Jinsi ya kufanya makadirio ya gharama za ujenzi wa nyumba

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
JINSI YA KUFANYA MAKADIRIO YA GHARAMA ZA UJENZI WA NYUMBA

Habari wana Ujenzi! Watu wengi wanapata changamoto ya kufahamu makadirio ya material wanayo hitaji katika ujenzi wa nyumba ama majengo mbalimbali. Kwasababu hiyo nimeamua kuanza mfululizo wa kutoa elimu hiyo na leo tutaanza na mahesabu ya idadi ya tofali zinazo hitajika kujenga

Ramani.jpg

Kabla haujaanza kufanya mahesabu lazima uwe na vitu vifuatavyo:

1. Uwe na ramani yenye vipimo ili kujua ukubwa wa jengo lako. Ramani inachorwa na wasanifu majengo wataalamu ambao wanasomea — wataalamu hawa wanahitimu katika vyuo vinne tu hapa nchi navyo ni Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, Chuo Kikuu cha Ardhi), na vyuo vya kati Ardhi Institute — Tabora, Ardhi Insitute — Morogoro, Institute of Lands Dar es Salaam.

2. Ufahamu aina ya material ama tofali utakazo tumia, kama ni hydraform, tofali za kuchoma ama blocks, hii ni kwasababu tofali zina tofautiana size ama ukubwa hivyo hata idadi yake itakuwa tofauti. Tofali zipo za aina tatu, ukubwa wake ni (length x width x thickness/urefu x upana x unene)

HYDRAFORM; 90 mm x 240 mm x 40 mm

BLOCK; 450 mm x 230 mm x 130 mm

KUCHOMA; 450 mm x 230 mm x 150 mm

Hapa tuta tumia mfano wa nyumba hii yenye vyumba viwili-kimoja kikiwa na choo/bafu ndani, sebule, jiko, choo cha wageni na vibaraza viwili; kufanya mahesabu ya tofali zetu.

Hapa kuna hatua mbili za kufuata

1. Tafuta eneo la kuta zote

2. Jumla ya eneo lote la kuta gawanya kwa ukubwa wa tofali

KUTAFUTA ENEO LA KUTA

Hapa tuta tumia kanuni ifuatayo

Eneo = Urefu( wa kuta) x kimo (urefu wa ukuta kwenda juu)

Sasa kujua urefu wa kuta zote, utatakiwa kujumlisha urefu wa kuta zote

Kwenye mchoro wetu pale juu nime weka namba kila kuta hivyo itakuwa kama ifuatavyo {vipimo vipo katika milimita (mm)}.

1 m = 100 cm = 1,000 mm; 1 cm = 10 mm

Ukuta 1= 6,500 mm; ukuta 2 = 9,150 mm; ukuta 3 = 4,000 mm; ukuta 4 = 4,000 mm; ukuta 5 = 9,450 mm

Ukuta 6=11,046 mm, ukuta 7=6196 mm +3200 mm, ukuta 8=9,101 mm, ukuta 9 =3,060 mm, ukuta 10 = 2,900 mm

Sasa uki jumlisha kuta hizo zote unapata jumla ya = 68,603 mm

Eneo la kuta = urefu wa kuta x kimo cha kuta

Hapa kama utajenga nyumba ya kozi 13 maana yake ni kimo cha 3000 mm

Hivyo eneo litakuwa = 68,603 x 3000= 205,809,000 mm

Sasa kumbuka tuna sehemu za wazi ambazo hizi hazihitaji tofali, mfano milango, madirisha na sehemu za wazi za vibaraza

Kanuni ni ile ile urefu x kimo:

Tuna madirisha 6 yenye urefu 2,000 mm & kimo 1,800 mm= 2000 x 1800 sawa na 3,600,000 mm

sasa, tuna madirisha sita yenye vipimo sawa hivyo 3,600,000 x 6 = 21,600,000

Tumia dirisha 1 lenye urefu 1,400 na kimo 1,500 = 1,400 x 1500 sawa na 2,100,000 mm

Tuna dirisha 1 lenye urefu 1,000 na kimo 1,800 = 1,000x1, 800 sawa na 1,800,000 mm

Tuna madirisha 2 yenye urefu wa 800 na kimo 600 = 800x600 sawa na 480,000 mm

480,000 zidisha kwa 2 sawa na 960,000 mm

Tuna milango 9 yenye urefu wa 900 na kimo 2,400 = 900 x 2,400 sawa na 2,160,000 mm

