Jinsi ya kuondoa au kupunguza mafuta tumboni kwa wanawake (Vitambi vya kike)

Mkuu umekusudia Mnyama yupi wa Taifa? Ng'ombe? Nyama ya Ng'ombe ina madhara bora ule nyama ya kuku kuliko kula nyama ya ng'ombe au Kitomoto nyama zote zina madhara ila nyama ya kuku ndio bora inafaa kuliwa wakati wote mkuu.

Kaka mbona unazunguka? KITIMOTO ndo hatari zaidi na ndio wataalamu wanavyosema! pia sio sahihi kusema kuku wapo poa? una maana gani maana kuku wa sasa wanafugwa kwa wiki 6 tu na wanakula madawa balaa nasikiwa watu wengine wanawapiga na ARV kidogo basi ananenepa hatari, kwa hiyo sidhani kama kuku hawa ndio uliowazungumzia!
 
Ongeza na asali limau na maji ya uvuguvugu utaona faida yake kubwa. PUNGUZA UNENE KWA ASALI NA LIMAU


​Unene wa mwili wa kupita kiasi (obesity) ni miongoni mwa matatizo ya kiafya yanayowasumbua watu wengi. Kuna njia nyingi za kufanya ili kupunguza unene, yakiwemo mazoezi ya viungo na kutumia baadhi ya vyakula kimpangilio.
Unene wa kupita kiasi ni hali inayomtokea mtu pale mafuta yanaporundikana kwenye ‘tishu' za mwili hivyo kusababisha matatizo kwenye moyo, figo, ini, viungio vya mwili kama vile magoti, n.k.

Halikadhalika, watu wenye matatizo ya uzito wa kupindukia huweza kupatwa na matatizo pia ya shinikizo la damu, kisukari, magonjwa ya msuli, ini na hata kibofu cha mkojo. Kwa ujumla unene siyo mzuri na ni chanzo cha maradhi mengi hatari. Kama unajali afya yako, unene ni wa kuogopwa kama ukoma.

Habari njema kuhusu tatizo hilo ni kwamba unaweza kujikinga nalo kwa kutumia asali na kama tayari unalo unaweza kulitibu au kulidhibiti kwa kutumia asali kwa kuchanganya na limau kwa utaratibu maalum.


Asali ni tiba nzuri ya kiasili ya kutibu tatizo la unene pamoja na shinikizo la damu, kwani hupunguza mafuta mabaya mwilini (bad cholesterol) kwa kuyageuza mafuta ya ziada kuwa nishati ya mwili. Mtu unaweza kufunga kula vitu vingine na badala yake ukatumia asali na limau tu kama tiba ya unene, bila kupoteza hamu yako ya kula au nguvu ya mwili.

JINSI YA KUTENGENEZA ASALI NA LIMAU

Kuna imani potofu kwa baadhi ya watu kuhusu limau na asali kuwa ni sumu. Ukweli ni kwamba mchanganyiko huu ambao ni wa ‘alkalaini' mwilini siyo sumu bali ni tiba kwa matatizo mengi ya kiafya, likiwemo tatizo la unene.

Ili kupata mchanganyiko sahihi, weka asali mbichi kwenye kijiko kimoja kidogo kwenye glasi yenye maji ya uvugu uvugu (siyo yaliyochemka), kisha weka vijiko viwili vya juisi ya limau (saizi ya kijiko cha chai) halafu koroga na unywe mchanganyiko huo.

Kunywa mchangayiko huo asubuhi kabla hujala kitu chochote au unaweza kunywa mchangayiko huo kila baada ya mlo mkubwa au ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi, mchanganyiko huo husaidia usagaji wa chakula na uondoaji wa sumu mwilini.

Katika kutekeleza mpango huu kwa lengo la kupunguza unene, usisahau kuzingatia suala la ulaji wa vyakula vyenye faida mwilini na vinavyoruhusiwa kiafya. Itakuwa ni kazi bure iwapo utatumia tiba ya asali huku ukiendelea na ulaji wa vyakula usiyokubalika kiafya. Halikadhalika mazoezi ya mara kwa mara ni suala muhimu kuzingatiwa.

COCKTAIL YA MATUNDA NA ASALI

Aidha, katika kuimarisha kinga na kuondoa sumu zaidi mwilini, unaweza kutengeneza mchanganyiko wa matunda mengi (fruit cocktail) pamoja na asali na kisha ukanywa. Kufanikisha hilo, chukua matunda kama vile epo, nanasi, zabibu, machungwa, karoti na mapera, yaandae vizuri kisha weka kwenye blenda na tengeneza juisi, bila kusahahu kuweka vijiko viwili vya asali mbichi. Tengeneza kiasi cha glasi moja na kunywa wakati ule ule kwa lengo la kupata vitamini zote bila kupotea.

Mwisho, ili kujiepusha na unene wa kupindukia, usipende kula kupita kiasi, hasa vyakula vyenye mafuta, ili hali hufanyi mazoezi wala hufanyi kazi yoyote ya shuruba. Unene ni dalili ya maradhi, jiepushe nao.
 
FAIDA YA TUNDA LA LIMAU


Limon
Limau: Tunda linalotumiwa kama kiungo. Lina umuhimu mkubwa kwa afya ya binadamu.

