Wakati najifunza kuogelea ilikua nikiwa darasa la pili au la tatu!! tukafunga safari mpaka mtoni tukiwa group la watoto...hao mpaka kwenye mto!!
Sasa kufika pale naona wenzangu wanavua nguo na kurukia kwenye maji mimi niko nje tu nashangaa wakawa wananicheka, nikajikaza kiume nikavua nguo nikaruka ndani!! bila kujua nikaingia kwenye kina kirefu hahahaha yani najitahidi kunyoosha miguu ili nisimame nashangaa nazidi kuzama tu na ardhi siifikii duuh acha kabisa...wenzangu wako wananicheka tu mimi natapa tapa kujiokoa na kifo cha maji huku nikiwa nimebugia maji bila kupenda!!
Jamaa waka kuniokoa daaah nikatoka kwenye maji nikaa pemebeni nikiwa siamini kilichotokea!! basi wakaanza kunifundisha na mimi, nikaanza kwenye kina kifupi taratibu mpaka nikazoea, na mpaka leo hata maji yawe marefu kiasi gani siwezi zama!!!
Mleta mada nakushauri kama ni mara yako ya kwanza usiende nae unaweza enda kupata aibu ya kufungia mwaka...nenda mwenyewe kwanza kajifunze alafu ndio uende nae!!!
Maji hayataki mbwembwe mkuu!!