2,160,000 zidisha kwa 9 sawa na 19,440,000 mm

Uwazi wa vibaraza jumla uref 10,010 kimo 2,400 =10,010 x 2,400 sawa na 24,024,000 mm

Jumla ya wazi = 21,600,000 + 2,100,000 + 1,800,000 + 960,000 +19,440,000 + 24,024,000 = 69,924,000 mm

Eneo kamili linalo hitaji tofali za kuta lita kuwa

ENEO LA KUTA — ENEO LA WAZI0 = 205,809,000–69,924,000= 135,885,000 mm

hivyo basi, IDADI YA TOFALI, itakuwa kama ifuatavyo:

Sasa urefu wa msingi wako utategemea na nature ya eneo lakini tuchukulie utakuwa na urefu wa 900 mm, ambapo ni sehemu tambarare (isiyo korofi)

Kumbuka jumla ya urefu wa kuta zote ni 68,603 mm

Kwahiyo 68,603x900 = 61,742,700 mm

Kwahiyo kupata tofali tutalazimika kuchukua jumla ya ukubwa wa kuta ukiwa umetoa uwazi na jumla ya eneo la kuta za msingi kisha tuta gawanya kwa eneo la tofali moja

135,885,000+61,742,700= 197,627,700 mm

Kumbuka tofali ya block lina urefu wa 450 mm na kimo cha 230 mm

Hivyo eneo la tofali ni 450 x 230=103,500 mm

Idadi ya tofali itapatikana kwa 197,627,700mm/103,500mm = 1,909 matofali

Hapa utahitaji kuongeza asilimia kidogo ya tofali kwaajili ya zile zitakazo vunjika na ngazi pia, tutatumia 5%, kwahiyo jumla ni tafali 1909+ 0.05(1909) = 2,004.45 ≈ 2,000 tofali

MAHESABU YA IDADI YA MIFUKO YA CEMENT NA MCHANGA INAYO HITAJIKA KUJENGEA NYUMBA YAKO

hapa tunaingia sehemu nyingine ambayo itahusu ukadiliaji wa idadi ya mifuko ya cement itakayo hitajika kujengea jengo lako.

NB: kumbuka haya huwa ni makadilio, hivyo sio lazima yawe sawa kwa asilimia 100, lakini mara nyingi yanakaribia ukweli halisi kwa asilimia kubwa sana

Tukichukulia mfano wa TOFALI 2,000

Hapa nazungumzia tofali ambazo wengi wanaziita za block, ambazo kitaalamu zinaitwa SAND CEMENT BLOCKS

Hapa tuseme idadi ya tofali za Msingi (inch 6) ni tofali 700

Idadi ya tofali za kuta (inch 5) ni tofali 1300

A: IDADI YA MIFUKO YA CEMENT KWAAJILI YA MSINGI (TOFALI ZA INCH 6)

-Ikumbukwe hapa tofali hizi hujengwa kwa kulazwa

-hivyo tofali hizi zitahitaji cement na mchanga Zaidi kuliko zile za kusimama (inch 5)

KANUNI

Mfuko 1 wa cement unajenga tofali 45 za msingi (inch 6- za kulaza)

Hivyo ukichukulia zile tofali 700 za msingi kwenye ule mfano wetu itakuwa ifuatavyo

Tofali 700 gawanya kwa 45 = 15.5 sawa na mifuko 16 ya cement

NB: (ikumbukwe watu wengine hufanya mfuko 1 wa cement unajenga tofali 50 ama 60 za msingi za kulaza). Hii hufanywa ili kupunguza gharama japo kama ni kwenye kiwanja korofi inaweza kuleta shida.

B: IDADI YA MIFUKO YA CEMENT KWAAJILI YA KUTA (TOFALI ZA INCH 5)

-Tofali hizi mara nyingi hujengwa kwa kusimama hivyo hazili mchanga na cement nyingi kama zile za msingi

KANUNI

Hapa mfuko 1 wa cement unajenga tofali 60 za kuta (inch 5- za kusimama)

Hivyo ukichukulia tofali 1,300 za kuta kwenye ule mfano wetu, itakuwa kama ifuatavyo

Tofali 1,300 gawanya kwa 60 = 21.6 sawa na mifuko 22 ya cement

NB: (ikumbukwe watu wengine hufanya mfuko 1 wa cement unajenga tofali 70 mpaka 90 za kuta, za kusimama), pia hii ni ili kupunguza gharama.

NB: KIPIMO CHA MCHANGA

Mfuko 1 wa CEMENT una changanywa na NDOO 9 kubwa za MCHANGA

Ama mfuko 1 wa CEMENT unachanganywa na NDOO 18 ndogo za MCHANGA

KWA WENYE MPANGO WA KUJENGA VITUO VYA MAFUTA MSISAHAU KUSOMA KITABU HIKI.

