Jinsi ya kupata mtaji mkubwa kwa mwanachuo

Kigorohe

Senior Member
Joined
May 21, 2019
Posts
160
Reaction score
255
Habari wana jf. Nipende kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kuendelea kutupa uzima na kuyasongesha maisha.

Natambua kuwa mpaka wakati huu kuna mtu anaumia sana kwa sababu alivyopangilia mipango yake pindi anaingia chuoni sivyo inavyoenda sasa hivi. Kuna watu walikuwa na malengo mazuri sana ya kukusanya mtaji kutoka katika pesa ya mkopo (boom) lkn wengi wao wamefeli kufanya hivyo kutokana kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusiana pesa hiyo. Nadhani leo lazima ufunguke akili kwa uzi wangu.

Ndugu mwanachuo mwenzangu, kulingana na uhaba wa ajira tumeamua sisi kama wasomi kutafuta njia mbadala ya kujiajiri kwani tunasoma elimu ili tuweze kupata utashi wa kuyatawala mazingira yetu. Hivyo ni vyema tuwe na wazo la kutengeneza mtaji wetu sisi wenyewe. Ukiwa una mtaji wako kila kitu kitaenda sawa.

Sasa bila kupoteza muda twende kwenye somo letu. Sasa kitu cha kwanza kufanya ni kutambua wewe upo mwaka wa ngapi? Mfano kwa mwaka pili umebakiza maboom 5 lkn mwaka wa kwanza kabakiza maboon 9. Ukisha tambua hilo nenda benki yeyote fungua account ya tsh50,000 kama hela kianzia cha account. Account hizi znatofautiana majina kulingana na benki yenyewe. Ukisha fungua em jinyime kila boom angalau uweke kwenye account yako tsh150,000 au zaidi. Mfano kwa mwaka wa baada ya maboom matano utakuwa na 750,000 na kwa mwaka wa kwanza baada ya maboom 9 utakuwa na tsh 1,350,000. Jamani hii ndiyo njia rahisi na sahihi ya kukufanya wewe upate mtaji hata kama hufanyi biashara pindi upo chuoni.
Pia una ruhusiwa kushare wazo lako na wewe.

Asanteen sanass
 
Kila la kheri kwenu, kipindi chetu tulikua tunapewa elfu 5, sikuweza kusave zaidi nilimaliza na deni la elfu 40
 
hela ya Boom haikai.. otherwise uwe unapewa hela na wazaz.. ila kama unategemea boom uje ujengee na usomeshe ndugu,ule.. ulipe kodi uvae.. ukiumwa utibiwe.. ktk boom.. halikufikishi popote

labda kwa mtu ambaye anapewa hela kutoka kwa mtu mwingine ikiwemo mzaz.. hapo hiyo plan itafanikiwa.
 
Ushauri wangu musiwe waoga wa maisha kiasi cha kutaka kujifanya baili ili uwe na mtaji mkubwa utapokuja kitaa.. Kuna fikra moja ipo kichwani mwa watu hili la mtaji mkubwa ndio ufanye. ni uwongo Kuna watu ambao leo hii wamepiga hatua kubwa mtaji wao ulikuwa ni nguvu tu.... Na wamepata kidogo then wanapiga hatua nyengine mbele mpaka mtaji ukawa mkubwa kwaiyo unaweza kuanza na mtaji hata chini ya laki moja cha msingi ni Nia yako tu ukiwa na shiling elfu tano ukiwa na malengo nataka niikuze basi inakuwa na pesa inakuwa kubwa... kinacho wa shinda wengi ni uvumilivu na wengi wenu mkija mtaani mnataka maisha ya fasta fasta mkiona wenzenu mliowaacha kitaa wapo hatua fulani.. Jitahid Sana usipaniki maisha ukituliza akili unatoboa kumshinda yule aliye Anza na mtaji mkubwa.. Unaweza ukaanza biashara huko chuo hata ndogo ili ukuze mtaji.. Note 😛atience, persistence and perspiration make an unbeatable combination for success
 
