Mulokoz
New Member
- Jul 20, 2021
- 1
- 1
Naitwa Dickson Hynes natamani kusimulia safari yangu ya usomaji mpaka kufikia chuo kikuu.
Nimezaliwa Tanzania mkoa wa Kagera halmashauri ya wilaya ya Bukoba tarafa Bugabo kata Kaagya. Nimesomea Kaagya Shule ya msingi kipindi ambapo Shule za kata zilianza kufanya kazi mikoa yote Tanzania. Hatimaye 2010 nilijiunga Shule ya Sekondari ya Kaagya ambayo kipindi naanza walikuwepo walimu watatu na wawili wa kujitolea huku ikiwa imetoa wahitimu wa kidato cha nne kwa Mara ya Kwanza bila mwanafunzi wa kwenda kidato ya tano.
Baadhi ya vipindi vya Sayansi hatukuwa na walimu, tulienda hivyo hivyo tukiwa na ufaulu mbovu na mtihani wa kidato Cha pili tulifanya vibaya maana nilikuwa na wastani wa 47.5. Nilipo ingia Kidato cha tatu sikukata tamaa licha walimu walishakata tamaa muda. Mazingira ya usomaji hayakuwa rafiki na nyumbani hamna taa wala Sola na vibatari mafuta yako juu, watu wa maisha ya chini inabidi ubajeti kwa hiyo ikanilazimu niwe nasomea jikoni wakati napika. Muda nilioupata shuleni niliutumia kikamilifu.
Nilikuwa nikisoma mada za mbele kabla hatujafika huku nikiuliza walimu pia nikipitia karatasi za mitihani ya nyuma. Uzuri ni kwamba 2012 tulipokuwa Kidato cha tatu waliongeza walimu wanne nao ni Sanaa ilinibidi niachane na Fizikia maana hatukuwa na mwalimu hata mmoja, niliendelea na masomo nane huku nikusumbua walimu kweli kweli, iwe kuchota maji, kuchanja kuni nakadhalika nipo na karatasi zangu za pointi nikimeza maana elimu yetu mpaka Sasa ni kukariri.
Mungu ni mwema 2013 nikafanya mtihani wa Kidato Cha nne na kufaulu huku nikiwa mwanafunzi wa Kwanza kufaulu kwenda Kidato Cha tano tangu Shule ianzishwe 2006. Tangu hapo Kila mwaka wanafunzi wanakwenda Kidato cha Tano licha na walimu ni wengi kulinganisha na nyuma.
Mwendelezo ukawa nzuri nikaingia Shule ya Sekondari Nyakato na kuhitimu 2016 baadae chuo kikuu Cha Dar Es Salaam ambapo niliitimu 2019.
UJUMBE: MAISHA NI MAPAMBANO TUSIKATE TAMAA HATA KIDOGO MUNGU NDIYE AJUAYE KILA MTU LINI ATAPATA BARAKA. UNACHOKIAMINI ASIJE MTU AKAKUKATISHA TAMAA. TAIFA HILI LINAHITAJI WATU WENYE FIKRA PEVU ILI TUFIKIE UCHUMI WA KATI.
Kupitia changamoto nilizokumbana nazo, Kuna mambo mengi Serikali inatakiwa ifanye ili tufikie uchumi wa Kati. Maboresho yenyewe ni Kama ifuatavyo:
Marekebisho kwenye mitaala. Maboresho ya mitahala yapo katika maeneo manne ambayo serikali ningependa iyafanyie kazi nayo ni Shule za msingi, sekondari, vyuo vya ufundi na Vyuo vikuu.
Shule za msingi: Naiomba serikali na wizara husika warekebishe maeneo yafuatayo;
Tehama: Wizara inatakiwa iandae bajeti ya kununua Komputa za kutosha kwa ajili ya kusambaza mashuleni angalau Kila shule komputa moja ili Wanafunzi wafundishwe kwa vitendo kwenye kuwasha na kuzima, vifaa vinavyounda komputa, kuhariri, kufuta, kuhamisha na msingi wa Microsoft word. Faida mojawapo ni kwamba wanafunzi wawe na uelewa juu ya komputa na awe na uwezo wa kuandaa nyaraka za kawaida Kama Barua za kikazi, kirafiki na CV.
Ujasiriamali: Wanafunzi watengenezewe njia ya kujitegemea mapema tangu Shule za msingi.