Screenshot_20241022_082416_WPS Office.jpg

Screenshot_20241022_082406_WPS Office.jpg

Hiki kitabu unaweza kudownload hapa: Mwongozo wa Ujenzi na Uendeshaji wa Vituo vya Mafuta kwa Gharama Nafuu

NYUMBA YAKO INAVUJA KIPINDI CHA MVUA?
Mtafute huyu fundi huto ona nyumba yako ikivuja tena katika kipindi cha mvua: Fundi wa Kuziba Bati linalovuja kwa Silicone
 
BLOCK; 450 mm x 230 mm x 130 mm

KUCHOMA; 450 mm x 230 mm x 150 mm
Mimi sijawahi kuona tofari ya kuchoma inayoizidi cement block kwa ukubwa labda sijakuelewa hapo naomba ufafanuzi, au huenda somo hili limelenga specific region ambako wanachoma matofari ya namna hiyo
 
Hapo tofari ya kuchoma katupiga kamba
 
Mimi sijawahi kuona tofari ya kuchoma inayoizidi cement block kwa ukubwa labda sijakuelewa hapo naomba ufafanuzi, au huenda somo hili limelenga specific region ambako wanachoma matofari ya namna hiyo
Hata mm hapo sjaelewa kwenye block na tofali ya kuchoma
 
Mimi sijawahi kuona tofari ya kuchoma inayoizidi cement block kwa ukubwa labda sijakuelewa hapo naomba ufafanuzi, au huenda somo hili limelenga specific region ambako wanachoma matofari ya namna hiyo
Kama hilo tofari unalo tayari unachukua rula unapima urefu, upana na kimo chake ili kupata uhakika zaidi. Maelezo mengi hutolewa kama mfano.
 
Watanzania hua ni wachoyo na wanafki sana, Ukitoa elimu ya kitu kizuri wanatafuta makosa tu ilimradi wakosoe na wengi wao wanataaluma hiyo au mafundi wanajisikia vibaya watu wengine kujua,
Nani asiye jua kama tofali la kuchoma na block lina vipimo tofauti,
Kaka umetoa elimu kubwa sana na kosa waliloona ni kipimo cha tofali la kuchoma tu.

Acheni unafiki

Ni mimi Accapulco bay
 
Uzi mzuri sana ninge shauri unge BOLD sijui niviite vichwa vya paragraph, nikiuangalia naona kama umeungana, kuna space nzuri ila naona kama ni habari ndeefu.

Mi huwa na taka kujua, kuna uwezekano kutandaza mabomba chini kabla ya kumwaga zege kwenye msingi ili kuepusha kutindua wakiwa wamemaliza? Yani plumbing na wiring ikinza nyumba inapigwa anainakuwa na nyufa.
 
JINSI YA KUFANYA MAKADIRIO YA GHARAMA ZA UJENZI WA NYUMBA

Habari wana Ujenzi! Watu wengi wanapata changamoto ya kufahamu makadirio ya material wanayo hitaji katika ujenzi wa nyumba ama majengo mbalimbali. Kwasababu hiyo nimeamua kuanza mfululizo wa kutoa elimu hiyo na leo tutaanza na mahesabu ya idadi ya tofali zinazo hitajika kujenga

View attachment 3146143

Kabla haujaanza kufanya mahesabu lazima uwe na vitu vifuatavyo:

1. Uwe na ramani yenye vipimo ili kujua ukubwa wa jengo lako. Ramani inachorwa na wasanifu majengo wataalamu ambao wanasomea — wataalamu hawa wanahitimu katika vyuo vinne tu hapa nchi navyo ni Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, Chuo Kikuu cha Ardhi), na vyuo vya kati Ardhi Institute — Tabora, Ardhi Insitute — Morogoro, Institute of Lands Dar es Salaam.

2. Ufahamu aina ya material ama tofali utakazo tumia, kama ni hydraform, tofali za kuchoma ama blocks, hii ni kwasababu tofali zina tofautiana size ama ukubwa hivyo hata idadi yake itakuwa tofauti. Tofali zipo za aina tatu, ukubwa wake ni (length x width x thickness/urefu x upana x unene)

HYDRAFORM; 90 mm x 240 mm x 40 mm

BLOCK; 450 mm x 230 mm x 130 mm

KUCHOMA; 450 mm x 230 mm x 150 mm

Hapa tuta tumia mfano wa nyumba hii yenye vyumba viwili-kimoja kikiwa na choo/bafu ndani, sebule, jiko, choo cha wageni na vibaraza viwili; kufanya mahesabu ya tofali zetu.

