Mimi pia ni mpenzi wa hizo bagia ila kwa kuzitengeneza mwenyewe si kwa kuzinunua mtaani au kula hotel coz maandaliz yake sijui wanafanyaje zinakuwaga na mchanga sana.Karibu!!!! Bajia Za Kunde
VIPIMO
Kunde za kupaaza 1 ½ Vikombe (hizi kunde kwetu tunaziita (njoombo)
Vitungu vya kijani iliyokatwa katwa ½ Kikombe
Baking soda ¼ Kijiko cha chai
*Bizari mchanganyiko 1 Kijiko cha chai
Maziwa 2 Vijiko vya supu
Chumvi 1 ¼ Vijiko vya chai
Unga wa ngano 2 Vijiko vya supu
Mafuta ya kukaangia
* Unaweza kutumia bizari ya pilau (cummin) ukipenda
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
Osha na kuroweka kunde kwenye bakuli la maji ya baridi usiku mpaka asubuhi.
Saga kwenye mashine (food processor) kisha mimina kwenye bakuli.
Ongeza vitungu, baking soda, masala, maziwa, na chumvi.
Koroga vizuri halafu tia unga kisha uchanganye pamoja.
Fanya vidonge kama nchi moja kisha ukipenda bana katikati ya mikono na kidole katikati ya bajia.
Kaanga kwenye mafuta ya moto mpaka ziive.
Andaa bajia kwenye sahani na chatini uipendayo.
Kwa hapo unaweza kuserve kwa chai, maziwa,juice au chochote unachopenda wewe!!Niliwahi kupost ila nimeshindwa kukutupia ili uone, sasa nimeamua kucopy na kupaste best.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.