Jinsi ya kuficha TV cables ukutani

Jinsi ya kuficha TV cables ukutani

RRONDO

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2010
Posts
55,727
Reaction score
123,094
Kuweka TV ukutani inapendeza sana. Lakini hamna kitu kinakera kama kuona mawaya yananing'inia kutoka chini kwenda juu kwenye TV. Haipendezi kabisa na inaondoa uzuri wote wa eneo hilo.

Jinsi ya kuficha hizo cable ni rahisi sana. Wakati wa ujenzi unachimbia bomba ya kama 2 inches hivi ukutani, kama unavyochimbia bomba za umeme.

Bomba hii itakuwa wazi chini ambapo ni mkabala na switch socket zako na juu ambapo ni nyuma ya TV na cable zote zitaingia na kutokea hapo. Baadae unaipigia plaster na rangi kama bomba nyingine za waya. Then utakuwa na TV yako na sound bar ukutani bila waya kuonekana.

Credit: ngakotecture

Screenshot_20211210-094305.png
Screenshot_20211210-094250.png
 
Hiyo ni nzuri sana ila najaribu kufikiri namna nyingine ya kifanya hilo..

Ukifanya hivyo maana yake ni kwamba Sebule yako itakaa hvyo hvyo miaka yote ya maisha yako.

Tv na music system zitakaa palee miaka yote, jambo ambalo kwa upande wangu naliona halipo sawa.

Nipo nadesign movable Show Case ambalo litapigwa wiring lote na kufanya hayo uliyoshauri kwenye hilo Case zima.

Hii maana yake ni kwamba itasaidia nikitaka badilisha location ya Tv na Ile music system Nasukuma tu lile Case zima linaenda upande ninaotaka likakae.

Sioni kama ni busara Mtu kutoboa ukuta wa nyumba yake kwa jambo hili naona kama atajipa limitation mwenyewe na kuna wakati utafika hatoweza enjoy tena nyumba yake maana atakua kashaizoea sanaaa..

Na raha ya nyumba inatakiwa kila miaka miwili au mitatu (kulingana na mapendekezo ya mtu) unabadilisha Kila kitu pale seblen kuanzia style ya upangaji, Tv, Makochi,nk.

hii inafanya muda wote ujione upo kwenye nyumba mpyaa na nzuri na yakuvutia.

So kwa idea hiii ni nzuri ila nashauri ifanyike kwenye lile Movable Case kama Kabati flani hiviii...
 
Hiyo ni nzuri sana ila najaribu kufikiri namna nyingine ya kifanya hilo..

Ukifanya hivyo maana yake ni kwamba Sebule yako itakaa hvyo hvyo miaka yote ya maisha yako.

Tv na music system zitakaa palee miaka yote, jambo ambalo kwa upande wangu naliona halipo sawa.
Hapo ilipo ndio sehemu imetengwa vikae miaka yote. Pande nyingine zina madirisha labda kama wewe pande zote Una kuta kama hio ndio unaweza kuhamisha kila ukijisikia.

Kuhusu kubadili muonekano rangi na decor nyingine zinatosha.
 
Mimi mwenyewe kwa design ya nyumba yangu tv itakaa sehemu moja miaka yote maana pande nyingine zina madirisha makubwa
 
Mimi mwenyewe kwa design ya nyumba yangu tv itakaa sehemu moja miaka yote maana pande nyingine zina madirisha makubwa
Ndivyo ilivyo kwenye nyumba nyingi. Tv za siku hizi watu wanaweka ukutani.
 
Hii ni sawa lakini pia sio safi sana...

Hiyo PVC pipe badala ya kuwa wazi kwenye hayo matundu juu na chini (kwa kuweka L-connector), unaweza ukaifanya iishie ndani ya electric switch/socket box...

Hii itakupa nafasi ya kuficha huo uwazi kwa kutumia blank plastic plate pale unapokuwa huutumii huo ukuta kwa kuweka TV...

Nashindwa weka picha, naona kama app ya JF inasumbua kuattach picha

View attachment 2087855

Screenshot-20220119-123558-2.png

Hii ni sawa lakini pia sio safi sana...

Hiyo PVC pipe badala ya kuwa wazi kwenye hayo matundu juu na chini (kwa kuweka L-connector), unaweza ukaifanya iishie ndani ya electric switch/socket box...

Hii itakupa nafasi ya kuficha huo uwazi kwa kutumia blank plastic plate pale unapokuwa huutumii huo ukuta kwa kwa kuweka TV...

Nashindwa weka picha, naona kama app ya JF inasumbua kuattach picha
Nimependa proporsal yako, inakaa vizuri sana, ukiwa hupatumii unaweza funga hata socket ambayo haifanyi kazi
 
Back
Top Bottom