Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532

Urembo na Mapambo
- Bangili, hereni na mikufu unayoitumia mara kwa mara vinafaa vitundikwe kwenye stand maalumu mahali panapofikika kiurahisi mfano juu ya dressing table ili iwe rahisi kuvichukua na kutumia kila unapohitaji na kuzuia visishikane na hatimaye kuharibika.
- Vito vya thamani viwekwe mahali salama kwenye container au box dogo zikizungushiwa kitambaa laini au sponji ili kuhifadhi thamani na mng’ao wake.
- Hifadhi vitu vya aina moja pamoja, mfano dhahabu, silva, plastic, shanga, n.k ili iwe rahisi kujua kitu fulani kipo wapi kinapojitajika.
- Hakikisha mikufu yote imefungwa vyema kuepuka kushikana na hatimaye kukatika.
- Viatu unavyovivaa mara kwa mara viweke kwenye ‘shoe rack’ mahali ambapo ni rahisi kuonekana kama ni kwenye korido au sehemu yoyote rahisi kufikika.
- Vipange viatu vyako kwenye shoe rack kufuatana na rangi, urefu wa kisigino, aina ya kiatu au matumizi.
- Hakikisha viatu vyako ni vikavu na safi kabla ya kivihifadhi na hifadhi sehemu kavu isiyo na maji au unyevu.
- Viatu ambavyo havivaliwi mara kwa mara kama vile vya kuvaa kwenye matukio maalinu ya usiku ni vyema vikihifadhiwa kwenye sehemu ya chini ya kabati.
- Kama viatu, pochi pia zinapendeza na pia kukusaidia kuokoa muda zikihifadhiwa kwa ukubwa, rangi, aina au matumizi.
- Pochi unazotumia mara kwa mara weka kwenye stand maalumu na nyingine unaweza weka kabatini ili kupunguza wingi wa vitu kutundikwa kila mahali.
- Pochi ndogo na wallet ziwekwe pamoja ndani ya droo au pochi kubwa ili kuepuka kupotelea ndani ya nguo au pochi nyingine.