SoC02 Jinsi ya kuijua fursa katika mazingira yako bila uzoefu mkubwa

SoC02 Jinsi ya kuijua fursa katika mazingira yako bila uzoefu mkubwa

Stories of Change - 2022 Competition

Miltony

Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
32
Reaction score
211
Katika karne ya leo ya 21 ni kweli ajira imekuwa ni kipengele kwetu sisi vijana na wengi wa wazazi wetu wanakwama pale wanapoamini kwamba kweli ufunguo wa maisha ni elimu wanasahau kwamba iyo elimu inaweza ikakukalisha nyumbani na yenyewe ni sawa na biashara tu mtaani kwani unawekeza mwisho wa siku unaweza pata faida au hasara na kujikuta tu nyumbani huna muelekeo.

Vijana tunaitaji kujitambua mapema sana hasa tukiangalia fursa zilizopo ndani ya uwezo wetu kwa mfano kuna biasha ambayo ukianza nayo haigharimi fedha nyingi ila shida inakuja kwamba sisi vijana usharobaro umetuzidi akili kwa kutupiga kwa kete nyingi sana unakuta kijana anatafta shilingi elfu ishirini kwa kubeba matofari na baada ya kuipata basi inaishia kwenye hesabu mbovu tu.

Kuna biashara kama biashara ya matunda biashara ambayo inakula nguvu lakini haitumii pesa na ndo inakamilika maana halisi ya kutafuta pesa kwa jasho mfano kwa kuanza biashara ya matunda hauitaji vitu vingi shilingi elfu kumi tu itakufanya kujiona bora zaidi kwa maana ya kuwekeza muda wako umakini wako pia katika biashara yako.

Tunakuja kuipigia iyo biashara kwa kuichambua taratibu iyo shilingi elfu kumi umetoa shiling elfu mbili umenunua zako papai moja kubwa, unatoa elfu moja unachukua parachichi zuri , unachukua elfu mbili unachukua nanasi moja safi, maembe ya buku pia na tango buku unabakiza elfu mbili ya kukulinda unachukua kindoo nyumbani unaanzia uko uko taratibu unajikuta ile elfu kumi imekuwa elfu ishirini unapanda chati ya kununua kindoo cheupe elfu sita unachujua vibakuli tu kwa muda huo kwa maana ndo unaanza hupaswi kuwa na haraka na muda huo kumbuka unazidi kuizoea biashara kadri muda unavyoenda unazidi kufanya maboresho ya hali ya taratibu mwisho wa siku unakuwa na mtaji mzuri unaweka kijana anakuwa anazungusha nawewe unaendelea na shughuli nyingine ukiwa tiyari umeshawekeza kwa hali ya kawaida ukiwekeza vizuri muda na kauli nzuri katika biashara hii unaweza pata faida hadi elfu ishirini kwa siku na zaidi.

Iyo ni moja tu ya biashara amabayo haitaji kukaaa darasani muda mrefu sana badala ya kusoma chuo na ukaja kuwa mzigo nyumbani na tatizo letu wengi tukishasoma tunaona tumemaliza maisha tunasahau kwamba muda unaenda na miaka inasonga kwa kasi na wazazi wetu kwa muda huo wanaokuwa wanatulinda kwa fedha zao inafikia muda wanaitaji sisi tuwahudumie bila kujali tuna kazi au hatuna na wengine wakiamini zaidi kwamba kama umesoma huwezi kosa pesa ila ni kweli njia ziko nyingi ila kikwazo kinakuja kwenye uelewa wako unaanza daah watu wataniona je elimu yangu yotr naishia kwenye matunda kweli? Naenda kuuza mikeka barabarani hapana ngoja nisubiri serikali itanipa kazi muda huo wenzako tushaanza zamani biashara ya matunda na tunafrahia na siku zote ukitaka ufanye vizuri kitu ridhika na ukifrahie hapo utakuwa umeiweka njia nzuri sana ya maishani kwako

Bila kujali umesomea wapi umelipa ada kiasi gani bado kama kijana kunayo nafasi nyingine ya kuonesha uwezo wa akili na kuionesha jamii kwamba sikuzaliwa kwa lengo baya la kutia hasara katika familia yangu kwa maana ya ada iliyolipa kupata iyo degree au masters naweza fanya jambo la ziada na ivyo ndivyo familia zetu zitanyanyuka kwa kasi tujiulize kwanini wenzetu unakuta mtoto ana miaka kumi lakini tiyari anacheza soka la kulipwa la watoto ?? Je ni kwamba wamesoma sana?? Je ni kwamba wana akili sana hata wasiposoma wanafanya vizuri??

Maswali ni mengi ila jibu ni hapana na kutambua jamii inataka nini kwa muda huo na unaweza kufanya nini kwa muda huo kikubwa ni kuitengeneza future bila kujali masomo wala vyeti , Kijana unaesoma hii makala leo nimekupa mfano wa matunda sijamaanisha kwamba ukakomae na matunda labda ni kucheza na fursa na kuitambua pia kuifanyia kazi sio kuijua ukaishia hapo ukidhani itakulipa hapana inaitaji utulivu wa hali ya juu unaweza kupitia sehemu tofauti tofauti kuona iyo fursa uliyoichagua kusoma mienendo yake kwa maana ya changamoto kwa kufanya ivyo utanikumbuka na hapo utakuwa na cheti chako pia na pesa yako bila mawazooo

#Kijana amka sasa tuzipambanie familia zetu zinatutegemea kwa kuruka viunzi vyote Mungu atutangulie.
Ila hapo hapo tukumbuke kuwa Mungu ndo mwenye kutupa nguvu na moyo wa kuendelea kupambana kwa udhamini wa pumzi yake anayotupea bure basi kama vijana tuishi katika yeye tukiamini katika utendaji wake kwa muda wote kwani bila yeye sisi hatuwezi kufanya chochote kile katika maisha yetu tukubali kukabidhi kila kilicho chetu mikononi mwake ila mambo yatunyokeee atufanye tuwe kama Daudi ambae pamoja na mihangaiko yake yote Mungu alikuwa anaona ndoto yake naye akaikamilisha bila mtu kutarajia na kumfanya Waziri mkuu sisi ni akina nani tushindweee?

Sisi tumekosea wapi tusiende mbele? Sisi ni akina nani tusimnyenyekee yeye hakika pamoja na yote kila ukiiona alfajiri basi jua ya kwamba umechaguliwa katika washindi wa siku nawewe usiruhusu iyo siku kwenda bure haijalishi unasoma au la fanya juhudi za kumuonesha Mungu uwezo wako aliokuopa kwamba unaweza kuutumia vizuri sana kwa namna hiyo atakupa uwezo zaidi wa kutafakari muelekeo wako zaidi ya wewe unapofkria atakufanya kuziona fursa ambazo zilipangwa kuonekana mbele yako na sio wengine kwa kila mtu kapangiwa chake na Muumba issue ni unakipataje au unakiona je icho kilicho chako?? Kaa karibu na Mungu kila kitu kinawezekana kwa nguvu za Muumba.

Vijana tunayo kazi ya kuzipandisha familia zetu juu zaidi ya zilipo na taifa kwa ujumla
 
Upvote 7
Back
Top Bottom