Jinsi ya kufanya windows yako iwake kwa haraka.

Jinsi ya kufanya windows yako iwake kwa haraka.

badshah

Member
Joined
Mar 16, 2013
Posts
51
Reaction score
32
JINSI YA KUFANYA WINDOWS YAKO IWAKE KWA HARAKA.
Kwa watumiaji wa Windows XP tu.

Fungua Notepad (start >> all programs >> accessories >> notepad) kisha andika maneno haya ndani ya notepad "del c:\windows\prefetch\ntosboot-*.* /q” bila kuweka hizo funga semi na fungua semi. Baada ya hapo save as ntosboot.bat na hakikisha chumba cha chini cha save as type umeweka all files na hakikisha unaisave katika local disk C. angalia picha hapo chini.
boot_faster.jpg



Baada ya hapo nenda start halafu tafuta neno Run au kwa kifupi bofya katika keyboard yako alama ya windows halafu kabla ya kuiachia bofya na herufi "R” baada ya hapo Run itatokea. Kisha andika maneno haya ndani yake "gpedit.msc” usiweke hizo funga semi na fungua semi kisha bofya neno ok au bofya enter kwenye keyboard.
run_with_gp_edit.jpg


Window itakayotokea utatafuta neno "Windows Settings” kisha utaclick hapo mara moja. Baada ya hapo kwa upande wa kulia uta double click neno Script (StartUp/ShutDown) kisha katika maneno mawili yatakayotokea utaDouble Click ShutDown. Hapa kuna window nyingine itatokea ndogo hivi, bofya button iliyoandikwa Add… (angali picha hapo chini)

g.policy.jpg


Kisha itatokea tena sehemu itakayokwambia add script… katika chumba cha Script name utabofya mbele yake button iliyoandikwa Browse… kisha utaenda kulitafuta lile faili ulilolisave hapo mwanzo katika local disk C ambalo ulilipa jina la ntosboot.bat kisha utaliselect halafu utabofya neno Open. Baada ya hapo utabofya tena ok katika windows yako ya add Script kisha itajifunga, halafu itabakia window ya Shutdown Properties ambayo nayo pia utaclick Apply halafu utaclick tena Ok kisha itajifunga. Funga kila kitu sasa twende kwenye hatua ya mwisho.

shutdown_properties.jpg


nenda start halafu tafuta neno Run au kwa kifupi bofya katika keyboard yako alama ya windows halafu kabla ya kuiachia bofya na herufi "R” baada ya hapo Run itatokea. Kisha andika maneno haya ndani yake "devmgmt.msc” usiweke hizo funga semi na fungua semi kisha bofya neno ok au bofya Enter kwenye keyboard.

Katika window itakayotokea Double click kwenye "IDE ATA/ATAPI controllers” kisha Right click kwenye neno "Primary IDE Channel" halafu click "Properties”.


dev_manager.jpg


Katika windows itakayotokea nenda kwenye sehemu inayoitwa "Advanced Settings" inapatikana kwa juu. Baada ya hapo kuna sehemu utaona za Device 0 na Device 1 hapa tafuta ile sehemu ya Device ambayo katika upande wa Device Type iko free kubadilishika yaani haijafungwa. Angalia picha hapo chini. Kisha sehemu hii ya device type chagua neno "None” badala ya neno Auto Detect. Kisha weka Ok.
Ide_Channel_Properties.jpg

halafu tena Right click kwenye neno "Secondary IDE Channel" halafu click "Properties”. Kisha fuata hatua zilezile ulizofanya katika Primary IDE Channel. Kisha weka OK halafu izime na uiwashe tena Kompyuta yako.

Hapo itawaka haraka sasa.

fore more: visit Staryte - Education, Entertainment & Development - Elimu, Burudani na Maendeleo
 
Mkuu kwa windo saba je?

Kwa win7 huna haja ya kutengeneza hilo faili hapo mwanzo, ila unachotakiwa hapa fuata hatua zifuatazo:

Go to Run, halafu andika msconfig kisha bofya Enter. Baada ya hapo itafunguka screen ya msconfig, kisha utaenda katika sehemu iliyoandikwa Sartup Inapatikana katika menu za juu kabisa kama kwenye picha hapo chini.


boottime-msconfig.jpg


Hiyo inamaana kuwa kuna program ambazo zinafunguka wakati windows inawaka na ukiangalia kuna nyingine hazina umuhimu hata kama hazifunguki, hivyo unatakiwa uondoe alama ya Tick katika kiboksi kinachoonyesha program ambayo unaona haifai kufunguka pale windows yako inapoanza, lakini unatakiwa tu uwe makini na uhakika juu ya hiyo program unayoiondolea Tick.

Kisha katika hiyohiyo msconfig nenda kwenye sehemu iliyoandikwa Services, kisha ondoa Tick katika Service ambayo unahisi haina umuhimu wa kufunguka pale windows inapowaka.

Kumbuka kuwa windows hucheleweshwa na application pamoja na services nyingi ambazo zinafunguka automatically pale computer inapowashwa hivyo kupunguza hizi kunasaidia kuondoa uzito wa windows yako kuwaka. Lakini unahitaji ujue vizuri hizi usije ukazima services ambazo ni muhimu.

Baada ya hapo hatua ya pili ni kama hiyo niliyoieleza ya win XP hapo, ambayo ni kuchagua neno "None" badala ya neno Auto Detect. Katika primary and Secondary IDE Channel.

Thanks a lot.
Staryte - Education, Entertainment & Development - Elimu, Burudani na Maendeleo
 
Back
Top Bottom