SoC01 Jinsi ya Kumuandaa mpakwa Mafuta/ anointed one kwa ajili ya Mali zako

SoC01 Jinsi ya Kumuandaa mpakwa Mafuta/ anointed one kwa ajili ya Mali zako

Stories of Change - 2021 Competition

MURUSI

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2013
Posts
4,537
Reaction score
8,824
Watanzania tumekuwa na Changamoto kubwa sana kwenye swala la kuandaa Msimamizi wa Mali/Biashara pindi Mungu anapo tuita.

İmekuwa ni kawaida kuona baadhi ya Biashara zikifa ndani ya mwezi au mwaka tangu Mwanzilishi kufariki na moja ya sababu kubwa ni kwamba hakukuwa na Maandalizi ya kuandaa Msimamizi wa Biashara.

İmekuwa ni kawaida baada ya Mazishi ndo Familia inakaa kikao kuchagua msimamizi wa Biashara au Miradi ya Marehemu, huyu anaye chaguliwa unakuta hana ABC za Biashara, hajui Marehemu alikuwa na Malengo gani na Project zake na mara nyingi huwa ni kama surprise kwake, na matokeo yake ni Project kuyumba na hatimaye kufutika kabisa miaka michache tu baada ya mwanzilishi kufariki.

Nini Tufanye sasa?

1. Anza kuandaa msimamizi wa Biashara kwa ajili ya wenzake;
Mpaka mafuta anapaswa kuandaliwa mapema mno wahenga husema Mkunje samaki angali mbichi, hivyo anza maandalizi mapema, andaa program ya kuandaa msimamizi mapema sana miongoni mwa watoto wako, usisubilia mpaka amekuwa mkubwa ndo umuandae.

2. Kufanya Uchaguzi wa Mpakwa mafuta. Hapa inahitajika utulivu sana na muda wa kutosha kwenye kuandaa mpakwa mafuta, kumbuka una kuwa na watoto wengi na unapaswa kuchagua mmoja tu, anaweza kuwa wasichana au wavulana na unahitahi kuchagua mmoja tu.

Unaweza waandaa watoto wote ila lazima awepo msimamizi mkuu.

Uchaguzi wa Mtoto atakaye kuwa Msimamizi mkuu:

- Andaa vigezo vyako vya ni nani hasa unataka awe msimamizi kwenye vigezo wapo wanao taka Mtoto wa kwanza, kuna wanao taka Binti wa kwanza, kuna wanao taka mtoto wa mwisho na kuna wanao taka mtoto anaye fanana nao kwa sura na kadhalila kwa kifupi kuwa na vigezo vya kutumia na usiongozwe na hisia.

- Washirikishe Watoto wote au familia na kila mmoja aeleze anapenda kuwa nani kwa baadae, wapo watakao taka kuwa Dakitari, Walimu, Marubani na hata Wafanya Biashara, thamini mawazo yao hapa, na hupaswi kuwaeleza unatafuta msimamizi.

- Mtoto mwenye mlengo wa biashara nadhani anza naye ingawa hata hao wengine unapaswa pia kuwaandaa kiana kwa sababu huwezi jua mbele ya safari ya kuandaa mrithi.

3. Elimu kwa Mpakwa mafuta
Mtoto utakae kuwa umemchagua ni vyema akasoma shule ya kutwa, usimpeleke Bording school kamwe, hii itasaidia kuwa naye karibu muda wote hivyo Bording school itakuwa sio mahali salama kwake.

Tafuta shule nzuri ya kutwa na asome huko.

Kwenye ratiba za shuleni lazima kuwe pia na ratiba za mambo nje ya shule, unaweza panga muda au siku ya kufanya haya ya nje ya shule.

4. Masomo yake; kwa sababu bado ni mdogo basi atakuwa anasoma masomo ya kawaida wanayo soma shuleni, İla kwa jitihada zako mtafutie vitabu vya Biashara vya kufundishia watoto na awe anasoma na pia awe anakupa mrejesho na utakuwa una mpa mtihani, tafuta hata vitabu vyenye katuni vya kufundishia ujasiriamali, vitasaidia saba kumjenga mpakwa mafuta.

5. Marafiki wa Mpakwa mafuta wako;
Hakikisha unajua marafiki wake, tabia zao zilivyo na ni watoto wa nani na je waba msaidia kijana wako? na hapa ile wazo la kusoma Day school linakuwa na maana, Mpakwa mafuta wako akiwa na marafiki wabaya wanaweza vuruga mipango yako yote, hakikisha unawajua na tabia zao uzijue fika, unapo ona rafiki zake hawaelekei kitabia basi mara moja mwambie aachane nao na unaweza pia kusaidia kumtafutia marafiki wazuri kitabia na wanao fanana malengo.

6. Kuwa naye sana karibu muda mwingi; anapo toka shule au siku za weekend hakikisha unakuwa naye karibu, story zako kwake ziwe na mwelekeo wa yale unayo taka afanye au asimamie.

7. Mtambulishe kwa marafiki zako wa Biashara;
Jitahidi sana kuwa unapo kuwa na meeting za kuonana na marafiki zako wa biashara basi nenda naye na mtambulishe kwao, na pia mweleze hawa wanafanya biashara zipi, hii itamjenga sana mpakwa mafuta wako na inampa sana confidence.

8. Muandalie ofisi ndogo ofisini kwako;
Kama office yako ni kubwa basi weka meza yake na siku ambazo hajaenda shule aje kukaa ofisini, kuwepo pale kutamjenga kwa sababu pia atakuwa anasikiliza maongezi yako na wateja au wadau wengine na hapa kujifunza hata rugha za biashara.

9. Nenda naye kwenye makongamano ya Biashara au semina za Biashara;
Kama kuna makongamano ya biashara nenda naye na kama ni ya kulipia basi mlipie na yeye awepo asikilize kinacho zungumzwa na sio kusikiliza bali na kuandika na atakuja kutoa mrejesho,

10. Anapo maliza shule kama ni kweda Chuo basi aende kusoma kile kinacho endana na atakacho kuja kufabya baadae,

11. Anza kumuachia baadhi ya majukumu awe anafanya, hii ni katika kumpima, Kama una Shamba Morogoro na unakaa Dar basi unaweza toa Gari na Dreva wa kumpeleka Morogoro na pale akaangalie shamba na arudishe report,

Hata baadhi ya mikutano unaweza kuwa ana mtuma yeye anaenda badala yako, unaweza mwambia unaumwa hata kama ukweli hauumwi, ila unakuwa unajua unacho fanya.

12. Anapo kuwa ameiva vya kutosha anza kujiondoa polepole kwenye majukumu na kumuachia yeye asimamie.

Muhimu; Kamwe usisubilie uko hoi kutandani ndo uanze kuandaa msimamizi wa mali za Familia itakuwa ni too laite sana, anza mapema sana kuandaa msimamizi atakaye beba maono yako kwa faida ya Familia yako.

Unaweza kuwa una watoto sita au saba lakini unaye muandaa sio mrithi bali ni msimamizi au kiongozi mkuukwa niaba ya wenzake.

Tujenge huu utamaduni, tuwe kama Wazungu, au wachina au Wahindi au Waarabu, angalia biashara zao zinanda kizazi kwa kizazi hii ni kwa sababu waliandaliwa.

Hakuna jambo baya umepambana na ulikuwa saa zi gine hulali ukitafuta mali ila unapo fariki ndani ya mwaka kila kitu kina sahaulika, alama yako inafutika kabida.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom