Jinsi ya kuokota pesa kirahisi

Joined
Jul 26, 2022
Posts
10
Reaction score
19
_________________________________

Pesa ya kuokota : Ni pesa ambayo haukulazimika kuifanyia kazi! Hapa kuna maeneo mazuri ya kutembelea ili upate hiyo bahati.


1. Tembelea Sehemu za Uoshaji magari: Watu wanaposafisha magari yao, sarafu zinaweza kuanguka. Wakati mwingine watu huzifagia pesa zao pamoja na takataka bila wao kujua .ukitembelea sehemu Kama hizo unaweza kuokota hela.

2. Angalia kwenye Vituo vya mabasi : kwenye Vituo vya mabasi watu huangusha chenji zao, Kama ujuavyo watu huwa bize Sana kwenye Vituo vya mabasi hivyo Kuna uwezekano wa kuangusha hela bila kujua. Ukiwa makini hizo hela zitakuwa Zako.

3. chunguza kwenye mifereji ya maji iliyo pembeni ya Barabara : Baadhi ya pesa huangukia kwenye mifereji ya maji hasa iliyopo karibu na Barabara. Hii hutokea pale watu wanapoingia na kutoka kwenye magari yao au watu wanapotembea, mfano mtu anataka kutoa funguo ya Gari mfukoni bahati mbaya anaangusha hela wakati wa kutoa mkomo mfukoni bila kujua. Mimi Nimeokota hela nyingi Sana kwenye mifereji ya maji.

4. Tembelea Viwanja vya michezo: Kuna watu hudondosha pesa uwanjani kwa sababu ya Vaibu la kushangilia mpira, Kuna uwezekano mkubwa mtu kuangusha pesa uwanjani bila yeye kujua. Hakikisha unatembelea haraka baada ya mechi kuisha na watu kutawanyika. Usichelewe usije kuta wenzako wameshaziokota

5. Chunguza Mtaani popote upitapo: Unapovuka barabara, tazama huku na huko huenda ukaona hela. Watu huangusha hela popote na muda wowote hasa ikiwa wana haraka Sana.

6. Tembelea Vituo vya treni : Angalia kwenye mashine za tiketi , chunguza chini mahali ambapo watu hununua tiketi. Wakati mwingine watu huangusha hela wakati wakiwahi kuingia kwenye treni hivyo hata wakiangusha hela hasahasa sarafu huwa hawajali kurudi kuiokota. Changamkia Fursa hiyo.

7. Chunguza kwenye Maegesho ya magari : Kuna watu wengi sana wanaoingia na kutoka nje ya magari yao katika maegesho ya magari hivyo uwezekano wa kupata hela zilizodondoshwa ni kubwa kuliko katika maeneo mengine mengi. Jenga tabia ya kutembelea kwenye Maegesho ya magari utakuja kunishukuru. Baadhi ya Maegesho ya magari kwa Hapa Coed Ni Kama Library, Mwarabu cafe, Mwafrika na Lecture rooms, pia unaweza kutembelea pale Benja yanapoegeshwa magari huwezi jua huenda Kuna hela imedondoka inakusubiri wewe tu.

8. Angalia kwenye viti (Bench) zilizopo katika maeneo ya kungojea Huduma fulani: Mabenchi katika maeneo ya umma ambapo watu huketi mara nyingi yanaweza kuwa na sarafu chache chini. Watu hukaa na sarafu huanguka kwenye mifuko yao mfano mtu anaweza kuangusha hela wakati anajaribu kutoa kitu kutoka kwenye begi lake.

9. Angalia kwenye Viti vya nyuma vya teksi au viti vya basi: Viangalie kila wakati. Pia ikiwa umekaa nyuma ya basi, angalia nyuma ya kiti. Ndugu mmoja wa rafiki yangu hufanya hivyo kila anapopanda basi, siku moja aliokota Tsh 10000 kwa sababu ya hiyo tabia aliyojijengea.

10. Chunguza Vyoo vya umma: Kuna watu huenda vyooni na hela na kwa sababu ya purukushani za shughuli za chooni huangusha pesa bila kujitambua, rafiki! Huenda unalalamika Sana huokoti hela Ila nikuulize Swali je umechunguza Mara ngapi kwenye Vyoo vya umma? Hebu Anza Sasa uone utakavopata bahati.

11. Kuwa makini Popote unapotembea: Ikiwa unapata nafasi kutembea eneo fulani, mtu mwingine ametembea huko kabla yako, kwa hivyo huenda ameangusha kitu. Daima angalia ardhini wakati unatembea.

12. Nenda Ufukweni: Ufukweni Kuna shughuli nyingi na watu ni wengi hivyo uwezekano wa watu kudondosha pesa Ni mkubwa. Nenda Ufukweni chunguza kwenye mchanga wa fukwe ikiwezekana beba sumaku Mana Baadhi ya Sarafu huangukia ardhini na kuzama kwenye mchanga wa fukwe, ukiwa na Sumaku utazivuta tu hizo Sarafu.

13. Chungulia Chini ya kitanda: ndo Mana Kuna methali inasema mtaka Cha uvunguni sharti ainame, hii Ni kwa sababu Kuna Baadhi ya hela zilishadondokea Chini ya uvungu, wahi kachungulie kitanda chako sahivi kabla wenzako hawajawahi.

Anyway: Tembea Zaidi upate pesa zaidi, mtembea Bure sio sawa na mkaa bure. Siku nyingine nitaandika kuhusu mbinu nyingine za kupata pesa.
 
Duh, kweli maisha yamekazaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚.

Huu uzi umejua kunifurahisha, nimejikuta nacheka peke yangu. Nikivuta picha mtoa mada anapiga mingo car wash au anapekua kwenye vungu za kitanda.

Muanzisha thread Mungu akubariki, umejua hasa kunichekesha.
 
Mara ya mwisho kuokota hela ilikuwa sikukuu ya idi mwaka jana.

Niliokota 2000 pale beach ya mji mwema.

Na mara ya mwisho kupoteza hela ni mwaka jana pia.
Nilienda tegeta wakati namsubiri malaya mmoja hivi ukapotea msimbazi kimiujiza.
 
Ni kweli ukiwa na tabia hizo utaokota pesa ila sio pesa za kutatua shida zako zako maana utaokota coin coin tu

Tulipokuwa wadogo kipindi Cha maonyesho ya sabasaba ilikuwa tukitembea mle ndani Sabasaba Kila siku mwenzetu mmoja alikuwa anaokota sana pesa ikabidi tumuulize mwenzetu anasili gani

Kumbe vile tunavyotembea tukiwa tunapiga story huyu mwenzetu kazi yake ni kuangalia chini tu ndio maana akawa anaokota coin coin
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…