiapo hicho ukitunze na kukiwakilisha sehemu yoyote ile ambayo utakutana na mgongano wa jina lako la awali na jina jipya. Kubadili jina kienyeji kunaweza kukukwamisha siku za usoni.
 
shukran kwa ushauri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…