SoC02 Jinsi ya kuboresha uhusiano wako na watu wanaokuzunguka kwenye jamii yako

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Jul 13, 2021
Posts
19
Reaction score
35
Mtaji mkubwa wa mtu ni watu kwa maana hiyo unahitaji kuwa na ujuzi wa kuishi vizuri na watu “Interpersonal skill” pasipo kujali upo wapi na unafanya nini; lakini kupitia makala hii utaenda kuwa mtu mwenye kuishi vizuri na watu na kufanya watu kuvutiwa na uwepo wako kwenye jamii yako, na amini upo tayari kujua si ndiyo eeh!

Mambo ya kufanya ili uwe mtu mwenye kuishi vizuri na watu;

i. Shiriki matukio ya kijamii, “Maisha ni yako lakini mazishi ni yetu” msemo wa kiswahili, inapokuja kwenye matukio ya kijamii elimu yako, cheo chako, taaluma yako, mafanikio yako weka pembeni kwa sababu ukibeba hivyo utajikuta unashindwa kushiriki baadhi ya mambo ya kijamii kwa kuona si hadhi yako na hapa ndiyo tatizo linapoanza, kwenye matukio ya msiba na sherehe shiriki ipasavyo hii itaboresha sana mahusiano na watu wengine “Watende wengine kama ambavyo ungependa na wewe utendewe” ni Kanuni ya dhahabu au ‘Golden rule’.

iii. Jifunze kuwasikiliza wengine, changamoto kubwa ya watu ni ujuaji mtu anaongea na wewe unaongea kunakuwa hamna maelewano ndiyo maana watu wenye ufanisi ili kuelewa watu wengine wanajifunza kusikiliza kwa usikivu na kuacha kila kitu wanachofanya kwa lengo kujua nini mtu anaongea na hata majibu ambayo utatoa yatakuwa yana uwiano na kile mtu ameongea, usipokuwa unasikiliza wengine ni dhahiri una kiburi na jamii itakuzama kama mtu mbinafsi “Jifunze kuelewa kabla ya kutaka kueleweka” alisema Steven Covey kwenye kitabu cha 7 habits of highly effective people. Kusikiliza inamafanya mtu akupende na kuongea hata mambo ambayo hakupanga kabisa kuongea ndiyo maana methali maarufu ya zamani inasema “Una masikio mawili na mdomo mmoja ikiwa na maana sikiliza mara mbili kisha ongea mara moja” ukiwa msikilizaji utajifunza mengi kuhusu watu na kuwa mtatuzi wa changamoto za wengine pia utafanya watu wengine wasijione wapweke inawezekana hitaji kubwa ni kusikilizwa kwa kumpa muda wa kumsikiliza tu.

iv. Samehe walikukosea, watu dhaifu ndiyo wanaishi kwa visasi, chuki, hasira na uchungu hii inapelekea kuwa na msongo wa mawazo na kusababisha kupata magonjwa ya vidonda vya tumbo, shambulio la moyo, shinikizo la damu , je unajua chuki inamtesa mwenye kuchukia na siyo yule ambaye anachukiwa? Jifunze kusamehe kwa ustawi wa afya ya akili yako na mwili wako pia itafanya watu wakupende sababu mtu mwenye chuki siku zote hukimbiwa maana ni hatari sana “Watu wenye hekima wanasamehe na watu dhaifu wanaweka kisasi” alisema Socrates baba wa falsafa duniani. Pia Dale Carnegie alisema “Ruhusu watu kukoseah” kwa sababu hakuna ambaye ni mkamilifu jifunze kuwasemehe wengine kisha akiendelea kusema “Kabla hujalala usiku samehe kila kitu na kila mtu fanya hivyo maisha yako yote, ulinde afya yako, amani yako na furaha yako”. Kusamehe siyo udhaifu.

v. Kutowasema watu wengine vibaya, usimhukumu mtu kwa maneno ya kuambiwa kuwa mtu fulani kufanya hiki au kile, jifunze kupuuzia baadhi ya mambo kwenye maisha yako pia epuka kuwasema watu wengine vibaya kwa sababu watu wakikubaini kuwa ni tabia yako utajenga taswira mbaya kwenye jamii yako “Si wanawake wala wanaume ni wambeya sana sikuhizi” msemo wa pwani, acha kusema wengine vibaya, je hujui ambaye unamsema anaweza kubadilika ndani ya siku moja? Pengine baraka zako zipo kwa mtu ambaye unamsema vibaya.

