Jinsi ya kuitumia Katiba

Jinsi ya kuitumia Katiba

SEMKIWA3

Senior Member
Joined
Feb 17, 2019
Posts
103
Reaction score
59
Habari wanaJF.

Mimi raia wa Tanzania,leo nimepitia jukwaa hili ili kutaka kujuzwa mawili matatu kuhusu jinsi na namna ya kuitumia katiba yetu pendwa.

Nimeomba kupewa maelezo ya jinsi ya kuitumia sababu napenda sana kuzijua haki na taratibu za maisha ya watanzania kulingana na katiba yetu ya Tanzania,shida inakuja kwenye kuielewa sasa ile katiba.

Kwa mfano juzi nilitaka nizijue sheria za ardhi,lakini sijaambulia kuona chochote kile kutoka kwenye katiba,lakini nilijaribu kuomba msaada kwa google nao wakaniletea mambo mengi mengi kuhusu sheria ya ardhi vivo hivyo nikajaribu tena kuangalia sheria ya ndoa lengo langu lilikuwa kutaka kujua majukumu ya mama na baba katika familia na haki za mama katika ndoa,lakini pia nilitoka kapa,ila nikaingia kwa google ili kupata msaada napo hapo wakaleta kile kitu roho inapenda.

Msaada wadau nijuzeni hili swala la katiba,pia mniambie hizi sheria kama za Ndoa,Ardhi na nyingine maelezo yake huwa yanaandikwa kwenye vitabu gani au kutafsiriwa wapi sababu kule kwenye katiba sioni kitu kule.

Picha za chini hapa nimejaribu kuonyesha jinsi nilivoitafuta sheria ya ndoa katika katiba yetu na picha nyengine ikionyesha sheria ya haki za mama kwa kumtumia google.

Awali ya yote mimi nimesoma PCB hivyo basi haya mambo mengine siyaelewi lakini sina budi kuyajua kupitia kwenu watanzania wenzangu.
Ahsanteni
Screenshot_20190427-094255.jpeg
Screenshot_20190427-093834.jpeg
 
Back
Top Bottom