Limau lina manufaa chungu nzima kama vile kutuliza, kutibu, kupunguza sumu mwilini n.k.

Shinizo la Mawazo:
Huondoa uchovu wa akili, kisunzi, na pia wasiwasi. Limau lina uwezo wa kutuliza akili kwa kuondoa mawazo. Aidha unapumua harufu ya limau unaweza kujiongezea umakinifu.

Usingizi:
Utumiaji wa limau husaidia kumpa mtu usingizi na kuepusha tatizo la kupata usingizi.

Mfumo wa Kinga:
Limau lina kiwango kikubwa cha Vitamini kwa hivyo ni zuri kwa kuimarisha kinga mwilini, kwa kuzipa nguvu chembechembe nyeupe za damu, na kuimarisha mzunguko wa damu mwilini.

Homa:
Linaweza kutumika kuponya maradhi ya kuambukiza kama homa, malaria na homa ya matumbo.

Matatizo ya Tumbo:
Hutibu maradhi tofauti ya tumbo kama shida za usagaji chakula, , maumivu ya tumbo, na mshipa.

Kupunguza Uzani:
Hutumika na wengi kupunguza Uzani.

Pumu:
Inaaminika kwamba limau linasaidia kutibu pumu.

Nywele:
Aidha limau hutumiwa kwa utunzaji nywele. Limau huzifanya nywele kuwa na afya na za kuvutia, na huondoa uyabisi.

Ngozi:
Limau hutumiwa kutunza ngozi, kwa kuipa afya. Hutibu vidodosi na mba.

 
Thnx kwa kushare nasisi mambo mazuri mazuri.
Mimi hilo la kunywa maji ya uvuguvugu asubuhi sijaweza, nakunywa ya kawaida km gilasi 3 au 4 kabla sijbrush, jee hayafai au niendelee nayo hayohayo.
Then mm nina ulcer matunda mengi yananishinda, nlijaribu kupractice lkn nlishindwa, jee unanishauri nitumie nn mbadala.
Nashkuru nimeweza kupunguza vitu vya sukari na mafuta, nimelose kg km 5 hivi ndani ya mwaka m1.
Inataka moyo, kazi si ndogo.
 
Mkuu mimi Siwezi kutoa Ushauri mbaya eti niruhusu Watu watumie KITOMOTO nyama ya nguruwe la hasha wewe kama unakula hicho Kitomoto nyama ya Nguruwe shauri yako wewe na afya yako. KITOMOTO nyama ya nguruwe ina madhara makubwa kwenye afya ya binadamu si vizuri kukitumia.

Pole sana bibie kwa hayo maradhi ya vidonda vya tumbo kuhusu kunywa maji asubuhi ningelikushauri uwe unakunywa maji ya Uvuguvugu glasi moja yaliyochanganywa na asali kijiko kimoja kila siku asubuhi kabla ya kula kitu hiyo itakusaidia kuondosha mafuta mwilini mwako haswa kwenye figo na moyo. Pili kuhusu maradhi yako ya Vidonda vya tumbo jaribu kutumia dawa hii

Pata au weka vijiko viwili vikubwa unga wangano,vijiko viwili mafuta ya kupikia, nusu lita Maziwa Fresh ya Ng'ombe. Unga wa ulezi kidogo. pika uji vikombe vinne ikisha unywe kutwa mara 4 kwa muda wa mwezi moja Inshaallah kwa kudra ya Mola utapona. tumia dawa hiyo kisha unipe Feedback.
 

Mzizimkavu unaweza kutumia limao na asali katika hili
Lakini pia tuaangalie vyakula tunavyokula.
Asubuhi unaamkia wali na maharage unashushia na chai ya maziwa ..au viazi vitamu na chai
Mchana Ugali na Nyama
Usiku wali na maharage
Hapa kuna diet utafanyika :sleepy:
 
Ok, Inshaallah.
Thanx
 

Hapo kwenye red, vileo (bia, wine, etc) vimekatazwa.
Soma Waraka wa kwanza wa Petro, mlango wa 4, kuanzia mstari wa kwanza mpaka wa mstari wa tano ( 1 Petro 04:01-05) inasomeka kama ifuatavyo:-
"
1 Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni silaha ya nia ile ile; kwa maana yeye aliyeteswa katika mwili ameachana na dhambi.
2 Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani.
3 Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali;
4 mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika ufisadi ule ule usio na kiasi, wakiwatukana.
5 Nao watatoa hesabu kwake yeye aliye tayari kuwahukumu walio hai na waliokufa."
 


Kuna ulevi na unywaji?
 
Kuna ulevi na unywaji?

Vyote viwili (ulevi na unywaji vimekatazwa.
Angalia vizuri mstari wa tatu hapo kwenye red
"2 Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani.
3 Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali; .......
 

Well said,

Mchangiaji umenipa wazo zuri hivi nikipata baisikeli inaweza kuserve purpose eeh.... Ngoja nikainunue faster kwani itanisaidia kwenye mazoezi na kupunguza adha za mafuta/nauli za hapa na pale.
 
Mim nina uzito wa kg 82, wakati nina urefu wa cm 166 jaman naomben msaada wa kijipunguza nimechoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…