Jinsi ya kukaanga mihogo na chachandu

Jinsi ya kukaanga mihogo na chachandu

Tume ya Katiba

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
4,896
Reaction score
1,862
Declare Interest:

Mimi jukwaa langu ni la siasa, huku nimekuja leo na sitorudi tena.

Why MIHOGO?

1) Rahisi kupatikana
2) Kila mtanzania anaijua sio kama mara egg chop, fish finger, Streetwise, KATLESS mapishi ambayo hata ujui utatoa wapi material! Majina ya ajabu ajabu.
3) Kila aliyepitia shule za msingi, secondary anajua utamu wa mihogo ya kukaanga na chachandu(masaro) hasa ya nyanya za kuoza.

Ok

Here we go


Ingredients


  • Mihogo mikubwa 3
  • mafuta lita 1
  • kitunguu 1
  • thoum kiasi
  • tangawizi kiasi
  • nyanya 4
  • limao 1
  • karoti nusu
  • hoho nusu
  • pilipili manga kidogo
  • chumvi
  • pilipili mbichi.

Directions


  1. Menya mihogo, ikatekate kiasi upendacho na kwa urahisi wa kuiva kisha ikoshe
  2. bandika karai, tia mafuta, yakipata moto weka mihogo ukaange, angalia moto usiwe mkali sana ili mihogo iive polepooe bila kubabuka
  3. ikishaiva itoe uitie kwenye chujio ijichuje mafuta. Anza kuandaa kachumbari yakulia mihogo.
  4. osha nyanya, karoti, hoho, tangawizi, chukua sufuria uvisage uvitie, kisha katakata kitunguu tia, twanga pilipili uitie pia. Weka chumvi na pilipili manga.
  5. bandika jikoni ueke na maji nusu kikombe na unyunyuzie mafuta kiasi. Funika acha ichemke kiasi dakika 5
  6. Kisha tia limau uache ichemke kidogo, epua kachumbari yetu yakulia mihogo tayari.


Sasa mihogo yetu twaweza kuila muda wowote, kwa chai, maji na hata juisi na hata ukipata samaki wakukaanga hunoga mno. Nasio lazima uwe na kachumbari waweza kula na tomato, chilli sio mbaya,

Karibuni sana.


Hii kitu nimeikopi hapo chini kwenye link

Mapishi | Jinsi ya Kupika | Blogu #1 Kwa Mapishi Mbalimbali ya Kiswahili

mihogo ya kukaanga na chachandu | Jinsi Ya Kupika
 
safi saha, hasa ukipata muhogo unaoiva vizuri sio uwe cherema.
 
Mhhhh, hapo uliposema nyanya za kuoza (masalo)......
Ila asante kwa kushare nasi.
 
Hiyo mihogo ushushie na askrimu ya ukwaju mweeeee asikwambie mtu
 
Hiyo mihogo ushushie na askrimu ya ukwaju mweeeee asikwambie mtu

mwe umenikumbusha pale mgulani primary, mihogo na askrimu ndo zangu, hela yangu ya shule mara nyingi huishia hapo
 
Ngoja tujaribu,ila ktk ukaangaji wa mihogo inabid uweke na maji kidogo ili iwe laini,
 
Back
Top Bottom