figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
Salaam Wakuu,
Hii ndo namna bora ya kujitengenezea heshima.
1. Acha kuwaomba watu kila wakati. Acha kuwa ombaomba kwa marafiki
2. Acha kutafuta asiyekutafuta. Mtu kama anakukalia kimya nawe Mkalie kiya
3.Usiwe muongeaji sana bali msikilizaji
4. Usile chakula cha watu wengine zaidi ya wao wanavyokula chaula chako.
5. Punguza jinsi unavyowatembelea baadhi ya watu hasa pale wanapokuwa hawaonyeshi kujali unapowatembelea
6. Kumbuka kujitengenezea furaha yako, usitegemee furaha kutoka wa watu.
7. Acha kuendekeza umbea na kufuatilia mambo ya watu
8. Fikiri kabla ya kuzungumza. Asilimia 80 ya jinsi watu wanakutathimini kutokana na maneno yanayotoka kinywani mwako.
9. Kuwa mfanisi kwa kujishughulisha na lengo lako. Fuata mambo yako si ya wengine
10. Heshimu watu wote wakati wote.
11. Usikae kwenye uhusiano|mahusiano ambayo unadharauliwa kila mara.
12. Kuwa na hofu wakati mwingine. Sio kila kitu ujione unakimudu. Wasiwasi ndo akili
13. Uwe mtoaji zaidi kuliko mpokeaji. Jitahidi kutoa zaidi
14. Jifunze jinsi ya kutumia pesa yako mwenyewe kuliko kutumia pesa ya wengine
15. Usiende mahali ambapo Hujaalikwa na ukialikwa usikaribishe watu wengine.
16. Watendee watu jinsi wanavyostahili.
17. Usipigie mtu simu mara nyingi. Ukipiga mara ,mbili asipokee inatosha, kama anakuthamini atakupigia baadaye
18. Kuwa mzuri katika kile unachofanya na kifanye kwa ubora kadri uwezavyo.[jitengenezee 18 zako ambazo mtu akiingia ameisha]
19. Tunza ahadi na utimize ahadi
20. Tunza utu wako
21. Shukuru kwa kila jambo
Ni hayo tu