Hapa kuna hatua mbili za kufuata

1. Tafuta eneo la kuta zote

2. Jumla ya eneo lote la kuta gawanya kwa ukubwa wa tofali

KUTAFUTA ENEO LA KUTA

Hapa tuta tumia kanuni ifuatayo

Eneo = Urefu( wa kuta) x kimo (urefu wa ukuta kwenda juu)

Sasa kujua urefu wa kuta zote, utatakiwa kujumlisha urefu wa kuta zote

Kwenye mchoro wetu pale juu nime weka namba kila kuta hivyo itakuwa kama ifuatavyo {vipimo vipo katika milimita (mm)}.

1 m = 100 cm = 1,000 mm; 1 cm = 10 mm

Ukuta 1= 6,500 mm; ukuta 2 = 9,150 mm; ukuta 3 = 4,000 mm; ukuta 4 = 4,000 mm; ukuta 5 = 9,450 mm

Ukuta 6=11,046 mm, ukuta 7=6196 mm +3200 mm, ukuta 8=9,101 mm, ukuta 9 =3,060 mm, ukuta 10 = 2,900 mm

Sasa uki jumlisha kuta hizo zote unapata jumla ya = 68,603 mm

Eneo la kuta = urefu wa kuta x kimo cha kuta

Hapa kama utajenga nyumba ya kozi 13 maana yake ni kimo cha 3000 mm

Hivyo eneo litakuwa = 68,603 x 3000= 205,809,000 mm

Sasa kumbuka tuna sehemu za wazi ambazo hizi hazihitaji tofali, mfano milango, madirisha na sehemu za wazi za vibaraza

Kanuni ni ile ile urefu x kimo:

Tuna madirisha 6 yenye urefu 2,000 mm & kimo 1,800 mm= 2000 x 1800 sawa na 3,600,000 mm

sasa, tuna madirisha sita yenye vipimo sawa hivyo 3,600,000 x 6 = 21,600,000

Tumia dirisha 1 lenye urefu 1,400 na kimo 1,500 = 1,400 x 1500 sawa na 2,100,000 mm

Tuna dirisha 1 lenye urefu 1,000 na kimo 1,800 = 1,000x1, 800 sawa na 1,800,000 mm

Tuna madirisha 2 yenye urefu wa 800 na kimo 600 = 800x600 sawa na 480,000 mm

480,000 zidisha kwa 2 sawa na 960,000 mm

Tuna milango 9 yenye urefu wa 900 na kimo 2,400 = 900 x 2,400 sawa na 2,160,000 mm

2,160,000 zidisha kwa 9 sawa na 19,440,000 mm

Uwazi wa vibaraza jumla uref 10,010 kimo 2,400 =10,010 x 2,400 sawa na 24,024,000 mm

Jumla ya wazi = 21,600,000 + 2,100,000 + 1,800,000 + 960,000 +19,440,000 + 24,024,000 = 69,924,000 mm

Eneo kamili linalo hitaji tofali za kuta lita kuwa

ENEO LA KUTA — ENEO LA WAZI0 = 205,809,000–69,924,000= 135,885,000 mm

hivyo basi, IDADI YA TOFALI, itakuwa kama ifuatavyo:

Sasa urefu wa msingi wako utategemea na nature ya eneo lakini tuchukulie utakuwa na urefu wa 900 mm, ambapo ni sehemu tambarare (isiyo korofi)

Kumbuka jumla ya urefu wa kuta zote ni 68,603 mm

Kwahiyo 68,603x900 = 61,742,700 mm

Kwahiyo kupata tofali tutalazimika kuchukua jumla ya ukubwa wa kuta ukiwa umetoa uwazi na jumla ya eneo la kuta za msingi kisha tuta gawanya kwa eneo la tofali moja

135,885,000+61,742,700= 197,627,700 mm

Kumbuka tofali ya block lina urefu wa 450 mm na kimo cha 230 mm

Hivyo eneo la tofali ni 450 x 230=103,500 mm

Idadi ya tofali itapatikana kwa 197,627,700mm/103,500mm = 1,909 matofali

Hapa utahitaji kuongeza asilimia kidogo ya tofali kwaajili ya zile zitakazo vunjika na ngazi pia, tutatumia 5%, kwahiyo jumla ni tafali 1909+ 0.05(1909) = 2,004.45 ≈ 2,000 tofali

MAHESABU YA IDADI YA MIFUKO YA CEMENT NA MCHANGA INAYO HITAJIKA KUJENGEA NYUMBA YAKO

hapa tunaingia sehemu nyingine ambayo itahusu ukadiliaji wa idadi ya mifuko ya cement itakayo hitajika kujengea jengo lako.

NB: kumbuka haya huwa ni makadilio, hivyo sio lazima yawe sawa kwa asilimia 100, lakini mara nyingi yanakaribia ukweli halisi kwa asilimia kubwa sana

Tukichukulia mfano wa TOFALI 2,000

Hapa nazungumzia tofali ambazo wengi wanaziita za block, ambazo kitaalamu zinaitwa SAND CEMENT BLOCKS

Hapa tuseme idadi ya tofali za Msingi (inch 6) ni tofali 700

Idadi ya tofali za kuta (inch 5) ni tofali 1300

A: IDADI YA MIFUKO YA CEMENT KWAAJILI YA MSINGI (TOFALI ZA INCH 6)

-Ikumbukwe hapa tofali hizi hujengwa kwa kulazwa

-hivyo tofali hizi zitahitaji cement na mchanga Zaidi kuliko zile za kusimama (inch 5)

KANUNI

Mfuko 1 wa cement unajenga tofali 45 za msingi (inch 6- za kulaza)

Hivyo ukichukulia zile tofali 700 za msingi kwenye ule mfano wetu itakuwa ifuatavyo

Tofali 700 gawanya kwa 45 = 15.5 sawa na mifuko 16 ya cement

NB: (ikumbukwe watu wengine hufanya mfuko 1 wa cement unajenga tofali 50 ama 60 za msingi za kulaza). Hii hufanywa ili kupunguza gharama japo kama ni kwenye kiwanja korofi inaweza kuleta shida.

B: IDADI YA MIFUKO YA CEMENT KWAAJILI YA KUTA (TOFALI ZA INCH 5)

-Tofali hizi mara nyingi hujengwa kwa kusimama hivyo hazili mchanga na cement nyingi kama zile za msingi

KANUNI

Hapa mfuko 1 wa cement unajenga tofali 60 za kuta (inch 5- za kusimama)

Hivyo ukichukulia tofali 1,300 za kuta kwenye ule mfano wetu, itakuwa kama ifuatavyo

Tofali 1,300 gawanya kwa 60 = 21.6 sawa na mifuko 22 ya cement

NB: (ikumbukwe watu wengine hufanya mfuko 1 wa cement unajenga tofali 70 mpaka 90 za kuta, za kusimama), pia hii ni ili kupunguza gharama.

NB: KIPIMO CHA MCHANGA

Mfuko 1 wa CEMENT una changanywa na NDOO 9 kubwa za MCHANGA

Ama mfuko 1 wa CEMENT unachanganywa na NDOO 18 ndogo za MCHANGA

KWA WENYE MPANGO WA KUJENGA VITUO VYA MAFUTA MSISAHAU KUSOMA KITABU HIKI.

View attachment 3146144

View attachment 3146145
Hiki kitabu unaweza kudownload hapa: Mwongozo wa Ujenzi na Uendeshaji wa Vituo vya Mafuta kwa Gharama Nafuu

NYUMBA YAKO INAVUJA KIPINDI CHA MVUA?
Mtafute huyu fundi huto ona nyumba yako ikivuja tena katika kipindi cha mvua: Fundi wa Kuziba Bati linalovuja kwa Silicone
Nitasoma nikitulia naona idia nzuri
 
Watanzania hua ni wachoyo na wanafki sana, Ukitoa elimu ya kitu kizuri wanatafuta makosa tu ilimradi wakosoe na wengi wao wanataaluma hiyo au mafundi wanajisikia vibaya watu wengine kujua,
Nani asiye jua kama tofali la kuchoma na block lina vipimo tofauti,
Kaka umetoa elimu kubwa sana na kosa waliloona ni kipimo cha tofali la kuchoma tu.

Acheni unafiki

Ni mimi Accapulco bay
Kukosoa sio jambo baya ikiwa ukosoaji huo hulenga kujenga. Nadhani mtoa mada analijua hilo ndio maana hata kwenye majibu yake yupo humble.

Kwa mfano bricks na blocks dimension zake kaziweka zinafanana jambo ambalo halipo sawa.

Lakini vyuo vinavyotoa kozi ya usanifu majengo amevitaja Ardhi Institute-Tabora na Ardhi institute-Morogoro jambo ambalo sio la kweli, badala yake angeweka Mbeya University of Science and Technology.
 
Back
Top Bottom