Jinsi ya kupambana na rushwa

Jinsi ya kupambana na rushwa

Jagwanana

Senior Member
Joined
Jul 3, 2024
Posts
130
Reaction score
224
Rushwa.jpg

Tubadili mfumo wa kupambana na rushwa.

Katika jamii yetu, taasisi iliyokubwa kuliko taasisi zote ni taasisi ya rushwa.
Hata mtoto mdogo wa miaka 7 au nane anaweza kikuhadithia kwamba mzazi alipata tatizo hili au lile kwa sababu hakuwa na hela ya kuhonga asaidiwe hawezi kutatuliwa tatizo hili au lile kwa sababu hana uwezo wa kwenda kuhonga mtu au shirika.

1. Katika kupambana na rushwa tatizo ni serikali au taasisi kutumia mtindo wa juu kuteremka chini kwa mfano kukamata watu na kuwafunga ikithibitika amekula rushwa ni nzuri na taasisi hizi lazima ziwepo

2. Kuanzishwa taasisi rasmi zitakazosimamia utokomezaji wa rushwa kama TAKUKURU jeshi la polisi na mahakama katika kutatua tatizo la rushwa kisheria.

Yote hayo ni muhimu na yamekuwa na mchango mkubwa katika kutatua shida na adha ya rushwa katika jamii lakini wakati huohuo rushwa za aina aina na tiofauti tofauti zimekuwa zikishamiri na kufikia hatua ya kuiaminisha jamii kuwa uhalali ni pale mtu atakapotoa hongo ili utatuliwe shida yake.

Jamii imeaminishwa kuwa ukitoa hongo utapokea hudumu kwa haraka zaidi na kwa ufanisi zaidi hata kama maisha ya mtoaji hongo yako hatarini bado hongo ndicho kitakachokuokoa.

Mfumo mzima wa rushwa unamfanya mwananchi aishi katika maisha yanayozidi uwezo wake, kufedheheshwa kama ilivyo rushwa ya ngono au kudhalilika inapokuwa umepata matatizo au maafa kwa sababu tu umeshindwa kupata uwezo wa kuhonga.

Tatizo la rushwa linaifanya jamii kuingia katika madeni iwapo ana tatizo kubwa na kwamba bila ya kukopa ili ahonge hatapata msaada.

Kumekuweko na matabaka kwa sababu mtuanayekula rushwa huwa na maisha mazuri na kujijenga kiuchumi sana tofauti na tabaka la mtu wa kawaida anayefanya kazi kwa uaminifu na heshima lakini akistaafu ndiye anayeadhirika katika jamii.

Rushwa imekuwa ikikua kimitindo katika kasi ileile ambayo tunapambana kuitokomeza bila mafanikio yoyote.

SULUHISHO LILILO BORA
Ni lazima tatizo litatuliwe kuanzia chini kwenda juu ni pale tu tutakapoweka somo maalumu la kufundisha watoto wetu kuanzia ngazi za chini za darasa la kwanza hadi vyuo vikuu ambapo somo hilo liitwalo RUSHWA litajitegemea na kupewa kipaumbele kama yalivyo Hisabati, Jiografia, kiswahili , biologia au saikolojia.

Faida zake
Somo hilo litawafundishwa watoto wetu na ambao ndio taifa la kesho maarifa mengi juu ya wa sura, rangi, harufu au sauti ya rushwa na jinsi ya kuzishinda.
Kama ilivyo katika hisabati au biolojia au fizikia huwezi kuendelea mbele bila kulifaulu somo hilo la rushwa. Apewe F kama amefeli na A kama amefaulu. Huwezi kuwa injinia bila kufaulu hisabati na huwezi daktari bila kufaulu biologia au chemia. Usiwe kiongozi au kushika nafasi muhimu kama umefeli somo la RUSHWA.

Utaratibu huu ukitumika naamini iko siku rushwa itatokomezwa kama vyombo na taasisi zilizopo zitaendelea kuchangia kuandaa, kusaidia zaidi katika kutoa formal education na sio tu kukamata watu na kuwafunga pekee wakati hata hatumwandaa kielimu formaly kwamba rushwa ni kitu kibaya kimasomo akiwa mtoto mdogo, kijana na hata mtu mzima.
Serikali , mashirika ya ndani na nje yatakuwa muhimu katika kuwezesha somo la ruswa kuanzishwa kwa sanabu liwekwe katika mitaala na hivyo fedha kubwa zitahitajiwa katika kusomesha waalimu, kuanzisha mtaala wenyewe na katika mambo yote yatakayowezesha somo kuanzishwa na kufundishwa kama masomo mengine yalivyo.

Tukiwafundisha watoto wetu kuanzia utotoni hadi ukubwani basi mtu ataona aibu na kujisikia uchungu na kuona haki ya kujiadhibisha kabla hajaadhibiwa kwa sababu alifundishwa.

Dalili kubwa ya kutambua rushwa inaanza kutokomezwa ni pale mwombaji au mtoaji rushwa ataona aibu kutenda jambo hilo na atadharaulika katika jamii kama mla rushwa au mtoa rushwa.
Sasa hivi wala rushwa ndio wenye nguvu na heshima katika jamii zetu ikimaanisha kutenda mabaya kumbe kuna manufaa zaidi na hiyo inamsababisha mtu kuona nae lazima atende hivyo punde akiarjiriwa au kupewa nafasi muhimu.

TUANZISHE SOMO LA RUSHWA KATIKA MITAALA YA SHULE ZOTE NA VYUO VYOTE NCHINI.

Hata kama itaigharimu nchi gharama gani, awamu kwa awamu na tufanye hivyo na rushwa itatokomezwa. Hakuna njia nyingine na tumechelewa sana ila inawezekana kufaulu katika hili hata kama tumechelewa.

Dar es salaam,
Tanzania
 
Back
Top Bottom