Jinsi ya kuepuka prostate cancer

SHADRACK LUTOBECK

Senior Member
Joined
Sep 29, 2013
Posts
129
Reaction score
18
Habarizenu wadau wote wa JF.

Najua muu wazima wa afya njema na kwa ambao afyazenu haziko sawa nawapeni pole!Kuna magonjwa mengi yamekuwa yakisumbuasana kwa sasa katika duniahii tuliyonayo,Matatzo ya kibofu cha mkojo yamekuwa yakiwasumbua sana watu,kuna baadhi ya sababu zinazochangia kuwepo kwa matatizo hayo kama vile UTI,KASWENDE,KISONONO,GONOLEA N.K.

Ukijigundua una magonjwa haya ni vyema zaidi ukaenda hospital.

Maana magonjwa haya yamekuwa ndo chanzo hasa cha ugonjwa huo.

Matatizo ya kibofu cha mkojo yamegawanyika katika sehemu kuu mbili(1)prostate anlargement(mkojo kutoka kidogo tu na kwa maumivu makali hii hufikia hadi kuziba kwa njia ya mkojo).

Prostate encontinence(mkojo hutoka mara kwa mara halii hufanya mkojo kutoka kwa mfululizo).kuna tiba za awali za matatzo hayo.baadhi ya dawa zinazotumika kutibu matatzo hayo ni CLOXASILIN,DOXASILLIN,AMPICILLIN,CO-TRIMAX,LASIX N.K.kama tatzo linaanza unaweza ukatumia dawa hizi ukawa safi kabisa.

Lakini ukikawia kutibu mapema inaweza kusababisha prostate cancer.
 
Asante sana kwa ushauri huu

Hivi tatizo la kupotea kwa korodani moja kwa kuingia ndani na kutoonekana kabisa wakati wa kufanya ngono nayo ni moja dalili ya hii cancer??
 
Ungeshauri watu bora wakiona kuna Dalili fulani waende hospitali sio kutowa dawa pasipo na mtu kujuwa dalili ya maradhi yake ungeliweka Dalili ya Maradhi ya Prostate Cancer halafu ndio unaweza kuweka Dawa lakini wewe unazungumza pasipo na kuweka Dalili ya hayo Maradhi uliyoyataja Mkuu vipi tena?

Maradhi ya zinaa



Maradhi ya zinaa ni namna ya kutaja
magonjwayanayosambazwa kwa njia ya vitendo vya kijinsia, mengine ya zamani (kisonono, kaswenden.k.), na mengine mapya (ukimwin.k.).

Maradhi
hayo yanaweza yakaambukizwa kwa njia nyingine pia, au kwa vitendo vya kijinsia vilivyo halali kwa wahusika, lakini yanaitwa "ya zinaa" kwa sababu yanaenezwa hasa kwa wingi wa

vitendo hivyo vinavyofanyika nje ya
ndoa kwa kujamiiana na watu mbalimbali.
Katika matokeo hayo pia tunaona kwamba
uzinifu unamdhuru binadamu: hatuwezi kuchezea utakatifu wa uhai tusipatehasara katika roho, katika jamii na pengine hata katika mwili.



Uambukizaji wa magonjwa ya zinaa

Magonjwa ya zinaa huambukizwa na wakala wa magonjwa – bakteria wadogowadogo, virusi, parasites, fungi na protozoa wakaao katika sehemu vuguvugu na zenye unyevunyevu katika mwili

kama vile
sehemu za siri, mdomoni na kooni. Magonjwa mengi ya zinaa husambaa wakati wa kujamiiana(katika uke au mkunduni), lakini aina nyingine za kukutana kimapenzi kama kwa kutumia midomo (oral sex) zinaweza kusambaza magonjwa.

Magonjwa mengine ya zinaa yanaweza kusambazwa kwa njia nyingine zaidi ya
kujamiiana. Magonjwa fulani ya zinaa yanayosababishwa na virusi kamaUKIMWI yanaweza kuambukizwa kwa

kukutana na damu iliyoathirika. Kwa mfano, magonjwa yanayosababishwa na virusi yanaweza kusafiri miongoni mwa watu wanaochangia sindano zilizo na maambukizi, na mtu anaweza kupata

maambukizi kwa kupokea dawa iliyoambukizwa. Baadhi ya magonjwa ya zinaa huambukiza kwa kutoka kwa mama hadi kwa mtoto. Maambukizi yanaweza kutokea kabla ya kuzaliwa, wakati vijidudu vikifanikiwa kupita katika
kondo la uzazi(placenta, ogani katika mji wa mimba wa

mwanamke mjamzito ambayo huunganisha mfumo wa damu ya mama na wa mtoto) na kuingia katika mkondo wa damu wa mtoto. Maambukizi pia huweza kutokea wakati wa kujifungua, wakati

mtoto anapopita katika njia ya uzazi au baada kujifungua, wakati mtoto anapotumia
maziwa yaliambukizwa.

