Jinsi ya kufanikiwa kwenye biashara ya daladala

Tabutupu

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2010
Posts
13,206
Reaction score
18,549
1. Uwe na kifua kikubwa cha kukabili mambo magumu, uwe mvumilivu , issue kama kodi, madereva, adhabu, matengenezo

2. Uwe na fundi mmoja unaye mwamini

3. Kosa moja lisimfukuze dereva, wekeza kwenye mafunzo ( mfundishe taratibu yale unayo tamani ayafanye, wengi ni darasa la 7)

4. Fedha ya daladala isitumike kwa mambo mengine.

5. Jifunze kuwaelewa madereva, tabia zao, uwongo wao, etc

6. Usitume spare za kuunga unga, kama gear box inasumbua tafuta gear box mpya au used from Japan.

7. Hakikisha ratiba ya service inazingatiwa kwa oil na filter zenye ubora.

8. Lipa kodi zote

9. Lipa adhabu za barabarani haraka.

10. Usiwasumbua madereva bila sababu.
 
Ukinununua mpya boda ufunge camera kama ya mkoani ..
Japo kwenye daladala sijaona
 
Umeandika kilaini laini sana.

Hapo kwenye kulipa faini za barabarani na kutowafukuza bali kuwadekeza madereva ndipo penye siri ya mafanikio, na umetuingiza chaka.

Ninasema hivi, hakikisha unawaweka sawa traffic ili wasikulipishe faini za barabarani; na madereva hakuna kucheka nao!
 
1. Uwe na kifua kikubwa cha kukabili mambo magumu, uwe mvumilivu , issue kama kodi, madereva, adhabu, matengenezo

2. Uwe na fundi mmoja unaye mwamini

3. Kosa moja lisimfukuze dereva, wekeza kwenye mafunzo ( mfundishe taratibu yale unayo tamani ayafanye, wengi ni darasa la 7)

4. Fedha ya daladala isitumike kwa mambo mengine.

5. Jifunze kuwaelewa madereva, tabia zao, uwongo wao, etc

6. Usitume spare za kuunga unga, kama gear box inasumbua tafuta gear box mpya au used from Japan.

7. Hakikisha ratiba ya service inazingatiwa kwa oil na filter zenye ubora.

8. Lipa kodi zote

9. Lipa adhabu za barabarani haraka.

10. Usiwasumbua madereva bila sababu.
Biashara yangu ya zamani hiyo
 
Umeandika kilaini laini sana.

Hapo kwenye kulipa faini za barabarani na kutowafukuza bali kuwadekeza madereva ndipo penye siri ya mafanikio, na umetuingiza chaka.

Ninasema hivi, hakikisha unawaweka sawa traffic ili wasikulipishe faini za barabarani; na madereva hakuna kucheka nao!
Nilimaananisha
1. Kulipa faini kwa maana usilimbize faini
 
Umeandika kilaini laini sana.

Hapo kwenye kulipa faini za barabarani na kutowafukuza bali kuwadekeza madereva ndipo penye siri ya mafanikio, na umetuingiza chaka.

Ninasema hivi, hakikisha unawaweka sawa traffic ili wasikulipishe faini za barabarani; na madereva hakuna kucheka nao!
Kufukuza dereva ni nzuri ila utakua unaanza upya kila siku.. madereva wanafanana
 
Katika yooote ulioandika hapo mm naona point ni namba 5 tu. Kwa Kila bznes
Asante.

KAZI ni kipimo cha utu
 
Back
Top Bottom