Jinsi ya kubadilisha lugha ya kompyuta iwe Kiswahili

Tukudzi

Member
Joined
Jun 22, 2019
Posts
40
Reaction score
17
Ungependa kubadilisha lugha ya tarakilishi yako kutoka Kimombo hadi Kiswahili? Ungependa kutumia Microsoft Office kwa Kiswahili? Basi fuata maagizo haya.

Kitu cha kwanza unachofaa kujua ni kuwa Windows hutumia faili aina ya LIP (language interface pack) kuwezesha lugha zisizo Kimombo kuonyeshwa kwenye tarakilishi yako. Kwa hivyo, kwa kupakua faili hii inayolingana na lugha unayotaka, unaweza kuonyesha Windows na Microsoft Office kwa lugha yoyote, ikiwemo Kiswahili.

Kubadilisha Windows hadi Kiswahili:
  1. Pakua faili ya LIP ya Kiswahili kutoka seva za Microsoft. Zingatia iwapo tarakilishi yako ni 64-bit au 32-bit.
  2. Fungua faili hiyo na usakinishe lugha yako (Kiswahili) ukifuata maagizo.
  3. Nenda Control Panel -> Region and Language -> Keyboards and Languages. Hapo kwenye "Choose a display language", chagua Kiswahili.
  4. Utalazimishwa kuaga kwanza ili mabadiliko yako yatekelezwe. Fanya hivyo.
  5. Utakapoingia tena, utapata lugha inayotumika imebadilika ikawa Kiswahili.

    Hata hivyo, umbizo ya tarehe, saa na sarafu bado si ya Kiswahili. Kubadilisha hii inahitaji marekebisho ya mwisho, ambayo ni:
  6. Nenda Paneli Dhibiti -> Kanda na Lugha -> Maumbizo. Chagua Kiswahili. Bonyeza Sawa.

    (Iwapo ungependa kubadilisha muonekano wa AM/PM hadi ASUBUHI/USIKU au hata AS/US, nenda Mipangilio ya ziada... -> Saa -> Maumbizo ya saa).
Kwa hayo machache, tarakilishi yako sasa iko katika lugha ya Kiswahili.
 
Kubadilisha Microsoft Office hadi Kiswahili


  1. Jijuze ni version ipi ya Office uliyo nayo. Iwapo version ni Office 2010 au ya baadae, unaweza kupata faili yake. Iwapo version ni Office 2007 au awali, pole.
  2. Pakua faili ya LIP inayolingana na version yako. Kumbuka kuzingatia iwapo una Office ya 64-bit au 32-bit.
    Office 2010
    Office 2013
    Office 2016
    Office 365
  3. Sakinisha lugha uliyoipakua.


  4. Fungua programu yoyote ya Office (Word, Excel, PowerPoint, Publisher, Access ama hata OneNote).
  5. Nenda File -> Options -> Language -> Choose Display and Help Languages. Chagua Kiswahili kwa Display Language na pia kwa Help Language. Bonyeza Set as Default. Bonyeza OK.
    Utalazimishwa kuwasha upya programu zote za Office zilizo wazi. Fanya hivyo.

    Kwa hayo machache, sasa unaweza kutumia Office kwa Kiswahili.

    Iwapo unataka kuandika katika Kiswahili bila kuonyeshwa mistari miekundu eti maneno uliyoyaandika hayatambuliki, inabidi usanidishe Office yako hivi:
  6. Nenda Faili -> Chaguo -> Lugha -> Chagua Lugha za Kuhariri. Chagua Kiswahili. Bonyeza Weka kama Chaguo-Msingi.
 
Duh hapana aisee, hiyo lugha kwenye upande wa teknolojia lazima kichwa kikuume.
 
Duh hapana aisee, hiyo lugha kwenye upande wa teknolojia lazima kichwa kikuume.
Cha kusikitisha kiswahili (Kenya). Kenya wametuzidi aise yaani lugha inayotumia Tanzania inatambulika kama ya Kenya. Tanzania ni nini kinachojivunia?
Kilimanjaro inatambulika kama ipo Kenya
Wamasai-Kenya
Aisee. Ndiyo tatizo la kuweka siasa katika kila kona na matokeo yake unaanza kukimbizana na wapinzani na kuwapiga risasi watu. Tanzania hakuna kitu aisee
 
Hii lugha kwenye kisimu changu cha tochi imenishinda... Sa kompyuta si ntachanganyikiwa
 
Naona kiswahili kinakuwa kigumu kuliko hata kikorinto.......
Eti maumbizo duh[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Li lugha letu lina swagga lakini sasa kuna misamiati ya kidwanzi mfano umbiza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…