Jinsi ya kupika nyama ya ng'ombe ya kuchoma na viazi

Jinsi ya kupika nyama ya ng'ombe ya kuchoma na viazi

Michael Amon

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2008
Posts
8,768
Reaction score
3,622
mbuzi.JPG


Mahitaji

  • Nyama ya ng'ombe ya mafupa bila ya kukatwa (pande kubwa unalotaka)
  • Viazi 4 vya mviringo vilivyomenywa na kukatwa
  • Vijiko 2 vya chakula vya thomu na tangawizi iliyosagwa
  • Kijiko 1 cha chakula cha pili pili mbichi iliyosagwa
  • Kijiko 1 cha chakula cha maziwa ya mtindi
  • Vijiko 2 vya chai vya pili pili manga ya unga
  • Vijiko 2 vya chai vya binzari ya pilau ya unga (Jiyra/cummin powder)
  • Vijiko 4 vya chakula vya ndimu/limao
  • Chumvi kiasi

Jinsi ya kuandaa na kupika

  1. Changanya thomu, tangawizi, chumvi, pilipili manga, pilipili mbichi, mtindi, bizari ya pilau, na ndimu/limao katika kibakuli kidogo.
  2. Ichanje chanje nyama upate kuingiza mchanganyiko huo wa masala, kisha tia kidogo kidogo katika hizo sehemu wazi katika nyama na uroweke pande la nyama kwa muda wa nusu saa.
  3. Baada ya hapo ichukue nyama yako na uiweke katika trei ya kupikia ndani ya jiko (oven). Ifunike kwa jaribosi ya kupikia (foil paper) na ipike katika moto mkali 400º- 450º kwa muda wa saa au zaidi. Inategemea ukubwa wa nyama, ikiwa ni pande kubwa sana zidisha muda wa kupikia.
  4. Nyama ikikaribia kuwiva, vitie viazi chumvi na pilipili manga kidogo na umwagie juu ya nayma na uendelee kupika hadi viazi viwive pia.
  5. Vikishaiva epua na tayari kwa kuliwa.

Nyama hii pia inafaa kwa kuliwa na mkate

Ingawa recipe hii iliombwa na BADILI TABIA lakini nimeona si vibaya kama niidedicate recipe hii na kushare na watu ambao ni wapenzi wa jukwaa hili la mapishi nao si wengine bali ni Lizzy, Kongosho, Amyner, RussianRoulette, sweetlady, afrodenzi, WomanOfSubstance, AshaDii, CANtalicia, FirstLady1, Pretty, Jestina, Kipipi, Kabakabana, Mwali, X-PASTER, shosti, Smile, kisukari na wengine wote hata wale ambao sijawataja
 
Last edited by a moderator:
Youngmaster kumbe wewe ni mtaalam wa mambo mengi,lol kweli am lucky to have you....lol:A S 465:
 
Back
Top Bottom