Jinsi ya kupika mlenda wa unga

Safi sana hapo full kujilamba.
*Nyongeza:unaweza kutumia maziwa fresh badala ya maji
 
Ndio huu niliouandika,wengine wanauita nswalu.

Unatokana na kutwangwa kwa majani ya maboga na mchanganyiko mwingine sijui wa majani gani
Ni unga unga unaotumika kupika mlenda. Kwa wakazi huenda wanaujua.
 
Nswalu na mkunungu ni vitu viwili tofauti, nswalu inatoka shinyanga, tabora, kahama, singida, nswalu ni kinyiramba na nzubyo ni kisukuma ila mchanganyiko ni huo huo, mkunungu unatoka iringa, ili upate unga wa nswalu kuna majani yapo ya mlenda unaitwa mlenda bata, mlenda wima na mwingine unaitwa wibhela unachanganywa na majani ya limbe zinakaushwa kwa pamoja au kutenganishwa zikikauka unatwangwa unachekechwa tayari kwa matumizi, mwingine unakausha bamia zikiwa zimekatwa katwa na msusa au majani ya maboga zikikauka zinatwangwa tayari kwa matumizi.
ili kupika chota vijiko viwili vya karanga na kijiko kimoja cha chakula cha nswalu weka kwenye sufuria na maji kidogo ili mboga iwe nzito koroga mpaka uwe uji mzito weka chumvi weka mboga koroga vizuri weka jikoni ukiwa mzito ongeza maji kidogo usiwe mgumu sana moto uwe mdogo ili isiungue haraka ikianza kutoa mafuta tayari kajilambe.
 
Asante sana cute. Nimejifunza upishi mpya kwako. Be blessed
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…