Jinsi ya kubaki kuwa masikini

Gluk

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2017
Posts
1,859
Reaction score
3,008
1. Kamwe usiamke mapema, endelea kulala na kujinyosha mpaka pale njaa itakapokuuma.

2. Kamwe usipange jinsi ya kutumia pesa zako, wewe zitumie tu pale unapozipata. Na zikiisha kaa chini na jifikirie umezitumiaje.

3. Kamwe usifikiri juu ya ku 'save' pesa zako, subiri mpaka uwe nazo nyingi ndio uanze ku 'save', utasave vipi pesa zako wakati unazo kidogo? Wanaokuambia usevu pesa hawakutakii mema katika matumizi yako.

4. Kamwe usijiingize katika biashara ambazo huwa mnaziita 'za wasiosoma' wewe ni mhitimu wa chuo kikuu ulie soma bhana utafanyaje biashara ya viazi? Utauzaje duka? Utauzaje viatu vya mitumba? Hizo ni biashara za wasioenda shule. Wewe unapaswa ukae ofisini upigwe na kiyoyozi.

5. Kamwe usifikiri kuanzisha biashara mpaka pale Malaika atakaposhuka toka mbinguni kukuletea mtaji wa kuanzia biashara. Watakuambiaje uwekeze wakati hujapata hata Milioni? Hata kama wafanyabiashara wengi kama kina bakheresa walianza kuuza mgahawa, wewe ni smart, unatakiwa uanze na mamilioni katika biashara zako.

6. Lalamika kuhusu kila kitu, isipokuwa usilalamike kuhusu uvivu wako na attitude yako. Ilaumu serikali ya Magufuli, zilaumu benki zilizogoma kukukopesha fedha, zilaumu kampuni mbalimbali ambazo zimekutosa kwenye ajira. Wote hao wana roho mbaya hawataki kukufanya uwe tajiri!

7. Tumia pesa nyingi tofauti na unachokipata. Kufanikisha hili nunua bidhaa za kutumia kwa mkopo, azima pesa kwa washkaji nunua kitanda cha Milioni moja, nunua Brand new LG flat screen, pendezesha kwako. Kopa pesa benki nunua Verossa, watoto wa mjini wakukome.

8. Shindana katika kuvaa. Hakikisha unavaa kila aina ya fashion mpya ya nguo. Nunua kila aina ya simu mpya inayotoka, kama ulinunua sumsung galaxy S6 kwa milioni moja, uza hata laki sita halaf ongezea hela ukanunue sumsung galaxy S7. Zimetengenezwa kwa ajili yetu bhana.

8. Ukishindwa kununua gari mpya, nunua gari ya mtumba ambayo gharama zake za kulihudumia ni mara mbili ya mshahara unaoupata, au gari linalokaa.


By Gluk
 
Unaelewa maana ya masikini ??


Unadhani wasiofanya hayo yote Ni matajiri ?
 
Unaelewa maana ya masikini ??


Unadhani wasiofanya hayo yote Ni matajiri ?
Hapa nazungumzia umasikini wa kipato,
Na ukiwa na afya njema hupaswi kulalamikia umaskini bali jilaumu mwenyewe kwa kushindwa kutumia akili yako vizuri.
 
Unaelewa maana ya masikini ??


Unadhani wasiofanya hayo yote Ni matajiri ?
Pia si wote ni matajiri ila wanaonyesha nia ya wanachokihitaji katika maisha yao hata kama hawajatimiza ndoto zao.
 
Hapa nazungumzia umasikini wa kipato,
Na ukiwa na afya njema hupaswi kulalamikia umaskini bali jilaumu mwenyewe kwa kushindwa kutumia akili yako vizuri.
Kwahiyo masikini wote hawatumii akili zao vyema ???



Nasubiri ujibu hili swali ili nikuheshimu au nikudharau kiujumla.
 
Kwahiyo masikini wote hawatumii akili zao vyema ???



Nasubiri ujibu hili swali ili nikuheshimu au nikudharau kiujumla.
Kuwa maskini wa kipato ili hali una afya njema kabsa ni tatizo la kutoitumia akili yako apasavyo...Kwenye nchi yenye fursa kama TZ.
 
WANAKUJA KUKUPA MWONGOZO MKUU!!!
 
Matajiri wangekuwa wengi sana
Hivi unahisi utajiri unaanzia kiasi gani?
Ukiwa unauwezo wa kumudu mahitaji yote muhimu wewe si maskini.
Masikini ninayemzungumzia mimi ni yule asiyeweza kumudu mahitaji yake ya msingi ili hali ana nguvu na akili timamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…