Loading failed
JF-Expert Member
- Sep 14, 2023
- 2,603
- 7,501
Ndugu zangu
sio wanaume wote ni waadilifu, vilevile siyo kila Mwanamke huwa mpenda ugomvi.
kuna wanaume hutumia upole, huruma, kujali, kunyenyekea, kusamehe makosa, uvumilivu ambao mwanamke anaonyesha wanatumia kama UDHAIFU,akiona Mwanamke hana kazi,hana fedha,hana ndugu ,ni mgonjwa anatumia fursa hiyo kumpiga, kumfokea, kumtukana, kumkashifu, kumkaripia, kumgombeza, kumdhalilisha,kumnyima chakula, kumfukuza usiku wa manane,kumlaza nje n.k ujumbe huu hauna lengo la kuwazungumzia WANAUME wa kundi hilo.
ujumbe huu unazungumzia wanaume waadilifu,wenye heshima,upendo,wenye kutaka kujenga familia imara yenye upendo , huruma na mshikamano lakini wamepata wanawake wenye tabia za ubabe, udikteta, udhalilishaji, dharau, majivuno, kiburi jeuri na ujuaji.
Ninazungumzia wanawake wenye misimamo mikali sana (rigid),Mwanamke mjuaji,asieshaurika,Mwanamke mwenye majibu ya mkato, mwanamke asiekuwa na shukurani wala uvumilivu,nazungumzia Mwanamke ambaye anataka kumbambikia kesi mwanaume wake,Mwanamke anayesaliti na kumgeuzia kibao mwanaume, ninazungumzia mwanamke anaetoroka kwenda nyumbani kwao kisha anasingizia kunyanyaswa wakati yeye mwenyewe ndiyo anayefanya unyanyasaji kwa mwanaume wake, ninazungumzia wanawake wenye kutaka mashindano, mabishano, majibizano,mijadala,kupeana kashfa na tuhuma za usaliti, kutishiana kuachana namna gani ya kukabiliana na maudhi yake.
Ifahamike kwamba Mwanamke akimuamini mwanaume anakuwa laini sana,anakuwa mpole sana,anajilegeza,anakuwa na shukurani,anakuwa anaomba msamaha mwenyewe,anakuwa anajituma sana kumfurahisha mwanaume wake lakini akiwa na hasira kupitiliza,ubabe,tabia ya kisasi,wivu wa mapenzi uliopindukia huyo hafai kujenga naye uhusiano imara kwa sababu anakuwa kama mwanaume ndani ya mwili wa Mwanamke.
NB: Ujumbe huu ni mrefu kwa sababu sijaandika kwa ajili ya kusomwa na kila mtu ambaye anapatikana mtandaoni bali watu wenye kusoma makala ndefu na vitabu pekee
ZIFUATAZO NI NJIA 7 AMBAZO WANAWAKE HUZITUMIA KUMFANYIA MWANAUME MAUDHI/ VITIMBI NA UFUMBUZI WAKE
Njia 7 ambazo Mwanamke huwa anazitumia kumfanyia mwanaume maudhi, vituko,vitimbi na majaribu ya mara kwa mara ambapo wanaume wengi huwa wanachanganyikiwa na
Wataalamu wa saikolojia wameita maudhi, vituko, vitimbi na majaribu ya Mwanamke kama Female shit test na tabia hizi zipo kwa wanawake wote mwisho kabisa ni UFUMBUZI WAKE
1.KUMPIMA MWANAUME UWEZO WA KUJIAMINI (confidence test)
Mwanamke akimuona mwanaume kwa mara ya kwanza huwa anajaribu kupima kujiamini kwa mwanaume husika.
Hapa Mwanamke atatumia maneno kama "wewe siyo wa hadhi yangu",au "unaonekana ni mshamba mshamba",au "umewahi kuongea na Mwanamke mzuri kama mimi ?",au anaweza kumfokea, kumtukana, kumkashifu, kumkaripia, kumjibu vibaya, kudhalilisha, kumgombeza mwanaume pamoja na kuonyesha dharau, kiburi na majivuno kwa makusudi.
Kosa kubwa wanaume wengi hufanya ni kupaniki, kukasirika sana, kuchanganyikiwa,kumjibu vibaya , kumtishia kumdhuru, kufokeana, kutukanana, kujibizana,wengine huanza kulia, kuomba msamaha na wengine hupoteza uwezo wa kujieleza.
Ufumbuzi wake
Hakikisha unakuwa na UTULIVU WA AKILI kuliko kipindi chochote maishani mwako.
