Jinsi ya kuondoa doa au madoa kwenye nguo

Jinsi ya kuondoa doa au madoa kwenye nguo

Jskinondo

Member
Joined
Jan 9, 2020
Posts
36
Reaction score
34
Habari za leo wana jamvi,

Kama kawaida natoa elimu ambayo ina manufaa kwa watu wote walio enda shule na ambao hawa kwenda shule kabisa.

Ninapotoa elimu hii sio kwamba mimi najua sana kuliko wengine ila naamini wapo watu wanajua vitu vingi kunizidi mimi lakini wengi wao ni wabinafsi (selfishness).

Kama kichwa kinavyo ongea "jinsi ya kutoa doa au madoa kwenye nguo". nimeona nitoe uzi huu baada ya kundua watu wengi hasa wanao penda kuvaa nguo nyeupe madoa kwao ni changamotokubwa.

Uzi huu utakuwa muarobaini kwa watu wote ambao ameathiriwa au wanaogopa kununua nguo za gharama sababu ya madoa.

Bila kupoteza mda niende kwenye mada tajwa, soma maelekezo ya fuatayo ili kutoa madoa kwenye nguo yako, ndugu au rafiki.

Vifaa
● Ndoo ya maji
● Beseni la kufulia
● Limao
● Sabuni

Hatua za kufuata kutoa doa:
1. Weka maji kwenye beseni (weka kiasi yanayo tosha kufua nguo moja)
2. Loweka nguo yenye doa kwenye beseni (hakikisha imelowana yote)
3. Kata vipande vya limao kulingana ukubwa wa doa au madoa ( kama ni doa moja kubwa vipande 3 vya limao vina tosha)
4. Sugua sehemu iliyo athirika na doa huku ukiminya limao ili maji ya limao yaingie penyewe.
5. Baada ya hapo chukua sabuni kisha ifue nguo yako kawaida (anza kuifua na maji yenye mchanganyiko wa limao)
6. Fuata hatua za kawada za kufua nguo iliyo chafuka.
7. Anika nguo yako kisha subiri hadi ikauke utanipa majibu, kama nguo yako ina doa usijaribu fanya kwa kujiamini.

Note: Hatu ya kusugua sehemu yenye doa isijirudie ikisha pita mwaga maji na kisha fua nguo yako kawaida.

God is good, stay home, stay safe protect from covid 19.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom