Jinsi ya kupangalia chumba cha kulala kiwe na mvuto zaidi

SAWEBOY

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2011
Posts
241
Reaction score
174
Wakuu wana JF,

Poleni kwa majuku ya kila siku.

Naombeni ushauri wenu, nimehamia hapa DSM na kuanza maisha, takribani week imepita. Nilijibanza kwa ndugu sasa nimepata vyumba 2 ambavyo ndo nategemea kuingia.

Pamoja na maandalizi mengine muhimu niliyoyafanya (vitu basic )bado kuna kitu kimoja kinanisumbua: Jinsi ambavyo chumba (sebule ) nitakavyo-ipamba ili mpenzi wangu akija kunitembelea anione nipo juu kiasi -ku-maintain status!

Naombeni ushauri wenu watu wataalam wa kupamba room au sitting room.

Vitu gani hasa ni muhimu vya kupendezesha?

Natanguliza shukrani wapendwa.
=========

Unapaswa kujua jinsi ya kuweka kitanda ndani ya chumba cha kulala vizuri, kwa kuwa hii itaamua jinsi mpango utakavyogeuka na kama chumba kitakuwa na usawa.

Ni muhimu kuzingatia vipengele vya chumba na ushauri wa muhimu, ambao utakuwa rahisi kufanya uchaguzi sahihi. Pia unatakiwa kuwa na mweza ya pembeni ya kitanda.

Hizi ni dondoo chache za namna unavyoweza kupanga meza yako ya pembeni mwa kitanda, na kufanya chumba chako kivutie;

  • Tambua mtindo unaotaka kutumia kupamba meza yako ya pembeni; ukifahamu mtindo wako, itakusaidia kubuni ni muonekano wa namna gani unataka uwepo katika meza yako.
  • Ng’arisha kwa kuweka taa ya mezani; taa ya mezani ni moja yap ambo zuri la kuweka katika meza yako pembeni ya kitanda. Taa hiyo ina kazi nyingi mbali ya kupamba, lakini kama una tabia ya kuamka usiku, itakusaidia kukuangazia ili usije kujikwaa na kuanguka kwa kutoona.
  • Pamiliki kwa kuweka picha: uwekaji wa picha ni moja ya njia ya kupafanya paonekane ni sehemu yako binafsi. Unaweza kuweka picha zinazokukumbusha mambo mazuri ya familia. Unaweza pia kubadilisha na kuweka picha sanaa nzuri.
  • Weka trei ndogo: kwa ajili ya kuweka vitu vidogo vidogo pembeni ya kitanda chako. Trei ndogo ni timilifu kwa kutumia kupangia vitu kwenye meza ya pembeni mwa kitanda, ili kuepuka vitu kusambaa samba. Unaweza kuweka vitu vidogo vidogo kama herini, sarafu au vitu vingine vidogo.
  • Unaweza kuongeza nakshi kwa kuweka mmea pembeni ya kitanda kuongeza rangi; Kuweka mimea kwenye eneo lolote nyumbani huongeza uhai. Mimea kama ilivyo kwa taa ya mezani huongeza rangi na mvuto kwa muonekano mzima wa chumba. Kama wewe ni mtu usioweza kutunza mimea hai, basi weka mimea feki na hasa yakiwa ni maua.
  • Weka vipambo vidogo vizuri vya thamani; mapambo kama sanamu ndogo au saa vinaweza kufaa.


Michango ya wadau

----
----
----
----
 
Ku maintain status hakikisha upende kununua vitu quality, usijaze vitu vingi halafu vibovu... Basics za muhimu sebuleni kwa kijana wa kisasa ni Carpet, Sofa seats, TV & Deck, Pazia, Coffee table, Theatre system (si lazima but ni muhimu kwa entertainment) na Meza kwa ajili ya TV.

Hakikisha unaponunua/andaa vitu vi blend; blend in the sense kua unapokua/nunua vitu hivyo vya electronics hakikisha vinaendana rangi Vizuri, then unaangalia rangi ya ukuta wa hio sebule, unanunua pazia quality nzuri na rangi zilizopoa na za kiume kama coffee, beige, grey (kwa ufupi colours dark - usidhubutu sujui pink, yellow n.k). Mara nyingi coffe table nzuri za kisasa ni zile za kioo zenye stool zake, na hizi siku hizi zimeshuka sana bei sana i believe ukijipanga u can afford - miguu ya coffee table rangi ifanane na ya meza ya Tv.

Carpet nunua mwishoni, cause ni a guy mara nyingi nyie nafasi ya usafi ni finyu, nakushari dark colours; inaweza kua ya maua au michoro yenye rangi zote kama za pazia, sofa, meza n.k - ikiwa rangi moja walau iendane na pazia.. Carpet ikiwa dark colour itakusaidia coz ni nyumba ya vyumba viwili inamana lazima utapita sana hapo.