Magonjwa ya zinaa hayawezi kuambukizwa kwa kupeana mikono au kugusana, au kugusa nguo au katika viti vya chooni.


Magonjwa ya zinaa yanayofahamika.

Kuna magonjwa ya zinaa mengi, haya ni baadhi yale yanayofahamika sana

Klamidia

Klamidia ni ugonjwa wa kuambukiza ambao husababishwa na bakteriazinazoitwa na sayansi kama Chlamydia trachomatis.

Ugonjwa huu huwa hauonyeshi daliliza wazi kwa karibia asilimia 75 ya wanawake na asilimia 50 ya wanaume, hivyo maambukizi mengi hushindwa kufahamika mapema.

Kulingana na wakala wa
afya wa Marekani(Centers for Disease Control and Prevention) ndiyo ya kwanza kati ya maradhi ya zinaa yanayoripotiwa zaidi nchini humo: wataalamu wamekisisa kuwa karibia watu milioni tatu huambukizwa klamidia kila mwaka, lakini kulingana na CDC, ni maambukizi 660,000 tu ndiyo ambayo huripotiwa.

Watu ambao hawafahamu kuwa wameambukizwa klamidia wanaweza wasitafute
tiba na hivyo wakaendelea kufanya ngono, bila ya kujua kuwa wanaeneza ugonjwa.

Wakati dalili zinapoanza kujitokeza wanaume husikia maumivu wakati wa kukojoa au kutokwa usaha katika uume. Wanawake wanaweza kutokwa
damu nje ya kipindi chao, maumivu wakati wa

kukojoa, kutokwa
usaha katika uke, au maumivu chini ya kitovu.

Kama utaachwa bila kutibiwa katika wanawake, klamidia unaweza kuleta madhara makubwa kwa afya. Klamidia huaribu tishu za uzazi za mwanamke na kusababisha uvimbe katika
fupanyonga(pelvic inflammatory disease, PID). PID inaweza kusababisha mauvimu makali sana katika

fupanyonga, utasa/ugumba au utata katika
ujauzito ambao unaweza kusababisha kifo.

Watoto waliozaliwa na mama waliombukizwa klamidia huwa na hatari ya kupata upofu au maambukizi katika
mapafu.

Uchunguzi wa maambukizi ya klamidia hufanyika kwa kuchunguza
fupanyonga na kiwango kidogo cha majimaji kutoka katika uke au uume ambayo huchunguzwa kwa uwepo wa Chlamydia trachomatis.

Uchunguzi mpya kama ule wa mkojo ili kufahamu uwepo wa bakteria wa klamidia umekuwa ukitumika pia ili kufanya uchunguzi rahisi zaidi mwa watu ambao hawaonyeshi dalili za ugonjwa.

Klamidia inatibika kwa antibaotiki.


Kisonono

Kisonono ni maradhi ya zinaa ambayo husababishwa na bakteria zinazofahamika kisayansi kama Neisseria gonorrhoeae. Bakteria hizo hushambulia utandotelezi unaozunguka sehemu za siri.

Ingawa kwa makisio maambukizi 360,000 ya kisonono huripotiwa kila mwaka nchini Marekani, wataalamu wamekisia kuwa watu karibia 650,000 huambukizwa kwa mwaka.


Kama ilivyo klamidia, kisonono nayo huwa haionyeshi dalili. Kisonono ikiwepo huwa na dalili kama zile za klamidia ambazo huhusisha mauvimu wakati wa kukojoa na kutokwa kwa maji yanayonuka au usaha katika uke auuume.


Kisonono huonekana kwa urahisi kwa wanaume ambao hutoa usaha kutoka katika mfereji wa mkojo (urethra). Huanza kidogo, lakini huongezeka na huwa mwingi na kusababisha kusikia haja ya kukojoa mara kwa mara huku kukiwa na maumivu.


Kisonono ikisambaa na kufikia
prostate, mfereji wa mkojo huziba kwa kiasi fulani. Kwa wanawake maambuki hutokea katika urethra, uke au mlango wa uzazi (cervix). Ingawa mwasho unaotokana na majimaji katika uke unaweza kuwa mkubwa, mara nyingi dalili hizi huwa ni chache au hamna kabisa katika hatua za awali.