vi. Kusaidia watu wengine, kutoa ni moyo kuna baraka na furaha kubwa kwa kusaida watu wengine pasipo kutarajia malipo kuwa ipo siku moja utasaidiwa au kupewa shukurani, kwenye jamii yako wasaidie watu wenye uhitaji inaweza kuwa marafiki zako, watoto, majirani, walemavu n.k hii itafanya uwe mfano wa kuigwa kwenye jamii yako, lakini usitoe kwa ajili ya kujionyesha bali toa kwa sababu umeguswa. “Mtu bora zaidi ni yule ambaye furaha yake ipo kwa kutoa na kuwasaidia wengine na siyo kupokea au kusaidiwa na wengine” alisema Aristotle mwanafalsafa zamani wa kigiriki akiwa na maana unakuwa na furaha kubwa kwa kuleta furaha kwa wahitaji na ukumbuke msemo huu “Charity begin at home” ukiwa na maana moyo wa kuwasaidia wengine unaanzia nyumbani; kuna baraka unapata kwa Mungu na watu wengine kwa kuwatoa kwenye giza na kuwaleta kwenye nuru wala kuwasaidia wengine siyo mpaka uwe na fedha nyingi la hasha! Hapana unasaidia wengine kwa ushauri, kidogo ulichobarikiwa, kuwasikiliza, kuwaona n.k kuwa balozi wa kuwasaidia wengine kama ambavyo marehemu Reginald Mengi alivyokuwa anafanya.

vii. Kuwa na kauli nzuri, hakikisha mdomo wako unatoa maneno ya baraka na siyo ya laana” hakuna mtu ambaye anaweza kupendwa kwenye jamii kama ana Kauli mbaya kwa kutukana watu, kutoa matamko ya kumshusha mtu thamani, kuvua utu wa mtu n.k hii itafanya ushindwe kuishi vizuri na watu “Maneno hayavunji mkupa, lakini hayaumiza sana moyo” msemo wa kiswahili, mahali popote ambapo upo toa kauli nzuri kwa watu na kwako mwenyewe kwa sababu maneno uumba na hii ni nguvu ambayo Mungu katupa kwa maana hiyo ongea kauli zenye kuleta faraja, matumaini, upendo, amani, furaha kwa watu wengine itafanya watu wapende kuwa karibu na wewe; chunguza mtu ambaye anapendwa na kukubalika kwenye jamii yako na anasifika kwa kuishi vizuri na watu? Utagundua ukweli kuwa anatoa kauli nzuri pamoja na sababu zengine za juu hapo.

vii. Omba msamaha/radhi uliowakosea, usiishi kwa kusema nitaomba msamaha kesho badala yake sema naomba msamaha leo kwa yule ambaye nimemkosea kwa lengo la kudumisha upendo na kuondoa tofauti, kuomba msamaha wala siyo udhaifu bali ni kiwango kikubwa kuwa unajitambua na kujua kuwa wewe siyo mkamilifu kwa maana hiyo unaomba msamaha ili kuonyesha unakiri makosa yako; je hujawahi kusikia mtu fulani hana mahusiano mazuri ya watu wengine kwa kushindwa kuomba msamaha kwa makosa aliyofanya? Kwa sababu anaona kuomba msamaha ni udhaifu kumbe siyo kweli. Nenda leo kuwaombe msamaha wote ambao umewewakosea na utabaini nguvu ya msamaha ni kubwa kufanya mahusiano kuwa bora, Kama Mungu anatusamehe makosa yetu ya kila siku kwanini wewe unashindwa kuomba msamaha kwa uliowakosea?

Unahitaji kuthubutu kuboresha mahusiano yako na watu kwa sababu mtaji wa kwanza ni watu kabla ya fedha na vitu vingine, “Usiwachukulie poa watu na badili mtazamo wako kisha thamini watu” alisema Emmanuel Olumide mwandishi wa vitabu kutoka Nigeria.

HATUA YA KUCHUKUA; Orodhesha mambo 10 ambayo unadhani ukifanya utakuwa na mahusiano mazuri na watu?
 
Upvote 2
Ama kweli kuwa na utu na busara ni kitu cha muhimu sana, tuzidi kuishi na watu vizuri.
 
Kaka Inno
Nimekupigia Kura Naomba na Mimi unipigie Kura kupitia SoC 2022 - Tufuge nyuki kwa maendeleo endelevu na tuwalinde kwa wivu mkubwa
 
Back
Top Bottom