Wana JF,
Hili suala la mtu kutafuta ushauri wa jinsi ya kuondoa kitambi liliishaongelewa hapa kama sikosei miezi mitatu minne iliyopita. Kuna ushauri ulitolewa na jamaa yangu mmoja akaamua kuufuata kwa makini. Huwezi kuamini ndani ya siku 45 alibadilika kupita kiasi. Inawezekana nisiandike vile vile kama yule mshauri wa awali lakini huyu jamaa yangu alizingatia yafuatayo;
1. Awali alikuwa hali breakfast. Baada ya ushauri alianza kula breakfast.
2. Alikuwa anakula chakula kingi mchana na usiku. Alibadili na kuanza kula chakula kidogo mchana na usiku anakula chakula kidogo kabisa au siku nyingine hali.
3. Aliongeza kasi ya kunywa maji na kwa siku angalau alikuwa anakunywa lita 3 za maji
4. Alianza kwenye kwenye gym kila jioni ambako alipata nafasi ya ku-burn idle calories halafu kama nilivyosema hapo namba 3 akawa hali chakula kingi usiku.Kwenye gym machine alikuwa ana cover si chini ya kilomita 5 kila siku na alikuwa anakwenda kwenye gym 4 times a week.(He should spend at least 30 minutes in gym room exercising hard)
5. Alikuwa anaepuka kula vyakula vyenye jamii ya nyama usiku.
6. Alipunguza kasi ya kunywa bia.
This is a practical experience na nina imani huyo aliyeuliza akifuata haya maelekezo anaweza kufanikiwa kama jamaa yangu alivyofanikiwa.
Tiba