Jinsi ya kupanga uzazi kwa kutumia njia ya asili ya kalenda

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2012
Posts
2,968
Reaction score
8,139
Mara nyingi nimekuwa nikiona threads humu ndani watu wakiulizia unawezaje kuhesabu siku na kujua zile siku za hatari ambazo mwanamke anaweza kushika mimba; naomba leo nitoe somo kidogo.
Kwanza,napenda tufahamu yafuatayo.

1. Ili njia hii iweze kuwa effective ni muhimu kwa mwanamke akawa na mzunguko ambao haubadiliki badiliki(regular menstrual cycle).

2. Njia hii ni less effective kwa wasichana walio chini ya miaka 25 na ambao bado hawajawahi kushika ujauzito kwa sababu wanawake hawa mara nyingi wanakuwa na very irregular menstrual cycles(mizunguko yao ya hedhi inabadilika badilika sana).

Sasa tuanze somo;kwa wanawake wenye mzunguko wa siku 28,siku ya kupevuka kwa yai ni siku ya 14,na yai baada ya kupevuka lina uwezo wa kuwa hai kwa wastani wa masaa 72;pia mbegu za kiume zinakuwa hai kwa wastani wa masaa 48-72. Lakini pia,yai linaweza kupevuka siku mbili kabla au baada(yaani siku ya 12-16). Kwa mahesabu hayo basi, siku za hatari ni kuanzia siku ya 9 mpaka ya 19;ndani ya siku hizi hutakiwi kufanya mapenzi bila kinga kama hutaki kushika mimba. So either usifanye mapenzi katika siku hizi au utumie kinga.

Kwa wale wanawake ambao mzunguko wao si wa siku 28,wao siku ya kupevuka yai wahesabu kwa kuchukua jumla ya siku za mzunguko wao kutoa 14(mfano kama mzunguko wako ni siku 32;chukua 32-14=18,kwa hiyo siku ya 18 ndo siku ya yai kupevuka).

Njia hii inawafaa zaidi wale wanawake ambao huwa wanajua siku ambazo mayai yanapevuka kwa sababu huwa wanapata maumivu kidogo ya upande wa kulia/kushoto wa tumbo('ovulatory pain'-si wanawake wote wanapata hii hali).

Ahsanteni sana. Nakaribisha maswali.
 
Asante kwa soma Dr W.


Kwenye sikio na asikie
Mwenye macho aone.
 
kwa hiyo Dr. ukiacha hizo suku ulizosema ni za hatari siku zilizobaki ni za kuchapatua tuu
 
Swali; kama nataka kupata mimba nizae mtoto wa kiume nafwataje tarehe?
 
Swali; kama nataka kupata mimba nizae mtoto wa kiume nafwataje tarehe?
njia inayotumika katika timing ya gender inaitwa 'Shettles method' iliyoasisiwa miaka ya 1960s' ambayo inatumia the fact kuwa Y sperms(ambazo ndo za kiume) zina speed kubwa kuliko x sperms(za kike); kwa hiyo kama unataka mtoto wa kiume unakutana na mwenzi wako siku ya yai kupevuka(au siku moja kabla),kwa hiyo y sperms kwa sababu ziko faster zitalifikia yai mapema na kufanya fertilization.

Kama unataka mtoto wa kike,unakutana na mwenzi wako siku moja au mbili baada ya yai kupevuka,kwa hiyo y sperms zitakuwa zimeshajifia, na x sperms ndo zitarutubisha yai na kupatikana mtoto wa kike.
Hata hivyo, research za hivi karibuni zimeonyesha kuwa hakuna tofauti kubwa kati ya x na y sperms, kwa hiyo njia hii uhakika wake ni mdogo.
 
Hii njia chai sana hii, inaweza kukuingiza mkenge hivi hivi? Siku hatarishi ndio hunoga zaidi, sasa ya nini usizuie?
 
Hii njia chai sana hii, inaweza kukuingiza mkenge hivi hivi? Siku hatarishi ndio hunoga zaidi, sasa ya nini usizuie?
ni kweli hii njia inataka mtu uwe na discipline hasa, kwa sababu ni kweli kuwa hizo siku za hatari ndo unakuwa na mihemko kupita siku zote; hivyo ni muhimu uwe na self discipline.
 
Naomba kuuliza swali ndugu mleta somo: kama miezi kadhaa huko nyuma mwanamke alikuwa anapata siku zake kila tar.30 ya mwezi lakini mara yamwisho tarehe ikachange kwa kuongezeka siku 6 mbele ndo akapata siku zake. Je?, anawezaje kudetermine siku zake kwa mwezi unaofuata?
 
What is the point ya kupika chakula nikipendacho afu nisile?

ni kweli hii njia inataka mtu uwe na discipline hasa, kwa sababu ni kweli kuwa hizo siku za hatari ndo unakuwa na mihemko kupita siku zote; hivyo ni muhimu uwe na self discipline.
 
beyond human capacity.....................
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…