Kuepusha kuweka vitu kama glasses, sahani, jugs sehemu yoyote ya sebule ni vizuri ukachonga kimeza kidogo cha kuweka kona moja (hakikisha mgeni wako akiketi anakipa mgongo au ubavu) - hapo waweza funika na vitamba (zipo plastics but zinaonekana kama kitambaa) special kwa meza na water resistant. Hicho kitambaa cha plastic cha meza kiwe kinaendana walau na pazia. Hio meza waweza tumia kwa ajili ya kuweka all vyombo related things...

Good luk katika maandalizi... La ziada hizi mvua sisikudanganye fan muhimu.....
 

Dada Asha,

Nakushukuru sana kwa mchango wako, maana umenipa mambo matamu sana na naamini nitakapo yafanyia kazi basi dah room sebule yangu itapendeza sana.

Once again, nakushukuru sana kwa mchango wako juu ya hili jambo.
 
Subiri mahitaji..

Mkuu,

Ni mahitaji gani tena ? Si ndio nakusubiri wewe unihabarishe vema kuwa ninunue nini na madowido gani ili ni-ipendezeshe sebule , na hata chumba cha kulala !

Nakusubiri mpendwa kwa ajili ya ushauri wako ili mwenzio nisije chekwa akija kunitembelea nanihiiii!
 
Wakuu wana JF,

Poleni kwa majuku ya kila siku.

Naombeni ushauri wenu, nimehamia hapa DSM na kuanza maisha, takribani week imepita. Nilijibanza kwa ndugu sasa nimepata vyumba 2 ambavyo ndo nategemea kuingia.

Natanguliza shukrani wapendwa.

A yu sirias asee, kwanini usimsubiri huyo mpenzi wako mkapanga pamoja jinsi ya kupendezesha sebure yako?
 
Dada Asha,

Nakushukuru sana kwa mchango wako, maana umenipa mambo matamu sana na naamini nitakapo yafanyia kazi basi dah room sebule yangu itapendeza sana.

Once again, nakushukuru sana kwa mchango wako juu ya hili jambo.


Any time...
 

Nyie vijana wa siku hizi mna mambo kwelikweli. Utapamba nyumba weeeeeeee lakini mkifika kwenye 6x6 mnaanza kujitetea ooohhh ofisini ubusy ooohh najiskia malaria, ooh nimepata habari mbaya, ohh sijui nini vile!

Hayo unayotaka kufanya huenda rafiki yako yamemchosha machoni kwake. Kikubwa anachotaka kwako ni uanamume wako au usichana wako, full stop.

Mkitoka hapo ndipo mambo mengine yatafuata tena uzuri wake ni kwamba mkifanikisha yote hayo, hata ukipamba chumba chako hovyo, kitaonekana kizuri tu.
 

Kutoka kuwa jukwaa la watu makini na great thinkers hadi washauri wa wahamiaji na madalali !!!tunapotea taratibu!!
 
Reactions: Iza
Kama unataka kumfurahisha huyo mpenzi wako kweli muombe yeye akusaidie kupanga!!!
 
Huko chumbani usinunue kitanda kikuuubwa hadi mkose nafasi ya kupita. Nunua size ya kutosha ili chumba kiwe na hewa. Pia sio lazima ununue seti nzima ya makochi utajaza seble. Nunua kochi moja tu lenye 3 or 2 seats.
 
LENGO NI KUMFURAHISHA MCHUMBA WAKO! ILI NICHANGIE NAHITAJI DONDOO ZIFUATAZO tueleze ni wawapi (MJINI KIJIJINI, USWAHILINI, UZUNGUNI, MSOMI AU) ili uendane nae!
 
Uko tayari kulipia ushauri/kwaajili ya kazi hiyo?Na kama ni bure,basi ninaomba tukae chini na huyo mpenzi wako ili kujua nini angependelea paweje hapo maskani ili kuweza kumfurahisha.
 
LENGO NI KUMFURAHISHA MCHUMBA WAKO! ILI NICHANGIE NAHITAJI DONDOO ZIFUATAZO tueleze ni wawapi (MJINI KIJIJINI, USWAHILINI, UZUNGUNI, MSOMI AU) ili uendane nae!

Aaaah! Elia.
 

Wewe utakachokihitaji kwa wakati huo ndo utanunua ukitaka dressing table ukaona hakuna ndo ununue, ukitaka kioo hakuna ndo ukanunue, ukitaka kuangalia TV huna nenda dukani, ukiona unakanyaga chini kuna baridi nenda kanunue carpet, ukitaka kupika kuwasha mkaa au jiko la mchina unaona shida kanunue jiko la gesi upate urahisi na ukiaka chochote kwa wakati wowote ndo uende ukanunue kwa muda huo....sijui umenipata???
 

Ha ha ha umenichekesha sana hapo kwenye bold
 
Duh! status doesnt mean anything mheshimiwa! jenga maisha bwana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…