Jinsi ya Kuongeza thamani kwenye dagaa na furu

jangala22

Senior Member
Joined
May 20, 2021
Posts
165
Reaction score
141
Habari za majukumu wanafamilia wa JF
Naomba Kwa yoyote mwenye wazo la namna ya kufanya ili kuleta tija kwenye dagaa na furu wanaopatikana huku Kanda ya ziwa ikiwezekana tufanye kazi pamoja Mimi ninaishi huku mwanza na najishughulisha na uvuvi wa dagaa na furu changamoto ipo katika soko limekuwa la kusua sua hususani kwenye furu (n.b Kwa asiyefahamu furu wanakuwa wakubwa kidogo zaidi ya dagaa ila wanafanana na dagaa)
Vilevile kama Kuna mtu anaweza kuwa na connection na wenye viwanda vikubwa vinavyozalisha chakula Cha mifugo anaweza kufanya nao maongezi tunafanya kazi kuwakusanyia mzigo wa furu au dagaa.
Natanguliza shukran nakaribisha mawazo yenu wanafamilia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…