Jinsi ya kubaki kuwa masikini

D Metakelfin

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2017
Posts
3,399
Reaction score
3,666
1. Kamwe usiamke mapema wala usiwaze maendeleo waza ngono muda wa kuamka kama huna usingizi ingia FB au insta, endelea kulala na kujinyosha mpaka pale njaa itakapokuuma.

2. Kamwe usipange jinsi ya kutumia pesa zako, wewe zitumie tu pale unapozipata. Na zikiisha kaa chini na jifikirie umezitumiaje.

3. Kamwe usifikiri juu ya ku 'save' pesa zako, subiri mpaka uwe nazo nyingi ndio uanze ku 'save', utasave vipi pesa zako wakati unazo kidogo? Wanaokuambia usevu pesa hawakutakii mema katika matumizi yako.

4. Kamwe usijiingize katika biashara ambazo huwa mnaziita 'za wasiosoma' wewe ni mhitimu wa chuo kikuu ulie soma bhana utafanyaje biashara ya viazi? Utauzaje duka? Utauzaje viatu vya mitumba? Hizo ni biashara za wasioenda shule. Wewe unapaswa ukae ofisini upigwe na kiyoyozi.

5. Kamwe usifikiri kuanzisha biashara mpaka pale Malaika atakaposhuka toka mbinguni kukuletea mtaji wa kuanzia biashara. Watakuambiaje uwekeze wakati hujapata hata Milioni? Hata kama wafanyabiashara wengi kama kina bakheresa walianza kuuza mgahawa, wewe ni smart, unatakiwa uanze na mamilioni katika biashara zako.

6. Lalamika kuhusu kila kitu, isipokuwa usilalamike kuhusu uvivu wako na attitude yako. Ilaumu serikali ya Magufuli, zilaumu benki zilizogoma kukukopesha fedha, zilaumu kampuni mbalimbali ambazo zimekutosa kwenye ajira. Wote hao wana roho mbaya hawataki kukufanya uwe tajiri!

7. Tumia pesa nyingi tofauti na unachokipata. Kufanikisha hili nunua bidhaa za kutumia kwa mkopo, azima pesa kwa washkaji nunua kitanda cha Milioni moja, nunua Brand new LG flat screen, pendezesha kwako. Kopa pesa benki nunua Verossa, watoto wa mjini wakukome.

8. Shindana katika kuvaa. Hakikisha unavaa kila aina ya fashion mpya ya nguo. Nunua kila aina ya simu mpya inayotoka, kama ulinunua sumsung galaxy S6 kwa milioni moja, uza hata laki sita halaf ongezea hela ukanunue sumsung galaxy S7. Zimetengenezwa kwa ajili yetu bhana.

8. Ukishindwa kununua gari mpya, nunua gari ya mtumba ambayo gharama zake za kulihudumia ni mara mbili ya mshahara unaoupata, au gari linalokaa muda mrefu gereji kuliko barabarani.

9. Wape wanao kila wanachokitaka kwa kuwa wewe ni mzazi bora, hawatakiwi kuhangaika wala kufundishwa utu na thamani ya pesa, usiwafundishe juu ya kutunza na kuheshimu fedha. Usiwafuatilie kabisa katika masomo yao.

Waache wakue wakiwa wavivu na waje kuwa masikini kuhakikisha kuwa hawawezi kukusaidia pale utakapozeeka.

10. Tembelea viwanja vyote vya bata na ulale hukohuko pesa honga tu mademu na uzuri wamiliki wa maeneo ya starehe wanatujali yaani wanafungua maeneo mapya kila siku, tembelea yote. Kula bata kula bata

Na ukishakuhakikisha kwamba unatekeleza hayo yote, kaa chini na utafakari kuwa siku zote fainali nzuri huchezwa uzeeni!

[emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji113][emoji113][emoji113][emoji113][emoji113][emoji113][emoji113]
 
Mkuu binafsi nimekukubali,maana hapa hujamsema
mtu yeyote.Ungeweka mbinu za kuwa tajiri
wangekubeza kuwa wewe ni tajiri?
Lakini fasihi uliyotumia imekaa poa sana
mimi nimeona pa kujisahihisha nakushukuru sana
na ubarikiwe.
 
Mkuu binafsi nimekukubali,maana hapa hujamsema
mtu yeyote.Ungeweka mbinu za kuwa tajiri
wangekubeza kuwa wewe ni tajiri?
Lakini fasihi uliyotumia imekaa poa sana
mimi nimeona pa kujisahihisha nakushukuru sana
na ubarikiwe.
Ahsante.nawajua watanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…