Jinsi ya kukabiliana na foleni ya kutisha jijini Dar

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2015
Posts
27,031
Reaction score
49,928
Siku hizi kuna foleni ya kutisha maeneo mengi ya Dar. Yaani Hali ni tete
Jinsi ya kupunguza makali

Kwanza: Beba vitu vya Kula, bites zisikosekane kwenye gari au kama ni wa public transport kwenye pochi au kibegi Beba misosi na maji. Juzi kidogo nizimie nnavyopenda kula, masaa mawili tumesimama pale Mwenge, nimekoma

Pili: Jitahidi kuwahi kuondoka nyumbani kwenda unapotaka.

Kama umealikwa harusini saa mbili usiku, Fanya Tu kuondoka nyumbani saa Tisa mchana, saa kumi na mbili uwe ukumbini. Ukitoka nyumbani saa moja jioni utafika watu washaenda honeymoon na mtoto ashazaliwa.

Jana nilikutana na msafara wa Bibi harusi saa Tatu sijui walienda kupiga picha wapi Ile Mbezi ya chini, alikuwa analia tu njia nzima magari hayatembei. Sijui walienda kukuta wageni?

Tatu: Usipende kutoka na watoto wadogo bila sababu za msingi; ni kuwatesa. Njaa, kujisaidia etc sio fair

Nne: Kama sio lazima sana, usitoke na gari tumia tu boda. Sema ukimwagwa huko utajua mwenyewe!

Ila muhimu tunaomba serikali iingilie Kati jamani tunateseka
 
Kuna kamba ilikuwepo jana Sam Mujoma Rd aisee. Huu ujenzi wa BRT utatunyoosha.
Kikubwa hapo ni kucheza na rush hours.
 
Hi! Miss Natafuta ! Hivi kwanza bado hujapata? Halafu, kwani unatafutaga nini eti?

Kuhusu mada, nadhani Watanzania waanze kwenda na wakati. Kwa nini hujapendekeza serikali inunue mamia ya maelfu ya drones wagawiwe kila mtu ili zitumike kurukia juu kwa juu kutoka eneo moja hadi lingine?

Huoni kwamba kwa njia hiyo, hilo litachechemua suala zima la uchumi mkubwa kwenye taifa?
 
Hameni Dar mje huku Mpigamiti, hakuna mateso kama hayo..😜
Nasie tunao tokea vijijini sindio tutakua tunasafiri na maghala ya misosi kabisa mkuu..🤔
 
Hi! Miss Natafuta ! Hivi kwanza bado hujapata? Halafu, kwani unatafutaga nini eti?

Kuhusu mada, nadhani Watanzania waanze kwenda na wakati. Kwa nini hujapendekeza serikali inunue drones wagawiwe kila mtu ili zitumike kurukia juu kwa juu kutoka eneo moja hadi lingine?

Huoni kwamba kwa njia hiyo hilo litachechemua suala zima la uchumi mkubwa kwenye taifa?
Nakutafuta wewe bna.
WA kununua drone hakuna labda wanunue ungo
 
Kuna kamba ilikuwepo jana Sam Mujoma Rd aisee. Huu ujenzi wa BRT utatunyoosha.
Kikubwa hapo ni kucheza na rush hours.
Mimi Jana nimeliq yaani Acha tu .kila unaposema upite magari kama yote
 
Jana palikua na graduation ya vijana wa udsm pale mliman city so barabara ya bagamoyo, sam najoma pamoja na feed load zote zilikua tait
 
Siku hizi kuna foleni ya kutisha maeneo mengi ya Dar. Yaani Hali ni tete
Jinsi ya kupunguza makali

Kwanza: Beba vitu vya Kula, bites zisikosekane kwenye gari au kama ni wa public transport kwenye pochi au kibegi Beba misosi na maji. Juzi kidogo nizimie nnavyopenda kula, masaa mawili tumesimama pale Mwenge, nimekoma

Pili: Jitahidi kuwahi kuondoka nyumbani kwenda unapotaka.

Kama umealikwa harusini saa mbili usiku, Fanya Tu kuondoka nyumbani saa Tisa mchana, saa kumi na mbili uwe ukumbini. Ukitoka nyumbani saa moja jioni utafika watu washaenda honeymoon na mtoto ashazaliwa.

Jana nilikutana na msafara wa Bibi harusi saa Tatu sijui walienda kupiga picha wapi Ile Mbezi ya chini, alikuwa analia tu njia nzima magari hayatembei. Sijui walienda kukuta wageni?

Tatu: Usipende kutoka na watoto wadogo bila sababu za msingi; ni kuwatesa. Njaa, kujisaidia etc sio fair

Nne: Kama sio lazima sana, usitoke na gari tumia tu boda. Sema ukimwagwa huko utajua mwenyewe!

Ila muhimu tunaomba serikali iingilie Kati jamani tunateseka
Serikali wamekusikia, wataongeza kodi ya magari mara mbili ili kupunguza idadi.
 
Back
Top Bottom