Kisonono isiyotibiwa inaweza kusababisha PID kwa wanawake. Watoto wanaozaliwa na mama wenye kisonono huwa na hatari ya kuambukizwa wakati wa kuzaliwa; maambukizo haya yanaweza kusababisha magonjwa ya
meno kwa wachanga.

Uchunguzi wa ugonjwa hufanywa kwa kuchungunza usaha kutoka katika uke au uume au mkojo kwa uwepo wa Neisseria gonorrhoeae.


Kisonono iliongezeka kwa kiasi kikubwa Marekani mnamo miaka ya 1970 na mwanzoni mwa miaka ya 1980, hadi kukaribia kufikia kiwango cha magonjwa ya mlipuko (epidemic proportions) kwa vijana wanaobalehe na watu waumri wa kati.

Kisonono hutibiwa kwa antibaotiki kadhaa, ingawa maambukizi yamekuwa na ukinzani juu ya tiba ya baadhi ya madawa katika miongo ya nyuma.
Moja kati ya mambo magumu katika kupambana na kisonono ni kutafuta mahusiano yote ya kimapenzi ya nyuma ya aliyeambukizwa ili kuweza kuzuia usambaaji zaidi wa ugonjwa.



Kaswende

Kaswende ni gonjwa tishio linalosababishwa na bakteria inayofahamika kama Treponema pallidum.
Katika hatua za mwanzo, vipele katika sehemu za uzazi huanza kujitokeza muda mfupi baada ya maambukizi ambavyo baadaye hupotea vyenyewe.
Kama ugonjwa hautatibiwa, maambukizi huendelea kwa miaka, yakishambulia mifupa, ubongo na moyo na kusababisha madhara mengine yanayotokana na matatizo katika mfumo wa fahamu kama vile homa ya uti wa mgongo na magonjwa ya moyo na kiharusi.
Kaswende wakati wa ujauzito unaweza kuwa hatari kubwa kwa kiumbe tumboni, kama vile kusababisha kutoumbika vizuri (deformity) na kifo.
Wanawake wengi wajawazito katika nchi zilizoendelea huchunguzwa kwa uwepo wa ugonjwa huu katika majuma ya kwanza ya mimba ili kutibu ugonjwa kabla kitoto hakijaathirika.
Siku hizi kaswende inaweza kutibika kwa urahisi kwa penicillin.


Malengelenge sehemu za siri


Ugonjwa wa malengelenge katika sehemu za siri husababishwa na maambukizi ya herpes simplex virus(HSV). Aina nyingi za malengelenge huwa ni kutokana na aina ya pili ya HSV (HSV type 2). hatahivyo, maambukizi kutokana na aina ya kwanza ya HSV (HSV type 1) nayo yapo. Malengelenge katika sehemu za siri husababisha vivimbe vinavyouma vinavyojirudia kila mara, ingawa mara nyingi ugonjwa huwa hauonyeshi dalili kwa muda mrefu. Nchini Marekani, mtu mmoja kati ya watano wenye umri wa zaidi ya miaka 12 ameathirika na HSV, na idadi kubwa ya hao waliambukizwa - karibia asilimia 90 - hawafahamu kuwa wana ugonjwa. Upimaji wa damu huweza kuonyesha uwepo wa maambukizi ya HSV, hata kama mtu bado hajaanza kuonyesha dalili. Dalili za HSV zinaweza kutibika kwa kutumia madawa ya yanayopambana na virusi kama vile acyclovir, lakini HSV hawawezi kutoka katika mwili - hawatibiki.

