Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Jukwa la mapishi silioni, ninatamani kuelezea jinsi ya kupika ugali wa mhogo na ukatoka mweupe na si mweusi kama bada tulilo lizoea.
Bada ninapenda sana tena liwe na mboga ya kuku wa kienyeji apikwe chukuchuku. Back to the topic. Mhogo uliochemshwa na kuiva kabisa ukiwa bado wa moto unwekwa kwenye kinu na kupondwa mpaka unatoa ugali.
Ugali huu unapashwa moto kwa steaming, yaani unaufunga kwenye majani ya mgomba. Unabangidasufuria ya maji jikoni, ya kuanza kuchemka unaweka ugali kwenye ungo na kuweka kuu ya sufuria ya maji ya moto. Inafunika ungo na sinia na kuacha upate moto.
Kwa watoto wa .com basi unamenya mhogo na kukata vipande vidogo, unaweka kwenye food processor na maji ya kutosha. Utatoka uji mzito. Uji huu unauweka kwenye sufuria na kuandika kwenye moto. Unakoroka mpaka unashikana kuepuka mabonge. Ukishikana unaanza kusonga ugali mpaka ulainike na kuiva.
Weekend njema.