Kama vipi kijana mwenzangu fuga nguvu tu angalizo ukija huku ficha vyeti vyako jitoe ufahamu usiogope kuchekwa jichanganye.. Achana na tabia ya kuzarau kazi ukiona unaimudu piga bora iwe na maslahi tu.. Note :usipoteze marafiki wa mtaani uliowaacha ya kwamba ww msomi basi utapata wengine huko ulipo wa kitaa wanaweza wakakushika mkono au wakakusaidia kwa lolote lile hili jambo kaeni mlijue marafiki wa mtaani msiwadharau wala msiwapoteze maisha hayana formula kusoma siyo kufanikiwa na kupata pesa nyingi
 
Mchango wako wa darasa la saba ni mzito sana ndugu.
Waliofika chuo huwa wanafeli maisha kwa kutolijua Hilo.
Hufikiri kwamba akiwa na makaratasi ya vyeti Basi ndio kamaliza mafanikio yatakuja yenyewe.
 
Mchango wako wa darasa la saba ni mzito sana ndugu.
Waliofika chuo huwa wanafeli maisha kwa kutolijua Hilo.
Hufikiri kwamba akiwa na makaratasi ya vyeti Basi ndio kamaliza mafanikio yatakuja yenyewe.
Asante mkuu
 
Mimi mbona boom halijawahi nitosha? Na sikuwa nakunywa pombe, sikuwa naenda club,, sikuwa nasuka, nilikuwa nakula kawaida sana na Mara nyingi milo miwili kwa siku... yaani in short sikuwa na mambo mengi
boom nililipia ada...kodi ya chumba..kula... Kuvaa...na matumizi mengine kama kutoa copies za notes, Sheria n.k. ninyi ambao mnasave/mlisave huwa mnafanyaje?
 
Sio darasa la saba huyu anatuzingua tu
 
hii ni excuse ya kitoto sana, hakuna hela ambayo haikai, ni wewe wa kuamua ikae au isikae.
ukiweza kuvumilia vijishida vidogo dogo kwaajili ya future yako hakuna kinachoshindikana.
 
tu
likua tunajitesa sana sana sana aisee ili mrdi tu kusave kiasi fulani cha pesa. kula kawaida, mavazi ya kawaida, sometimes shatopori, notes ama tunaazima ila mara nyingi ni kutegemea pdf na slides.
YOTE KWA YOTE HAIKUWA KAZI RAHISI, ILIKUWA NI KWA MACHOZI, JASHO NA DAMU NA MWISHO WA SIKU ILIWEZEKANA.
 
hii ni excuse ya kitoto sana, hakuna hela ambayo haikai, ni wewe wa kuamua ikae au isikae.
ukiweza kuvumilia vijishida vidogo dogo kwaajili ya future yako hakuna kinachoshindikana.
umesoma mpaka chuo kikuu? ulipata mkopo?

skia kijana kila mtu ana familia yake na jinsi anavyo treatiwa na hiyo familia..

kuna watu wazaz wao wakijua una mkopo ndio tayar ushamaliza mkataba nao.

tatz hujawa exposure na mazingira ya aina hiyo sikulaumu kwa upeo wako mdogo wa kung'amua mambo na kupata majibu sahihi
 
Hahaha, ningepata wapi uthubu wa kuchangia nisichokijua mkuu,
ndiyo nmesoma mpaka chuo kikuu (UDSM, nimegraduate 2018, mwaka jana)
ndiyo nilipata mkopo

Yote kwa yote jitahidi kuepuka any kind of excuses, hii itakusaidia sana.
 
Hahaha, ningepata wapi uthubu wa kuchangia nisichokijua mkuu,
ndiyo nmesoma mpaka chuo kikuu (UDSM, nimegraduate 2018, mwaka jana)
ndiyo nilipata mkopo

Yote kwa yote jitahidi kuepuka any kind of excuses, hii itakusaidia sana.
kujifunza hakuna kikomo,endelea kujifunza zaidi hasa somo la Busara litakusaidia
 
Kuna watu tumeamua tukifika tu uko mtaani itajulikana kwa kuwa atuna namna...unakuta mtu ana boom lenyewe then inakulazimu kujilipia ada na direct cost zote bila support yoyote kutoka kwa wazazi....apo still unaangalia na hali ya nyumbani inabidi ufanye chochote apo unatakiwa usave pesa ya field....aya maisha mungu atafanya njia uko mbeleni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…