UKIMWI


UKIMWI, Ukosefu wa Kinga Mwilini, ni matokea ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi (VVU) - Human immunodeficiency virus (HIV). UKIMWI ni ugonjwa wa zinaa hatari na usitibika ambao hushambulia mfumo wa kinga ya mwili na kumwacha mgonjwa akiwa hana hata uwezo wa kujikinga dhidi ya maambukizi madogo. Maambukizi ya VVU haimaanishi kuwa mtu anaUKIMWI. Baadhi ya watu na maambukizi ya VVU na wasionyeshe hali ya kuumwa ile inayotambulika kama UKIMWI kwa miaka kumi au zaidi. Watabibu hutumia neno UKIMWI pale mtu anapokuwa katika hatua za mwisho, zinazotishia uhai za maambukizi ya VVU.
UKIMWI uligunduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1981 miongoni mwa wanaume waliokuwa wanaingiliana (mashoga) na miongoni mwa watu waliokuwa wanajidunga sindano katika jiji la New York na California. Baadaye maambukizi mengine yaligundulika pia kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika. Kwa haraka UKIMWI ukawa ugonjwa wa mlipuko duniani kote ukiathiri karibia kila nchi. Mpaka mwaka 2002, ilikadiriwa kuwa watu wazima wapato milioni 38.6 na watoto milioni 3.2 duania kote wanaishi na VVU au UKIMWI. Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO, limekadiria kuwa kutoka mwaka 1981 mpaka mwisho wa mwaka 2002 watu karibia milioni 20 walikuwa wamekufa kutokana na UKIMWI. Kiasi cha hao milioni 4.5 walikuwa ni watoto wenye umri wa chini ya miaka 15.
Wakati VVU wanaweza kuenezwa kwa njia nyingine, kujamiiana ndiyo njia hasa ya maambukizi ya virusi hivi. Wanawake ambao wameathirika na virusi vya UKIMWI wanaweza kumwambukiza mtoto wakati wa ujauzito, kujifungua, au mara kadhaa wakati wa kuwanyonyesha. Njia mbadala ya kupunguza makali ya VVU ni pamoja na kutumia madawa yanayozuia kuzaliana kwa VVU (protease inhibitors), ambayo husaidia kwa kiasi kikubwa kurefu maisha.
Pamoja na kuenea kwa elimu juu ya ugonjwa huu, CDC wamekadiria kuna maambukizi mapya 40,000 kila mwaka Marekani na kuwa kwa ujumla kati ya Waamerika 800,000 hadi 900,000 wameambukizwa VVU.


Dutu za Sehemu za Siri


Dutu huota katika uume na katika eneo la kuzunguka uke na mkunduni. Husababishwa na kundi la virusi lifahamikalo kama human papillomavirus (HPV) ambao husambazwa wakati wa kujamiiana. CDC wamekadiria kuwa kuna maambukizi mapya ya dutu milioni 5.5 nchini Marekani kila mwaka. Dutu za sehemu za siri zinaweza kutibiwa na kuondolewa kwa upasuaji mdogo. Aina fulani ya HPV ambao husababisha maambukizi katika sehemu za siri wanaweza pia kusababisha kansa ya mlango wa uzazi (cervical cancer).

Trichomonasi


Trichomonasi husababishwa na maambukizi ya protozoa anayefahamika kisayansi kama Trichomonas vaginalis. Ugonjwa huu husababisha muwasho na karaha katika uke kwa wanawake na katika mfereji wa mkojo kwa wanaume. Trichomonasi huweza kutibiwa kwa urahisi na antibaotiki. CDC wamekadiria kuwa Waamerika milioni tano huambukizwa trichomonasi kila mwaka.


Kuzuia na kudhibiti maambukizi


Tofauti na magonjwa mengine hatari, hatua rahisi zinaweza kutumika kuzuia maambukizi ya magonjwa ya zinaa.
Hatua ambaYo ni madhubuti kuliko zote ni kuepuka ngono kabisa. Bila ya kukutana kimwili hakuna uwezekano wa kupata maambukizi ya zinaa.

Kuwa na mwenzi mmoja tu katika ndoa na kwa wale wanaojiingiza katika mahusiano pia husaidia kupunguza hatari ya maambukizi.


Kondomu
inakinga dhidi ya maambukizi hayo lakini si kinga kamili kwa asilimia mia moja. Kondomu huvaliwa kwenye uume au kwenye uke na huwa kama kizuizi kwa vijidudu vinavyosababisha

magonjwa ya zinaa. Hata hivyokondomu huwa haifuniki sehemu yote ya siri ambayo hukutana wakati wa kufanya ngono, na uwezekano wa kupata maambukizi ya zinaa bado upo, hasa malengelenge na dutu.


Uchunguzi wa awali na matibabu kamili huzuia madhara zaidi ya maambukizi ya zinaa; wakati huohuo huzuia uambukizaji kati ya mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Hii ni muhimu sana kwa

magonjwa ya zinaa ambayo huwa hayaonyeshi dalili, kwa sababu wale walioambukizwa huwa
hawajui kuwa wana hatari ya kuwaambukiza wenzi wao.


Matibabu yote lazima yafuatwe hata kama matumizi ya awali ya dawa yalipelekea dalili zote kutoweka. Maambukizi yanaweza kuendelea bila ya kuwa na dalili na hivyo kupelekea aliyeambukizwa bila kujua kusambaza ugonjwa.


Mwenendo katika maambukizi ya zinaa

Wakati wowote katika historia, kushamiri na kuongezeka kwa magonjwa ya zinaa huakisi mabadiliko katika sayansi na jamii. Kwa mfano, katika nchi nyingi duniani, kuenea kwa magonjwa

ya zinaa kuliongezeka wakati na baada ya vita vikuu vya pili (1939-1945), wakati wanajeshi walipokuwa kwa kipindi kirefu mbali na nyumbani kwao na kujihusisha katika ngono na watu tofauti

ambao wengi wao walikuwa wana maambukizo ya zinaa. Wakatiantibaotiki - penicillin, ilipopatikana miaka baadaye, nchi hizohizo zilishuhudia upunguaji wa maambukizi.


