Wandugu, nashangaa sana, sikuwahi kuwa na hali hii.
Kila jioni mwili uota michirizi kama nimechapwa na fimbo hasa mgongoni.
Michirizi hii huongezeka nikijikuna, uwasha sana na inatokea pia kwenye mapaja, ubavuni na sehemu za mikononi kwa juu karibu na mabega.
Ni kama mdudu washa washa ametembea mwilini...ukioga inazidi, ila cha ajabu, ukiamka asubuhi haipo na mchana haionekani. Sijui ni tatizo gani kisayansi tiba.
Naandika ikiwa nawashwa sana na mishirizi kibao mgongoni.
Msaada tafadhali kama wadau mnafahamu chanzo na tiba yake.