Mtazame usoni bila kuonyesha hasira,ongea kwa ufasaha huku ukitumia sauti nzito yenye mamlaka ya mwanaume Rijali mwambie "Ninakuheshimu sana ninaomba tuheshimiane sipo tayari tuvunjiane heshima eneo hili... Kaa kimya kwa sekunde kadhaa mtazame usoni..Hapo anaweza kukuomba msamaha kwa kosa ambalo amefanya au anaweza kuondoka kwa fedheha na aibu kubwa.
Akiomba msamaha ongea naye kwa utulivu,akiondoka achana naye yeye sio Mwanamke pekee hapa ulimwenguni.
2.KUPIMA UANAUME WA MWANAUME (DOMINANCE TEST)
Wanawake wenye tabia za udikteta, ubabe, ukatili, udhalilishaji, wasioheshimu baba zao,ambao hawana maelewano mazuri na baba zao hufanya jaribio hili mara kwa mara tena kwa kujua au kutokujua.
Anafanya makosa kwa makusudi kabisa kisha anageuza kibao kwako,anamgeuza mwanaume wake kama mtoto mdogo kwa kumfokea, kumtukana, kumkashifu, kumkaripia, kumjibu vibaya, kumtishia kumuacha, kumgombeza mara kwa mara.
Atakuwa anakujibu kwa jeuri, dharau,kiburi na majivuno wala hajali chochote.Anaweza kumwambia mwanaume toa mshahara wako wote nipange matumizi kama huwezi tuachane,anaweza kumpiga marufuku mwanaume wake kuzungumza na wazazi wake au ndugu zake,atakwambia chagua mimi au mama yako mzazi pamoja na ndugu zako,akikwazana na mwanaume atamuamrisha mwanaume kulala sebuleni au chumba tofauti au kulala mzungu wa nne, anaweza kugoma kumpa unyumba mwanaume kwa makusudi mpaka mwanaume aishi vile ambavyo amepewa maagizo, anaweza kumuamrisha mwanaume kufanya usafi wa nyumbani wakati huohuo yeye (Mwanamke) hana kazi wala dharura yoyote, anaweza kutoka nyumbani bila ruhusa wala taarifa yoyote,anatoka muda wowote na kurudi muda wowote, anaweza kutoroka kwenda kwao mara kwa mara haombi msamaha akifanya makosa ila anakaa kimya hatoi ushirikiano wowote kwako, anaweza kumuomba mwanaume kiasi kikubwa sana cha fedha kuliko uwezo wa mwanaume.
Ufumbuzi wake
Mwanaume unapoishi na Mwanamke mwenye tabia hizo hapo juu epuka kupaniki, epuka kuonyesha hasira, epuka kuanza kulia,epuka kuomba msamaha,epuka kumpa fedha nyingi ili abadilike,epuka kumpa ushauri,epuka kumbembeleza,epuka kumkumbusha wema ambao umefanya kwake.
UFUMBUZI WAKE
Mwanamke ambaye anataka kuwa KICHWA cha familia hafai kuwa mama watoto wako kwa sababu watoto watakudharau,watakuona haujielewi,utamkosa huyo Mwanamke na utawakosa watoto wako muda si mrefu,utafokewa, kutukanwa, kujibiwa vibaya, kudhalilishwa hadharani tena ambao watafanya hayo ni mke wako pamoja na watoto wako kwa sababu hawaoni kama wanaishi na mwanaume ndani ya familia.Rudisha huyo Mwanamke kwao akae na mama yake kwa sababu wanawake wa tabia hizo huwa hawana baba anaejielewa.
3.KUPIMA WIVU WA MWANAUME (Jealous test)
Mwanamke anaweza kumpima mwanaume kwa kumfanyia vituko, vitimbi, maudhi, majaribu ya mara kwa mara kwa kupima wivu wa mapenzi.
Ataonyesha tabia zifuatazo atasema "kuna mwanaume ananitongoza" anaweza kumtaja au kuonyesha sms lengo uone wivu, anaweza kuvaa nguo za ajabu ajabu kisha atajifanya hajui lengo uongee chochote aone upo na wivu,anaweza kuanza kusimulia habari za ex wake , anaweza kutongozwa na mwanaume mwengine mbele yako lengo uone wivu, anaweza kutishia muachane mara kwa mara ili uone wivu, anaweza kupuuza simu zako na sms zako hajibu kwa makusudi kabisa lengo uone wivu.
