SoC01 Jinsi ya kujikwamua na ukosefu wa Ajira

SoC01 Jinsi ya kujikwamua na ukosefu wa Ajira

Stories of Change - 2021 Competition

Japhet2580

New Member
Joined
Jul 18, 2021
Posts
1
Reaction score
1
Habari za leo ndugu zangu Watanzania natumaini wote ni wazima wa afya.

Nachukua hatua hii kuwapa hongera wanachuo wote na wanafunzi wote wa elimu mbalimbali ambao wanamaliza masomo yao mwaka huu 2021 katika kozi mbalimbali hongeleni Sana!.

Nina ujumbe kwenu ambao utabadilisha maisha yenu na kuwasogeza katika hatua za mafanikio na kulishinda swala la ukosefu wa ajira.

Ni ndoto ya kila mtu baada ya safari ndefu ya masomo kuanzia elimu ya msingi hadi chuo kikuu kupata ajira ambayo itampatia kipato cha kujikimu kimaisha na pia lazima ifahamike ajira ni daraja la kukufikisha katika mafanikio yako. Lakini kila mtu anandoto ya maisha yake ambapo ndoto hiyo utakuta inakwamishwa au kucheleweshwa na mtu mwenyewe kwasababu ya kupoteza muda katika kusubiri ajira baada ya kuhitimisha masomo yake .

Katika Taifa letu la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kumekua na malalamiko ya vijana wengi kukosa ajira baada ya masomo yao hii ni kutokana na nafasi za ajira zinazotangazwa ni chache sana kuliko wasomi wanaomaliza kila mwaka hivyo basi Kama kijana msomi lazima uwe watofauti na zingatia mambo haya hili ufanikiwe kupambana na soko la ajira

1. ONDOA UOGA
Uoga ni kitu kibaya sana na unakwamisha watu wengi katika kufikia mafanikio, Wakati unasubiri ajira hakikisha unakitu cha kufanya...

(i) Usiogope kufanya kazi, Fanya kazi yoyote hata Kama umesomea Ualimu na ajira hujapata fanya hata kazi ya ulinzi.

(ii) Usiogope katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, Mfano.. M/kiti wa mtaa,Udiwani na Ubunge maana hivyo vyote vipo kwaajiri ya Mtanzania cha muhimu hakikisha unakadi ya chama kinacho tambulika.

(iii) Usiogope kujitolea katika shughuri mbalimbali za kijamii kwa moyo wote katika kujitolea kwako inaweza ikawa ni mlango wako wa kupata ajira.

2. JENGA USHIRIKIANO
Katika vitu ambavyo hukwamisha watu wengi ni swala la ubinafsi, kila mtu anapambana mwenyewe pasipo kuwa na ushirikiano. Usirikiano unauwezo mkubwa wa kupambana na ukosefu wa ajira kwa namna ifuatavyo;

(i) Kupata mikopo ya Serikali, Serikali imekua ikiwapaitia mikopo vikundi mbalimbali ambayo inakua ni sehemu ya mitaji katika kuanzisha vitu mbalimbali vitakavyobuniwa na kundi husika. Hivyo basi vijana hakikisheni mnaungana na kuanzisha vikundi,mfano... mliosoma pamoja na Kupata mkopo mkajikwamua katika ukosefu wa ajira.

(ii) Kupata njia mbalimbali,Kwa kishirikiana na watu wengine unaweza ukapata njia rahisi ya kuingiza kipato bila kupoteza muda wa kupata ajira.

3. TUMIA FURSA
Fursa yoyote ambayo unawepesi kuianza wewe pasipo mtaji mkubwa ianze haraka bila kuchelewa mfano...

(i) Fursa ya kilimo,
Kuna baadhi ya vijana ambao wazazi wao wana mashamba mengi kiasi kwamb mengine hawayalimi basi tumia fusra hiyo kuwaomba wazazi wako shamba hili uanze kilimo na wekeza maarifa ya elimu yako hapo utafanikiwa.

(ii) Fursa ya ufugaji,
Wengine wana wazazi na ndugu ambao Ni wafugaji waombe mbegu kisha anza kuzalisha utafanikiwa .
Kwa ujumla fursa ya aina yoyote usikubari ikupite hakikisha chochote ambacho ni rahisi kukianza unakifanya haraka.

HITIMISHO

Natoa wito kwa vijana wenzangu wote tujitahidi sana kujiari, tusipoteze muda kusubiri ajira ,Ajira isiwe ndio tumaini la mwisho ikapelekea kukata tamaa .Tuishi katika ndoto zetu ajira hiwe ni sehemu ya daraja kufikia ndoto zetu.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom