Jinsi ya kuomba Leseni/Cheti cha Usajili wa Kiwanda kwenye mfumo wa BOS

BRELA

Govt Institution
Joined
Dec 14, 2023
Posts
119
Reaction score
89
Habari! na Karibu, Kupitia video hii leo nitakujuza jinsi ya kuomba Leseni/Cheti cha Usajili wa Kiwanda kwenye mfumo wa BOS.

Baada ya kuingia kwenye mfumo bofya sehemu iliyoandikwa Industrial Licence na ukurasa ukifunguka utabofya sehemu iliyoandikwa Apply New Licence/Certificate na baada ya hapo utaona huduma zote zinazotolewa katika moduli ya Leseni za Viwanda.

Ili kufanya maombi ya Leseniau Cheti cha Usajili wa Kiwanda, chagua mahali Kiwanda kilipo kama ni Tanzania MainLand au Zanzibar na kisha chagua sehemu iliyoandikwa Issuance of new certificate/licence.

Hatua inayofuata utahifadhi taarifa zako kwa kubofya sehemu iliyoandikwa Save&Proceed. Na hapo fomu itafunguka, utajaza ili kuendelea na mchakato wa maombi ya Leseni ya Kiwanda au Cheti cha Usajili wa Kiwanda.

Kumbuka Leseni ya Kiwanda au Cheti cha Usajili wa Kiwanda kinatolewa kwa wale waliosajili kampuni au Jina la Biashara.

Ni muhimu kuzingatia kuambatisha nyaraka zifuatazo unapoomba Leseni au Cheti cha Usajili wa Kiwanda:

Fomu ya majumuisho (Consolidated Form)
  • Mchanganuo wa mradi (Business Plan)
  • Nyaraka za Uthibitisho wa eneo la kiwanda kilipo (hati ya kiwanja au mkataba wa kupangisha eneo)
Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti: www.brela.go.tz

Au tupigie kwa simu namba +255 222 212 800


Your browser is not able to display this video.



​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…