Wawepo walimu wa idara zote michezo, sayansi, Sanaa, teknolojia ya habari, kilimo n.k.
Shule za Sekondari; Naomba serikali iboreshe pia Sekondari kwenye maeneo yafuatayo
Tehama: Naomba pia Serikali iwekeze kwenye tehama sekondari angalau komputa mbili kila shule ili wanafunzi wapate uelewa juu ya Microsoft word, Microsoft Excel, Microsoft office, power point presentation na matumizi ya intaneti kwenye kutafuta nyaraka mbalimbali. Hii itasaidia wanafunzi wanakwenda vyuoni na sehemu za kazi wakiwa na uelewa juu ya matumizi ya komputa.
Wanafunzi wafundishwe kwa vitendo sio tu kukaririshwa. Mfano pawepo na maktaba na mahabara za kisasa, wapelekwe gereji, na idara tofauti lengo akiingia chuo hasione kila kitu kigeni pia awe na uwezo wa kujiajiri pindi anapomaliza na kushindwa kuendelea vyuoni.
Pia wapewe elimu ya ujasiriamali kila hatua wanayopiga. Nitafurahi nikisikia somo la UCHUMI na TEHAMA yamekua ya lazima sekondari
Vyuoni: Natamani kuona maboresho yafuatayo:
Serikari kila mwaka waandae miradi kwenye bajeti zao ambayo itakuwa inatekelezwa na wanafunzi kutoka vyuo hivi, mfano ukarabati wa barabara za vumbi na Rami mijini na vijijini, usambazaji umeme vijijini, kufunga umeme kwenye majengo mapya ya serikali, viwanda, hoteli, godown, Shule nk. , Ukarabati wa majengo,kuhamua kesi, kutibu wagonjwa, kuunda magari, pikipiki, baiskeli na mengineyo. Wanafunzi waandae taarifa zao na zipimwe kupitia walichokifanya.
Pia maboresho ya vitendea kazi Kama mashine za kujifunzia ziletwe za kisasa, wanafunzi wafunzwe uundaji wa vyombo vya Moto, utengenezaji makopo ya kupaki bia mfano Castle Lite, Grand malt, Kilimanjaro, Castle rager, safari rager n.k. haiwezekani hata makopo Tanzania tunashindwa.
Kuwafunza wanafunzi juu ya njia sahihi za kilimo Kama Kuandaa hekari za kuzalisha kimea (ngano), ufugaji samaki, ulimaji katani n.k. hawezekani vitu vyetu vinakosa ubora
Tuwekeze mashine za kisasa kwenye kilimo na ulimaji wa kisasa. Tujikite kwenye utengenezaji wa bidhaa zenye ubora zinazoweza kushindana kwenye soko la kimataifa. Mfano tunazalisha sukari lakini viwandani inaagizwa kutoka nje, madini tunayo ila yanachakatuliwa nje ya Tanzania.
Tufunze walimu wenye weredi wa kufundisha kwa vitendo sio nadharia tu.
Elimu ya Watu wazima:
Zitengenezwe website za lugha ya Kiswahili kwa ajili ya kuweka taarifa mpya zinazojili Tanzania na duniani.
Vituo vya kufundisha watu wazima viongezeke ili kupunguza utapeli Kama kusainishwa mikataba feki, kunyanganywa aridhi, unyanyasaji wa kijinsia kwa sababu ya kutojua kusoma na kuandika.
Udhamini kusoma nje:
Nawaza Jambo moja nafikiri likifanyiwa kazi baada ya miaka 20 tutakuwa na hatua ya mbali. Serikali ijikite kuandaa vijana wa kuleta mabadiliko ndani ya taifa hili kwa kutoa udhami wa watoto wa miaka 4-6 jumla 500 wapelekwe Ulaya, Asia na Amerika ili waanze chekechea na watoto wa huko mpaka vyuo kikuu. Tulifanya hivi tutatengeneza wataalamu wa kila idala kwa ajili ya mageuzi ya viwanda ndani ya Taifa letu. Watoto hawa wapatikane kwa kufanyiwa usahili kutoka mikoa yote ya Tanzania.
HITIMISHO
Elimu endelevu ndani ya Tanzania itapelekea ukuaji wa uchumi zaidi ya hapa tulipo.
Asante sana.

Upvote
1