Jinsi ya kuosha mchele kwa ajili ya mapishi

Jinsi ya kuosha mchele kwa ajili ya mapishi

Bavaria

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2011
Posts
53,092
Reaction score
53,496
Mahitaji:
Mchele ambao tayari umeshatolewa uchafu.
Maji masafi ya baridi.

Process;
Chukua mchele wako uliochambuliwa weka kwenye chombo chako chenye maji masafi, maji yanatakiwa yazidi kidogo mchele ili uweze kuutoa mchele ambao ni safi.

Inamisha kidogo chombo chako kidogo halafu tikisa upandeupande ili kama kuna uchafu usioonekana ulale chini na mchele ukae juu.

Toa mchele wa juu kidogokidogo huku ukiwa unatikisa chombo chako. Mchele ukiwa unakaribia kuisha kwenye chombo chako kwa chini utaona uchafu umebaki.

Mwaga ule uchafu na mchele uhakikishe mchele uliosafi unakaushwa maji ili usivunjike vinjike.
 
Mkuu Bulldog hiko chombo kikiwa sufuria itapendeza zaidi sababu km kuna mawemawe ukiwa unachekecha/kutikisa utakua unayasikia yale mawe chini..
 
Last edited by a moderator:
Sikuhizi naona kwenye shughuli nyingi, eg. harusi, msiba mchele hauoshwi hii imekaaje wadau?
 
Sikuhizi naona kwenye shughuli nyingi, eg. harusi, msiba mchele hauoshwi hii imekaaje wadau?

Kweli kuna watu hawaoshi mchele wakipika ila mie naona si sawa kama haukuosha ile harufu kama vumbi itabaki kwenye wali
 
Kweli kuna watu hawaoshi mchele wakipika ila mie naona si sawa kama haukuosha ile harufu kama vumbi itabaki kwenye wali

Asante sana, watu wanadai eti ndio unakuwa mtamu nikawa nashangaa tu wacha tuendelee kuosha sie.
 
Sikuhizi naona kwenye shughuli nyingi, eg. harusi, msiba mchele hauoshwi hii imekaaje wadau?

Kweli kuna watu hawaoshi mchele wakipika ila mie naona si sawa kama haukuosha ile harufu kama vumbi itabaki kwenye wali

Asante farkhina.

Usipoosha mchele kuna vumbi na baadhi ya chembechembe zinabaki kwahyo zinaenda kujikusanya kwenye appendix.
 
Last edited by a moderator:
Hii ni jinsi ya kuosha au kupembua mchele? Umenikumbusha kuna rafki yangu aliwahi kuniambia akiwa anfanyia usaili mpishi wa chakula cha kiswahili test yake anapenda kuwapa kupembua mchele, anapima kilo mbili za mchele na robo kilo ya mchanga, anachanganya halafu anamwambia apembue na kusibaki punje ya mchanga!
 
Back
Top Bottom