Hata hivyo kuanzia miaka ya 1950, huko Marekani kisonono kilianza kuenea kutokana na kuongezeka kwa tamaa za ngono. Vijidudu vya ugonjwa viliunda ukinzani dhidi ya penicillin, na

mpaka miaka ya 1970 na 1980 ugonjwa ulifikia hatua ya kuwa ugonjwa wa mlipuko kwa vijana na watu wa umri wa kati.


Kuingia kwa VVU katika jamii ya binadamu kumepelekea janga la kimataifa la UKIMWI ambalo lilianza katika miaka ya 1980 na kuendelea hadi leo hii.


Majanga ya magonjwa ya zinaa yanaendelea, hata pamoja na utumiaji wa kondomu ambao umeongezeka tangu kuanza kwa UKIMWI. Maafisa wa afya wanaamini kuna mambo mengi

yanayowezekana kuwa yanachangia kuongezeka kwa maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Miongoni mwao ni mienendo ya tabia hatarishi. Katika miongo kadhaa iliyopita, umri ambao watu

hufanya ngono kwa mara ya kwanza umepungua, wakati wastani wa wenzi wa kimapenzi ambao mtu hufanya nao ngono katika kipindi cha maisha yake umeongezeka. Kwa pamoja mienendo hii huongeza hatari ya kupata magonjwa ya zinaa

SARATANI (CANCER) YA KIBOFU CHA MKOJO: PROSTATE PROBLEM (CANCER)

Ni vigumu kidogo kuelewa kiswahili cha tatizo
(jina la ugonjwa huu kwa lugha ya Kiswahili) hili ambalo hujulikana kwa lugha ya kitaalamu kama Pprostatitis. Hivyo basi, kwa haraka haraka tunaliita kama tatizo la kibofu cha mkojo.

Prostate ni kokwa ndogo ambayo ipo chini ya kibofu cha mkojo. Kokwa hii hutoa maji maji ambayo kazi yake ni kusafirisha mbegu za kiume. Kokwa hii ikipata uambukizo wa aina yeyote ambao ukachelewesha tiba husababisha mtu kupata saratani ya kibofu cha mkojo
(prostate cancer).

Vile vile tatizo hili likicheleweshwa tiba, hupelekea mtu au mgonjwa kufanyiwa operation ya kibofu cha mkojo na kuondoa kokwa hiyo ambayo ni muhimu sana katika mfumo wa uzazi kwa wanaume. Kokwa hii ikishaondolewa, si rahisi tena kwa mwanaume kufanikiwa kupata mtoto.


Zamani tatizo hili lilikuwa likiwapata watu wazima kuanzia umri wa miaka 60, ila kwa miaka ya sasa huwapata hata vijana ambao hawajafikisha miaka 20 ya kuzaliwa.


Kokwa hii ikipata uambukizo inaweza vimba na kusababisha kugandamiza kibofu cha mkojo, hali ambayo hupelekea mtu kujisikia kama vile amebanwa na haja ndogo, na akienda msalani huwa anatoa mkojo kwa kiasi kidogo sana.


Kinachosababisha tatizo hili, pamoja na dalili ambazo zinaonekana kwa mtu ambaye ana ugonjwa huu tutazielezea kweye makala itakayofuata….usikose kufuatilia makala hiyo. Vilevile nitaelezea nini cha kufanya ili mtu asipate au nini cha kufanya kwa mtu ambaye tayari ana tatizo hili.

Ufahamu Afya Asilia, Ufahamu wa Maisha Mazuri inawapenda, inawajali



HAYA MKUU TUTAJIE NA DAWA ZA HAYA MARADHI PIA.
 
Hapana kaka.mara nyingi cancer za tezi husababishwa na bacteria.bactera hawa hushambulia tezi na kusababisha vijidonda vidogovidogosana kwa asiejua huwa ni vigumu sana kufam.vidonda vivyo husababisha usaa ktk tezi na kuzifanya zishindwe kufanya kazi yake vizuri.pia kwa asiefahamu tezi huwa zina tabia kuu mbili (1)kutanuka zinapopata maambukizi(2)kusinyaa kutokana na maabukizi ya bacteria.Unapogundua tatzo ni vyema zaid kumwona daktar kwa tatzo kama hilo dawa zipo na zinatibu.kwa meng zaid 0759217720
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…