It depends. Hakuna lililo bora.
Mi ni bachelor. Self employed. Nafanya kazi from home na inapobidi naenda site kwa client. Ila muda mwingi niko nyumbani.
Kwangu hakuna jiko hata la kuchemshia maji. Hizi ni sababu zangu, na zinaweza zisifanane na zako.
1. Nina kazi nyingi za kufanya. Kuandaa, kupika, post clean up itanichukua si chini ya masaa 6 kwa siku. Time better spent working.
2. Kuweka jiko, store ya vyakula na viungo kutaharibu the overall aesthetic ya my place. Kumbuka ni home office - air conditioned, electronics kibao. Upepo wa mzungu hauendani na harufu ya vitunguu
3. Vyakula ninavyopendelea kula sio optimal kupikia nyumbani. Nyamachoma, uta grill kila siku?
4. Sina hobby ya kupika. Sina hii talanta, siko creative jikoni. Najua kupika just the basics for survival.
5. Kula nje kunanipa variety. Naweza kula hata vitu nisivyoweza kupika. Najiuliza tu leo nile nini kisha natafuta sehemu kinapouzwa.
6. Nina usafiri binafsi unaoniwezesha kwenda kula popote haraka sana. Siko locked to a single provider. Always nabadilisha sehemu ninapokula ili kubadilisha ladha na kutafuta the best.
Kwa upande wa gharama nadhani what you want to eat matters more kuliko whether you cook or buy. Mimi ni foodie. My expenses za msosi zinarange katiya 200k - 350k a month.