UFUMBUZI WAKE
Hakikisha akili ipo na UTULIVU wa hali ya juu sana kuliko kipindi chochote maishani mwako.
Epuka kumnyenyekea,epuka kupaniki, epuka kukasirika,epuka kumpa vitisho, epuka kuonyesha huzuni kwake,epuka kupekua simu yake,epuka kumfuatilia kimyakimya.
Kaa kwa utulivu kabisa kisha ukiwa naye faragha au kwa njia ya simu mwambie "Nakupenda sana XYZ,ninakuheshimu sana na ninahitaji tuishi pamoja mpaka mwisho wa uhai wangu pamoja na hivyo ninataka tuheshimiane,ikiwa haiwezekani kabisa kuheshimiana nitakuwa tayari tuachane muda wowote bila kujali muda ambao tumekuwa pamoja au uwekezaji ambao nimefanya kwako"
Sisitiza kwamba utamuheshimu na unataka HESHIMA tu, sisitiza kwamba unataka mawasiliano yenye ukweli na uwazi .Mwambie aongee moja kwa moja anataka nini siyo kuleta "Mind game" za kupima upendo kwa njia za ajabu ajabu.
Zingatia kwamba sifa ya mwanaume ni UONGOZI ndani ya familia siyo kutawala au kutawaliwa.
4.KUPIMA HASIRA NA MIPAKA YA MWANAUME
Mwanamke huwa anajaribu kupima hasira ya mwanaume kwa makusudi kabisa hasa kama mwanaume ni mpole sana, mnyenyekevu, muaminifu, mstaarabu sana,anapenda amani,hataki migogoro.
Ni hulka ya Mwanamke kumkera mwanaume kwa makusudi ili aone hasira ya mwanaume.
Anaweza kupuuza simu zako kwa makusudi, anaweza kukujibu vibaya, kutishia muachane, kuibua ugomvi mara kwa mara bila sababu,anaweza kuonyesha hasira kupitiliza bila sababu zozote za msingi,anaweza kununa nuna bila sababu hapa kosa kubwa ambalo wanaume hufanya ni kuanza kulia, kupiga magoti,kuomba msamaha,kumpa ushauri, kumbembeleza hapa utafanya apate kiburi na atakupanda kichwani.
Anaweza kumuomba mwanaume fedha nyingi sana lakini hataki pesa anataka aambiwe sina pesa , anaweza kuomba aondoke zake kwenda kwa marafiki au mashoga zake lakini hataki kuondoka anataka kusikia neno HAPANA,leo hautoki humu ndani ile sauti ya mamlaka ya mwanaume ndani ya familia huwa inampa furaha sana.
Ukiwa wale wanaume ambao wakiombwa fedha muda wowote wanatoa utamchosha na atakuchukia bila sababu -Epuka kuwa Bwanandiyo atakuona sio mwanaume
Ufumbuzi wake
Mwanamke akiwa na "mood swings" hizo ni hisia zake sio za kwako wala siyo jukumu la mwanaume kubadilisha kununa nuna kwake, kubadilisha "mood swings" hayo ni maumbile ya Mwanamke na ataendelea kuwa hivyo.
Ongea unataka nini sio unataka kuona anakuwa na furaha saa 24 haiwezekani.Hakuna mwanamke ambaye anaweza kuwa na furaha saa 24 hayupo duniani.
Mwambie makosa gani unaweza kusamehe na makosa gani hauwezi kusamehe hata iweje utafanya maamuzi magumu.
Mpe huduma na mahitaji kulingana na uwezo wako siyo vile watu wengine wanavyodai .Kama unaweza kumpa 5000 fanya hivyo atakuwa na maamuzi ya kuridhika au kutafuta mwenye hadhi yake.
Epuka kuhatarisha maisha yako ili kuzuia asije kukuacha utachemka.
5.KUPIMA KAMA MWANAUME ANAWEZA KUMPA CHANGAMOTO (Challenge test)
Hapa wanaume wengi huwa wanachanganyikiwa eti wanawake wanataka nini
Wanawake huwa wanaishi kwa kuongozwa na hisia zao yaani "mood swings" .Anaweza kukupenda dakika moja na kukuchukia dakika inayofuata hayo ni maumbile yao sio jukumu lako kumbadilisha.
Wanawake huwa hawapendi mwanaume mwenye sifa zifuatazo mstaarabu sana,mpole sana, mnyenyekevu sana, mvumilivu sana,mpenda amani muda wote,anayejali sana,anaejitoa mhanga muda wote,anayepokea simu saa 24,anaejibu sms saa 24, Bwanandiyo,anaesamehe kila kosa.
