Jinsi ya kudhibiti wasiwasi

Jinsi ya kudhibiti wasiwasi

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Weekend nilikuwa nimekaa na washikaji zangu wanne sehemu tunakunywa pombe wote ni watumishi wizara mbalimbali na sio wenyeji wa huu Mkoa. Sasa pembeni ya ile bar alikuwepo amekaa jamaa fulani ambaye kwa maelezo ya washikaji zangu ni Kuwa jamaa ni usalama wa taifa japo mimi sina uhakika sana maana simjui.

Basi tukawa tunapiga stori za mambo ya kiutumishi ikiwemo shutuma mbalimbali maofisini ila mwisho nilichogundua wafanyakazi wengi tunaogopa Sana wanausalama wa taifa tukiamini kwamba wanaweza kusababisha ukafukuzwa kazi.kwa mfano labda kashfa za ulevi hata Kama unakunywa baada ya kazi kwamba usalama wa taifa wanakuwaga na ma file ya wafanyakazi na tabia zake mitaani katika jamii.

Mimi mwanzo nilikuwa sijui Kama mambo ya nje ya ofisini yanaweza kukuharibia maana naonaga walimu kibao huko vijijini NI walevi hata wakija darasani ila usalama wa Huku mijini hawaangalii kazi yako unafanyaje Bali wanaangalia mambo mengine unatumiaje pesa yako.Sasa mimi ile kujishtukia nimesema siitaki mtu Kama NI usalama wa taifa akaamua kunichomea kazini mwache anichomee Kama ni kwa ubaya Basi utamrudia tu.Chuki hazina faida na majungu sio mtaji.

Ninachotaka kusema NI kuwa wasiwasi kupita kiasi kunaweza kuathiri mwili na hisia zako. Hata kunaweza kukusababishia matatizo makubwa zaidi ya tatizo ambalo awali lilifanya uwe na wasiwasi.hakuna haja ya kuwaza Sana kitu ambacho hakijatokea tatizo halipo mtu linaanza kukupa msongo wa mawazo.

Kingine ni punguza kiasi cha habari mbaya unazopata. Si lazima upate taarifa kuhusu kila tatizo linaloendelea ulimwenguni. Ukifuatilia kupita kiasi taarifa mbaya kunaongezea hofu na kutuvunja mioyo.tujitahidi kufikiria mambo mawili au matatu yanayofanya tuwe wenye shukrani.na mwisho kabisa NI kufanya mambo kwa kufuata ratiba maalumu Kama unalala saa nne Basi jitahidi muda ule ule kila siku.
 
Kwaiyo jinsi ya kudhibiti wasi wasi ni kujikuta una ropoka au
 
Hayachunguzwi maisha ya mtu binafsi kama hakuna kitisho, alafu kingine jua kuwa wana majukumu mbalimbali na si wote wakusanya taarifa. Ndiomana wamegawanywa kuanzia, wiraya, mkoa kikanda na taifa wakiwa na majukumu mbalimbali kwa mfano idara ya ulinzi kwa viongozi waandamizi wa serikali.
 
Usalama wa taifa ana deal na mambo ya msingi sana. Kuna vitu vingine tunawasingizia kwamba wanajihusisha navyo we kunywa zako pombe tu.
 
Kwanza kila ofisi wanakuwa wamo kwa kazi maalum pia unatakiwa maisha yako yawe private unapofanya mambo kwa kujichoresha inakufanya hata usifikiriwe kbs kweny uteuzi wa apo ofisin kwenu coz tyr wanakua wanajua life style yako kuna watu wanakosa teuzi coz wanajulikan ni wazinzi ama walevi N.K kujichoresha kwao kunawaharibia mengi san
 
Kwanza kila ofisi wanakuwa wamo kwa kazi maalum pia unatakiwa maisha yako yawe private unapofanya mambo kwa kujichoresha inakufanya hata usifikiriwe kbs kweny uteuzi wa apo ofisin kwenu coz tyr wanakua wanajua life style yako kuna watu wanakosa teuzi coz wanajulikan ni wazinzi ama walevi N.K kujichoresha kwao kunawaharibia mengi san
Mkuu dunia ya Sasa mambo mengi inakuwa ngumu kuyafanya kwa Siri.. otherwise uwe unanunua pombe halafu unakunywa chumbani kwako kitu ambacho NI kigumu mtu unahitaji uka socialize na watu wengine bar huko ukachome na nyama kidogo Sasa hio ndo kitu naambiwa mtumishi hatakiwi kuwa mlevi..me naona haiwezekani kunywa chumbani.
 
Wasi wasi au kujishtukia ni ugonjwa mbaya sana...
Halafu Cha ajabu kinachofurahisha watu wengi Sana Wana wasiwasi..unaweza kumuhofia boss wako kumbe na yeye anahofu kwa wa juu yake..usikute hata makamu wa raisi anamuogopa Rais anakuwa na wasiwasi kwamba Kuna mambo yake yanamfikia Rais [emoji3][emoji3]
 
Mkuu dunia ya Sasa mambo mengi inakuwa ngumu kuyafanya kwa Siri.. otherwise uwe unanunua pombe halafu unakunywa chumbani kwako kitu ambacho NI kigumu mtu unahitaji uka socialize na watu wengine bar huko ukachome na nyama kidogo Sasa hio ndo kitu naambiwa mtumishi hatakiwi kuwa mlevi..me naona haiwezekani kunywa chumbani.
Kama umesharidhika na nafas uliyonayo sio mbaya kuanika life style yako ila kama ni mtu ambae hujaridhika na nafas uliyonayo inahitajika uishi maisha ya private ili ufikiriwe na hao watu wa kitengo hawamo umo maofisi kwa ajili ya kuchunga tabia za watu wamo kwa ajili ya kuchunguz nan anafaa kwenye uteuzi
 
Back
Top Bottom