Jinsi ya Kupata Masoko kwa ajili ya bidhaa zitokanazo na kuku

Jinsi ya Kupata Masoko kwa ajili ya bidhaa zitokanazo na kuku

mbota

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
1,054
Reaction score
585
Wanabodi ni matumaini yangu kuwa mnaendele vizuri na kumalizia weekend.
Niende moja kwa moja kwenye point, Vijana wengi tumekuwa wajasiria mali hasa kwenye ufugaji wa kuku,lakini changamoto kubwa tunayokutana nayo ni jinsi ya kupata masoko ya bidhaa zetu yaani Mayai, Kuku kwa ajili ya nyama, kienyeji na chotara.

Changamoto hii mara nyingi imesababishwa na ukosefu wa taarifa sahihi kwa wakati sahihi kwahiyo ili kuondokana na hii changamoto ni vizuri kuwa na kitu kitakacho tuunganisha wafugaji wote wa kuku ambao tunapatikana Tanzania nzima ambapo tutakuwa tunapata taarifa kwa wakati sahihi.

Mimi siyo mtaalamu wa sayansi ya computa lakini nashauri tuwe na App itakayowakutanisha wauzaji na wanunuaji. Hivi kuna chama cha wafugaji wa kuku Tanzania?

Karibuni tushauriane ni kwa jinsi gani tufanikishe kufanikiwa kwenye masoko ya kuku hapa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla
 
Ni wazo zuri kuwa na platform kama hiyo, kwa maana mnunuzi na muuzaji mnakutana hapo.
Itakuwa slow kwakuwa jamii imezoea hii ordinary system ya kutafuta masoko kwa kuwafuata wanunuzi au kusubiri eakufate. App au website ni nzuri (online marketing)
 
Kwanini jukwaa hili hapa jamiiForums lisitumika kwa hilo wazo lako?
 
Wazo Nzuri sana ila, wafugaji wengi bado hawana uelewa na biashara ya mtandao, wachache sana wamejiunga na WhatsApp ao Jamiiforum.
 
Mimi Nina shamba Arusha LA kuku wa kienyeji.Nauza jogoo wenye kilo kuanzia 2
 
Bei za mayai ya kisasa. Huko uliko Tshs ngapi kwa rejareja na jumla ?
 
Mkuu uko Arusha sehemu gani? Unauza bei gani?
Kama unauhitaji mimi pia niko nao wakienyeji pure pamoja na mayai mimi kuku nauza kuanzia 15,000-20,000 niko arusha maeneo ya kijenge my contact 0784320071 you can even whatsup me.
 
Back
Top Bottom