Hakikisha anakuona kama kiongozi sio bendera hufuata upepo.
Kila kitu fanya kwa kiasi,kuwa mpole baadhi ya nyakati na uwe unakemea utovu wa nidhamu,samehe baadhi ya makosa na baadhi ya makosa fanya maamuzi magumu hasa anapofanya kwa makusudi.
Binadamu anaishi kwa mazoea hivyo ukiwa mpole sana atakuona DHAIFU na vilevile ukiwa mkali sana utageuka mnyanyasaji
Fanya kwa kiasi .Kama Mwanamke anajua kwamba kosa lolote ambalo atafanya unasamehe atakuwa na KIBURI, DHARAU, MAJIVUNO na atakuwa anatishia kukuacha.
Akiwa mstaarabu ishi naye kwa upendo, amani na utulivu,usitafute ugomvi naye,mdekeze lakini akiona ni UDHAIFU badilika.
6.KUTAFUTA SABABU MUACHANE (Nuclear test)
Pale ambapo Mwanamke anataka muachane ataonyesha tabia zifuatazo
Anaweza kupuuza simu zako na sms hajibu, anajibu kwa mkato, anaibua ugomvi bila sababu zozote, anatoroka kwenda nyumbani kwao mara kwa mara,anaomba pesa nyingi sana kuliko uwezo wako ili ushindwe muachane, anaweza kufanya makosa kwa makusudi kabisa kisha anageuza kibao kwako,atakuwa na huzuni sana,hasira kupindukia na mara kwa mara anakufokea kukutukana, kukudhalilisha hadharani, kukuita majina ya aibu,hakupi unyumba, anaweza kutuma sms ya mapenzi kwa namba ngeni kisha anachukua simu yako na kukupa tuhuma za uongo za usaliti,atakuwa na manung'uniko, malalamiko,kukusema vibaya,kukuzudhia kesi ukweni,atakuwa anakukosoa kupita kiasi kwa kila kitu ambacho unasema au kufanya,atakulinganisha na wanaume wengine mara kwa mara,atatishia muachane mara kwa mara.
UFUMBUZI WAKE
Mwanamke akionyesha tabia hizo hataki umkumbushe wema ambao umefanya kwake,hataki risala, haitaji ushauri, haitaji vitisho,haitaji kubembelezwa bali anataka muachane tu aondoke zake.
Epuka kunyenyekea,epuka kumpa vitisho,epuka kuanza kulia,epuka kupiga magoti.
Tambua makosa ambayo unaweza kusamehe na makosa gani ambayo hauwezi kusamehe hata iweje,tambua nini unaweza kuvumilia na nini hauwezi kuvumilia kutoka kwake kisha mwambie akuheshimu ikiwa haiwezekani muachane kwa amani.
7.KUKAA KIMYA SANA BILA TAARIFA (Unexplained distance)
Hapa utaona simu hapokei, sms hajibu,kwa muda mrefu sana epuka kupiga simu mfululizo,epuka kutuma sms mfululizo.Akiwa kimya kaa kimya ilimradi umepiga simu haijapokelewa.
Epuka kulalamika,epuka kupaniki, epuka kumkumbusha wema wako,onyesha kwamba ukimya wake umekua fursa kwako ya kuboresha maisha yako bila yeye.
Kuwa busy sana,kama alikuwa anatafuta kisingizio muachane utakuwa umeokoa fedha zako na muda wako na kama alikuwa anakupima atakuja yeye mwenyewe na visingizio kibao.
8.KUVUNJA MAKUBALIANO GHAFLA (FLAKE TEST)
Tabia hii huwa inatokea pale ambapo umepanga kuonana na Mwanamke sehemu XYZ muda ABC kisha baada ya makubaliano anasubiri nusu saa kabla ya muda wa makubaliano anapiga simu au kutuma sms ya kutoa taarifa ya DHARURA au anazima simu haipatikani kabisa.
Kuna vitu 3 eneo hilo
a.Hana hisia zozote kwako lakini hajui namna ya kukataa
b.Anakujaribu ili kupima tabia yako
c.Ipo sababu ya msingi ambayo ni DHARURA
ufumbuzi wake
Epuka kupiga simu au kutuma sms mfululizo,epuka kupanga muda mwengine wa appointment badala yake acha yeye mwenyewe atakuja na maelezo yake na kama alikuwa anatafuta kisingizio muachane utakuwa umeokoa fedha zako na muda wako.