Jinsi ya kulinda taarifa zako ununuapo bidhaa mtandaoni

Jinsi ya kulinda taarifa zako ununuapo bidhaa mtandaoni

JamiiForums

JF Official Account
Joined
Nov 9, 2006
Posts
6,229
Reaction score
5,285
JINSI YA KULINDA TAARIFA ZAKO UNUNUAPO BIDHAA MTANDAONI

1646814372917.png

Chati hii inaonyesha kwa asilimia nchi zinazoongoza kwa ukuaji wa mauzo ya rejareja ya biashara mtandaoni, huku Ufilipino ikishika nafasi ya juu zaidi

Ukuaji wa Teknolojia ya mawasiliano nchini Tanzania, umechangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la manunuzi ya bidhaa mbali mbali mitandaoni. Watu wengi wakikimbilia kununua bidhaa mitandaoni kutokana na urahisi.

Ununuzi wa bidhaa mtandaoni unao faida na hasara zake.

Faida kubwa inayozungumzwa na wengi ni urahisi wa manunuzi ikiwemo kukwepa kupanga foleni kwa muda mrefu, watu wengi huchukizwa na kitendo cha kusubiri muda mrefu waendapo kufanya manunuzi mfano kwenye supermarket na hata masoko ya kawaida.

Manunuzi haya ya bidhaa mtandaoni yanazo hasara au changamoto zake pia, moja wapo ikiwa ni ulinzi dhaifu kwenye vifaa vinavyotumika kufanya manunuzi, hali inayopelekea watu kuibiwa fedha mara wafanyapo manunuzi mitandoni.

Ziko baadhi ya application ambazo humtaka mtu kuingiza taarifa zake binafsi pindi anapopakua, hali inayohatarisha usalama wa mtumiaji iwapo atapakua application yenye lengo la kumdhuru pasipo kujua.

Hatua zipi uchukue pindi unapotaka kufanya manunuzi kupitia simu au tarakishi yako
  • Chuja kwa umakini taarifa zako binafsi unazotumia ufanyapo manunuzi
  • Usitoe taarifa zako binafsi iwapo hazina ulazima wa kufanya hivyo
  • Hakikisha nywila yako inajulikana na wewe binafsi tu.
 
Back
Top Bottom